Nalipongeza Jeshi la Polisi kwa mtindo wa kuwaita watuhumiwa na kufanya mahojiano kwa njia ya amani

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,013
8,369
Nimeamka na furaha leo nalipongeza Jeshi la Polisi. Mimi sikuwahi kufunguliwa Jalada na kuitwa kwa ajili ya kutoa ushirikiano dhidi ya tuhuma fulani bali niliwahi kupitia JamiiForums, jukwaa kubwa hili lenye watu weredi na manguli kuandika habari ya mambo ya ovyo yaliyokuwa yanafanywa na Askari wa kituo kimoja mkoani Kilimanjaro.

Baada ya kuandika Ile habari, kijana mmoja Afisa wa ngazi ya juu kabisa wa Jeshi la polisi (nadiriki kukiri huyu kijana ana akili na utashi mkubwa kuliko mkuu wake wa kituo) aliniita ofisini kwake in friendly way na kutaka kujua zaidi nilichokiandika na nini maoni yangu dhidi ya utendaji wa Jeshi la Polisi.

It' was e very fantastic moment walah, maana jamaa alinihakikishia ulinzi, kijana wenu nawaambia sikuwaangusha, nilimtemea madini yule Afisa hatimaye akaniunganisha na kijana mwingine Afisa mwenzie. Nae nikamtemea madini dhidi ya uovyo wa polisi wenzake pale mkoani mpaka wilayani.

Nashukuru yule Afisa alinielewa, kilichojiri pale wewe polisi uliyekuwa pale itakuwa shahidi na hata ulipojitizama ukiendelea na tabia hizo itakula kwako.

Kwa ufupi, yote niliyomwelezea yule Afisa ni yale niliyokutana nayo sero yakiwemo mahabusu, kukaa sero zaidi ya mwezi mzima, kunyimwa chakula manyanyaso na matumizi ya lugha zisizo na staha kutoka kwa maaskari wa jinsia ya kike na kiume, vitendo vya Rushwa na mengine mengi.

Kilichonishutua nilipoitwa nikatoe ushirikiano na maoni dhidi ya nilichokiandika, yule Afisa alikuwa tayari ameshapata taarifa zangu nyingi (this means know your client; hii nilijua polisi hawaitumii tunaitumia sisi wafanyabiashara kumbe kuna baadhi ya Maafisa wako very smart.)

Nina declare ya kuwa, yule Afisa kutoka Mwanza (Msukuma) pale Central Moshi, yuko very smart, more than even his boss! Ninasema hivyo maana wote wawili nilikutana nao kwenye scenario mbili tofauti.

Nilipokutana na huyu Msukuma alipima uelewa wangu na kuniitia kijana ambae nae alionekana kuwa very smart, kuanzia kuongea mpaka jinsi ya kuandika maelezo. Mara ya pili nilipoenda kwa bosi wao kwa issue nyingine kabisa, yule boss alimuita kijana ambae masikini ya Mungu mwanzo mwisho wa elimu yake mimi namjua vyema.

Yaani mpaka mtihani wa kidato cha nne yule kijana alipiga ziro maana nilisoma nae kidato kimoja shule moja (sasa hivi eti ni mkaguzi hahahaha hahahah) katika Ile ishu niliwagalaza mpaka wakijiona wako uchi wakaishia vitisho.

Kwa Uzi huu nalipongeza Jeshi la Polisi kwa utaratibu wa kuwaita waarifu kituoni kwa ajili ya mahojiano wakati uchunguzi ukiendelea. Ni jambo zuri, litapunguza mrundikano wa wahalifu magerezani na hata vituoni kwenu.

Iteni watu muwahoji huku mnapiga stori life lisonge, yawezekana mnaowaita msipowatisha watatema madini ya ajabu na nyinyi mtayapeleka kwa Rais nae yatamsaidia maana wanaomzunguka yawezekana wanamdanganya mama yetu kwa masilai yao.

Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom