Waziri Mwigulu, pitia huu uzi wa mwaka 2016 unaweza kukusaidia kupata vyanzo vya mapato kwa ajili ya Bodi ya Mikopo

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,371
Oktoba 31 mwaka 2016, nilipendekeza vyanzo vya mapato kwa ajili ya Bodi ya Mikopo kupitia Jukwaa la Siasa(mada ilihamishiwa Jukwaa la Elimu)ingawa teyari mojawapo ya chanzo mwaka huu mpya wa fedha serikali imekifanyia kazi kwa kukitumia kama chanzo cha kodi(tozo kwenye ving'amuzi).

Wanachokosea serikali ni kila tozo kubeba jina kodi wakati vitu vingine vinapaswa kutozwa tozo kama cost sharing kwenye maeneo yanayogusa watanzania wengi mfano kuchangia gharama za elimu ya juu na huduma za afya.

Kwa mfano, ukiwaambia watanzania tutozo kiasi fulani cha fedha kwenye ving'amuzi kwa ajili ya Mfuko wa Bodi ya Mikopo, walau watu wanaweza kukuelewa na vizuri tozo hiyo ikabeba sura ya cost sharing kwenye elimu ya juu au afya kwani gharama za kusomesha watoto au vijana wetu elimu ya juu inagusa karibu kila familia kama ilivyo katika afya.

Ushauri:Waziri Mwigulu pita huu uzi na ufanyike kazi mapendekezo haya:

- Hivi vinaweza kuwa vyanzo mahususi vya mapato kwa ajili ya Bodi ya Mikopo
 
Back
Top Bottom