Waziri Simbachawene, usijifanye hujaona mahojiano ya Rose Muhando akilituhumu jeshi la polisi na serikali. Mtendeeni haki, washughulikieni watesi wake

CreativityCode

Senior Member
Aug 8, 2020
158
653
Sina mengi,

Rose Muhando akihojiwa na wasafi TV alitoa tuhuma nzito kwa jeshi la polisi na serikali kushirikiana na watu waliomtesa na kumnyanyasa kiasi cha kukosa pa kushitaki lakini cha ajabu Simbachawene unajifanya hujaona mateso ya huyu dada.

Ni lazima haki itendeke kwa Rose Muhando na watesi wake wote na watu walioko serikalini na jeshi la polisi waliowalinda watesi wakamatwe na kufikishwa mbele ya sheria.

Usijifanye hujayaona mahojiano, nakuwekea hapa.

Mungu awabariki!
 
Aisee!

Mungu hamtupi mja wake!

Ni wakati muafaka watesi wa Rose na washirika wake wachukuliwe hatua stahiki.

Huyo mwimbaji wa Injili aliyeshindwa kumsaidia Rose afahamike,kusudi hata kazi zake zisusiwe iwe fundisho kwa wengine.

Pole sana Rose "Your sun will never set"
 
Sina mengi,

Rose Muhando akihojiwa na wasafi TV alitoa tuhuma nzito kwa jeshi la polisi na serikali kushirikiana na watu waliomtesa na kumnyanyasa kiasi cha kukosa pa kushitaki lakini cha ajabu Simbachawene unajifanya hujaona mateso ya huyu dada...
Unataka akamatwe wewe?

Tanzania mtendewa akilalamikia jeshi la Polisi anakamatwa yeye kama Mwingira.
 
TEJA kama TEJA

Ukisikiliza vizuri story za mateja unaweza tengeneza MOVIE na ikabamba sana.

Ray C
Chid Benz
TID
ZONGO

Na wengine
 
Aisee!
Mungu hamtupi mja wake!
Ni wakati muafaka watesi wa Rose na washirika wake wachukuliwe hatua stahiki.
Huyo mwimbaji wa Injili aliyeshindwa kumsaidia Rose afahamike,kusudi hata kazi zake zisusiwe iwe fundisho kwa wengine.
Pole sana Rose "Your sun will never set"
Kwa Serikali ipi?
 
Itoshe kusema yule hakuwa binadamu, ila kujifanya waliopata madhira ushangae kuwa eti yote haya yatokee usiripoti popote, asemae anamatatizo, kwani nini kingefanyika uenda hali ingeongezeka kuwa mbaya, hamuaminiki kihivyo!
 
huyo rose mhandoo upstair na downstair kote kote hayupo sawa, ngada ilisha mharibu hivyo anaweza kupayuka lolote
 
Sina mengi,

Rose Muhando akihojiwa na wasafi TV alitoa tuhuma nzito kwa jeshi la polisi na serikali kushirikiana na watu waliomtesa na kumnyanyasa kiasi cha kukosa pa kushitaki lakini cha ajabu Simbachawene unajifanya hujaona mateso ya huyu dada...
Sasa hao watesi watajulikanaje bila huyo mwingila kuhojiwa ili awataje?

Anayewajua ni.mwingila sasa polisi watawatafuta wapi wakati mteswa hajasema?

Kabla hujawaza kuandika kaa ufikili unataka kuandika nini.

Simbachawene amesema tuhuma ni nzito hivyo mteswa anatakiwa akatoe hayo maelezo huko police ili hatua zichukuliwe kwa hao waliotaka kumuua.

Sasa wewe unarukaruka unataka nini?

Sina mengi,

Rose Muhando akihojiwa na wasafi TV alitoa tuhuma nzito kwa jeshi la polisi na serikali kushirikiana na watu waliomtesa na kumnyanyasa kiasi cha kukosa pa kushitaki lakini cha ajabu Simbachawene unajifanya hujaona mateso ya huyu dada.
 
Sina mengi,

Rose Muhando akihojiwa na wasafi TV alitoa tuhuma nzito kwa jeshi la polisi na serikali kushirikiana na watu waliomtesa na kumnyanyasa kiasi cha kukosa pa kushitaki lakini cha ajabu Simbachawene unajifanya hujaona mateso ya huyu dada.

Ni lazima haki itendeke kwa Rose Muhando na watesi wake wote na watu walioko serikalini na jeshi la polisi waliowalinda watesi wakamatwe na kufikishwa mbele ya sheria.

Usijifanye hujayaona mahojiano, nakuwekea hapa.

Mungu awabariki!

Nakumbuka hata Marha Mwaipaja alimnanga sana Rose Mhando wakati anayapitia yale mapito.

Shame on Martha Mwaipaja, umoja uko wapi katika kazi ya Bwana!
 
Ukimtazama kwenye mahojiano, kwa makini kabisa, ni wazi tuhuma zote mbaya kuwa alitumia madawa siyo za kweli, bali kulikuwa na watu wanamnyanyasa na kumtesa, lakini hakuwa na sehemu ya kushitaki.
 
Msanii mkubwa kama RM anakosa pa kusema kadhia zake? Huyu ana uwezo wa kuwasiliana na Waziri wa Utamaduni, Waziri Mkuu, RPC, IGP!
 
Back
Top Bottom