Waziri wa Fedha amjibu Prof. Lipumba

Waziri wa Fedha amjibu Prof. Lipumba

inawezekana labda hakuna zaidi yake mwaminifu na mwenye uwezo. au anamalizia kipindi. kuweka jembe litatifua plan
 
Kwa hiyi mheshimiwa waziri anafanya internship wizara ya fedha? coz phD ni demanding course, atagawaje muda wake ili kuivusha nchi hii? wizara hii ni nyeti mtu hawezi kwenda kufanyia filed practical au intern.

Afu wote ye na Nchemba bado wapo masomoni shida hii Uncle Sam
 
tatizo elimu kaunganisha unganisha sana, pia elimu za malaysia ubora wake bado sana, alitakiwa awe waziri wa fedha huko huko zanzibar
 
Waziri Mkuya alisema elimu yake wala haina mashaka, alisoma kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Lumumba mjini Zanzibar.
Baada ya hapo, alijiunga na masomo ya diploma ya Biashara katika Chuo cha Stamford cha Malaysia, ambapo pia alichukua diploma nyingine ya biashara nchini Uingereza kwa njia masafa.

pia amesoma shahada ya pili ya biashara katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) na kuhitimu mwaka 2009.
“amehitimu Shahada ya Uzamili ya Utawala na Biashara (MBA) ya Chuo Kikuu cha WATT kilichopo Edinburgh, Scotland.
“Kwa sasa anachukua Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Utawala wa Biashara Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, tawi la Dar es Salaam,” alisema Mkuya.
Hapa kuna kitu, akija yule ndugu Msemakweli Kainerugaba akambana sawa sawa utasikia mtu anatangaza kurudi shule. Akina Nchimbi wanaijua habari yake.
 
Lipumba is absolutely right. Her credentials and experience are questionable.

Further it seems she has been FAST TRACKED to a very senior position in record time. Is it matter of merit or as often is the case a matter of who you know and not what you know?
 
Yaani anaenda kufanyia mazoezi (intern) Wizara ya fedha?Katika wakati huu ambao uchumi wa nchi umedorora kwa kiwango cha kutisha!?

ONLY IN TANZANIA!
 
Akizungumza na MTANZANIA Jumatatu kuhusu madai hayo, Waziri Mkuya alisema elimu yake wala haina mashaka, kwani alisoma kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Lumumba mjini Zanzibar (wala primary na olevel hajasoma)

Baada ya hapo, alijiunga na masomo ya diploma ya Biashara katika Chuo cha Stamford cha Malaysia, ambapo pia alichukua diploma nyingine ya biashara nchini Uingereza (chuo amesahau). hata mwaka pia.

Alisema mbali na masomo hayo, pia amesoma shahada ya pili ya biashara katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) na kuhitimu mwaka 2009. "Nimehitimu Shahada ya Uzamili ya Utawala na Biashara (MBA) ya Chuo Kikuu cha WATT kilichopo Edinburgh, Scotland. (Hapa kapiga double double)

"Kwa sasa nachukua Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Utawala wa Biashara Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, tawi la Dar es Salaam," alisema Mkuya.
Huyu madha huyo nondo...!
 
Hivi lipumba vyeti vyake vimesaidia nini taifa hili make chama chenyewe kimekufa anachokiongoza leo anaanza kugombana na kubishana na watoto wa kike huyu mzee vipi kumbe kuwa na kichwa kikubwa siyo upeo wa mawazo.

Muulize m7 anaelewa uwezo wa Lipumba
 
Prof LIPUMBA

View attachment 135021

Waziri wa fedha amjibu Prof. Lipumba

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amelishushia tuhuma nzito Baraza la Mawaziri, baada ya kudai baadhi ya mawaziri walioteuliwa hawana elimu ya kutosha.

View attachment 135020
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Profesa Lipumba alisema mmoja wa mawaziri hao ni Waziri wa Fedha, Saada Mkuya.

Alisema chama chake, kina wasiwasi na elimu ya Waziri Mkuya, kutokana na wasifu wake kutoonyesha vyuo alivyosoma wakati wa kupata shahada ya kwanza na ya pili katika masuala ya biashara.

Alisema katika tovuti ya Bunge, wasifu wa waziri huyo umeonyesha sehemu aliyosoma elimu ya sekondari na kuhitimu kidato cha sita.

Alisema katika tovuti hiyo, haionyeshi chuo alichosoma shahada ya kwanza ya biashara, ingawa inaonyesha masomo aliyochukua jambo ambalo linatia mashaka uhalali wake kuongoza wizara hiyo nyeti.

“Ukiingia kwenye tovuti ya Bunge, utaona wasifu wake kuanzia elimu ya msingi hadi kidato cha sita na shule alizosoma, lakini kuanzia elimu ya shahada imeonyesha masomo aliyochukua na kupata shahada ya kwanza ya biashara, haionyeshi vyuo, jambo ambalo linatia mashaka,” alisema Lipumba.

Alisema nafasi aliyopewa inahitaji kiongozi mwenye upeo wa hali ya juu, kuweza kupambanua mambo yanayohusu uchumi wa nchi kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za kifedha za ndani na nje ya nchi.

“Napata wasiwasi kama Rais Jakaya Kikwete, aliangalia wasifu wa waziri wake kwa sababu asingeweza kumchagua kushika nafasi kubwa kama hii, wakati vyeti vyake vina mashaka,” aliongeza.

Alisema kitendo cha kumuweka mtu mwenye vyeti vya mashaka, kunaweza kusababisha nchi kuyumba kiuchumi, kuongezeka kwa deni la taifa, kwa sababu uamuzi wake unatokana na ufahamu wake.

