Bodi ya mikopo (HESLB) huu mnaofanya ni wizi

Mnyunguli

JF-Expert Member
Dec 21, 2020
1,569
3,906
Waslaaam

Hivi nyie bodi ya mikopo ni kwamba pesa za posho na hela za kuiba huko offisin kwenu zimeisha mpaka mje nje kutuibia watanzania kwa njia ya kutuma maombi ya mkopo(application)

Iko hivi bodi ya mikopo mwaka huu walitangaza kutoa mikopo kwa wanafunzi wa stashahada(diploma), wakatoa na kozi zao pendwa za kusoma ili ukidhi kupata huo mkopo ambazo kozi hizo ni mambo ya ualimu wa math na ict,ualimu veta, afya,madini,kilimo n.k.

Kwanza nianze kwa kusema zoezi lilikuwa na dosari mosi walitangaza kipindi vyuo vyingi vilikiwa vishafunga zoezi la kutuma maombi hapa watu wengi walikosa nafasi vyuo vyao pendwa vya mfukoni, pili can you imagine vyuo vimefunguliwa tangu october leo november 30 karibia watu waanze test 1 ndio wanasema wamemaliza kuchambua majina ya wanufaika sasa unajiuliza hii inakuwaje mtu anaanza kusoma kabla ya kupata mkopo chuo gan watakupokea?? Mienzi miwili mwenzi na wiki kadhaa tangu masomo yaanze ndio unakuja kutoa mkopo seriouly?

Anyway ishu ya msingi hapa ni hiyo list ya vyuo vyao 36 kukosekana chuo cha UDOM na vyuo vengine vyenye hizo kozi zao pendwa na watu wenye vigezo wa vyuo hvyo kupigwa chini.

Hii program ilikuwa na lengo zuri tu ila naona kuna upigaji mkubwa sana unaenda kufanyika kwa maafisa wa bodi ya mikopo na hivyo vyuo vya private.Hapa kuna harufu ya upigaji kwa kuwapa wanafunzi hewa mikopo.

Kwanini wasingetangaza watu watume maombi kwenye vyuo walivyoviorodhesha(vyuo vyao vya mfukoni)? Je, wanaJF huu sio wizi wa kiwaibia watanzania pesa zao za kutuma maombi tsh 30,000 ambazo ukijumlsha na gharama zingine kama verification ya rita na mihuli ya mahakamiani jumla ya gharama inakuwa sio chin ya tsh 70,000.

Aibu kwako Mkurugenzi Abdulazak Badru na watendaji wako.Mmetusumbua mmetutia hasara kumbe mna vyuo vyenu vya mfukoni ambavyo vingi ni private.

Kweli umaskini ni laana .....70k yangu imeniuma sana.

Nipo UDOM hapa naishi maisha Magumu sana kwa ajili yenu.
 
Huu ni uizi kama wizi mwingine na ni udhalilishaji kama wa Babati!Maana ni aibu Tena Bora waseme hakuna mikopo yaani inauma sana.pole mwanangu!
Asante mzee wangu.

Hapa kuna harufu ya upigaji wa fedha za umma kuna majizi yashatoa macho kwenye hizo biliob 48 za serikali.
 
Acha tuu mzee
Mimi mwenyewe wafanyakazi wa serikali wameshanikera kisa tamaa ya hela, hata nikimkuta anashida nitajifikiria mara mbili mbili kumsaidia.
Wanakatisha tamaa na kutufanya tuichukie hii nchi kwa mambo yanayofanyika.
 
Umechelewa sana kuwagundua hao wahuni. Imagine kuna watu wamemaliza makato waliyowekewa kwenye salary slip zao miaka zaidi 5 iliyopita, na bado mwaka huu wameletewa makato mapya yanayoitwa New Loan Board na hao wapuuzi.

Wakiulizwa sababu za kuwakata makato upya na wakati walishamaliza madeni yao miaka kadhaa nyuma, wanatoa sababu za kijinga jinga tu.
 
Poleni vijana.

Mmejaribu kuwaulizia wenzenu upande wa pili Zanzibar kelele zipo?

ZHELB nako hakuna pesa?

Mkurugenzi wenu anasema angalieni majibu kwenye akaunti zenu.

Hataki kutoa orodha kama ile sijui nani scholarship 😂😂🤣🤣
 
Poleni vijana.

Mmejaribu kuwaulizia wenzenu upande wa pili Zanzibar kelele zipo?

ZHELB nako hakuna pesa?

Mkurugenzi wenu anasema angalieni majibu kwenye akaunti zenu.

Hataki kutoa orodha kama ile sijui nani scholarship
Hii nchi kuna watu wanapewa nafasi za juu halafu wanafanya ujinga.
 
Umechelewa sana kuwagundua hao wahuni. Imagine kuna watu wamemaliza makato waliyowekewa kwenye salary slip zao miaka zaidi 5 iliyopita, na bado mwaka huu wameletewa makato mapya yanayoitwa New Loan Board na hao wapuuzi.

Wakiulizwa sababu za kuwakata makato upya na wakati walishamaliza madeni yao miaka kadhaa nyuma, wanatoa sababu za kijinga jinga tu.
Hakuna mtu anayejali na hakuna kitu tunafanya.
 
Back
Top Bottom