WAZIRI AJIBU

Akizungumza na MTANZANIA Jumatatu kuhusu madai hayo, Waziri Mkuya alisema elimu yake wala haina mashaka, kwani alisoma kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Lumumba mjini Zanzibar.

Baada ya hapo, alijiunga na masomo ya diploma ya Biashara katika Chuo cha Stamford cha Malaysia, ambapo pia alichukua diploma nyingine ya biashara nchini Uingereza.

Alisema mbali na masomo hayo, pia amesoma shahada ya pili ya biashara katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) na kuhitimu mwaka 2009.
“Nimehitimu Shahada ya Uzamili ya Utawala na Biashara (MBA) ya Chuo Kikuu cha WATT kilichopo Edinburgh, Scotland.

“Kwa sasa nachukua Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Utawala wa Biashara Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, tawi la Dar es Salaam,” alisema Mkuya.

source: darnewsline.blogspot.com

Yeye ni Professor na atuambie amelifanyia nini Taifa kulisogeza mbele? Hili la kudharau watu kabla ya kuona utendaji ni tabia ya uchoyo wa kielimu!
 
Hivi lipumba vyeti vyake vimesaidia nini taifa hili make chama chenyewe kimekufa anachokiongoza leo anaanza kugombana na kubishana na watoto wa kike huyu mzee vipi kumbe kuwa na kichwa kikubwa siyo upeo wa mawazo.
usiwadhalilishe kina mama mkuu..
 
Prof LIPUMBA

View attachment 135021

Waziri wa fedha amjibu Prof. Lipumba

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amelishushia tuhuma nzito Baraza la Mawaziri, baada ya kudai baadhi ya mawaziri walioteuliwa hawana elimu ya kutosha.

View attachment 135020
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Profesa Lipumba alisema mmoja wa mawaziri hao ni Waziri wa Fedha, Saada Mkuya.

Alisema chama chake, kina wasiwasi na elimu ya Waziri Mkuya, kutokana na wasifu wake kutoonyesha vyuo alivyosoma wakati wa kupata shahada ya kwanza na ya pili katika masuala ya biashara.

Alisema katika tovuti ya Bunge, wasifu wa waziri huyo umeonyesha sehemu aliyosoma elimu ya sekondari na kuhitimu kidato cha sita.

Alisema katika tovuti hiyo, haionyeshi chuo alichosoma shahada ya kwanza ya biashara, ingawa inaonyesha masomo aliyochukua jambo ambalo linatia mashaka uhalali wake kuongoza wizara hiyo nyeti.

“Ukiingia kwenye tovuti ya Bunge, utaona wasifu wake kuanzia elimu ya msingi hadi kidato cha sita na shule alizosoma, lakini kuanzia elimu ya shahada imeonyesha masomo aliyochukua na kupata shahada ya kwanza ya biashara, haionyeshi vyuo, jambo ambalo linatia mashaka,” alisema Lipumba.

Alisema nafasi aliyopewa inahitaji kiongozi mwenye upeo wa hali ya juu, kuweza kupambanua mambo yanayohusu uchumi wa nchi kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za kifedha za ndani na nje ya nchi.

“Napata wasiwasi kama Rais Jakaya Kikwete, aliangalia wasifu wa waziri wake kwa sababu asingeweza kumchagua kushika nafasi kubwa kama hii, wakati vyeti vyake vina mashaka,” aliongeza.

Alisema kitendo cha kumuweka mtu mwenye vyeti vya mashaka, kunaweza kusababisha nchi kuyumba kiuchumi, kuongezeka kwa deni la taifa, kwa sababu uamuzi wake unatokana na ufahamu wake.

WAZIRI AJIBU

Akizungumza na MTANZANIA Jumatatu kuhusu madai hayo, Waziri Mkuya alisema elimu yake wala haina mashaka, kwani alisoma kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Lumumba mjini Zanzibar.

Baada ya hapo, alijiunga na masomo ya diploma ya Biashara katika Chuo cha Stamford cha Malaysia, ambapo pia alichukua diploma nyingine ya biashara nchini Uingereza.

Alisema mbali na masomo hayo, pia amesoma shahada ya pili ya biashara katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) na kuhitimu mwaka 2009.
“Nimehitimu Shahada ya Uzamili ya Utawala na Biashara (MBA) ya Chuo Kikuu cha WATT kilichopo Edinburgh, Scotland.

“Kwa sasa nachukua Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Utawala wa Biashara Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, tawi la Dar es Salaam,” alisema Mkuya.

source: darnewsline.blogspot.com
Haitoshi hata kidogo!! hivi kweli Rais anamchagua huyu junior/mwanafunzi kushika uwaziri!?
Ukiona mtu anaanzia kukumbuka primary school aliyosomea tia mashaka!! ahsante Lipumba!! ualimu wa UDSM umeutumia kunusa ufisadi wa kitaaluma!!
 
Nchi ya kusadikika,

Nchi ya kufikirika!

Tanzaniaaaaaaaa....
 
Hapa mtaani kwangu kwa nyuma ya nyumba yetu kuna jamaa wana Software ya kugushi vyeti vya kila aina na ndio kazi yao, kwahiyo kwa Tanzania watu kua na vyeti vya elimu ya kila aina sio tatizo sana inawezekana! Lipumba tafuta hoja nyingine.

Mkuu Ndallo naomba nipe mawsiliano na hao jamaa kwani nina shida ya cheti fulani, sitanii mkuu!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom