Kodi ya mfuko wa saruji ni kielelezo cha udhaifu wa Wizara ya Fedha kutafuta vyanzo vya mapato

LUS0MYA

JF-Expert Member
Aug 4, 2011
862
1,097
Mpaka sasa sielewi wataalamu wa fedha kama kweli wanatumika kusaidia serikali kupata vyanzo bora vya kodi vyenye sifa ya kuitwa kodi.

1. Je, jukumu la kulipa fedha kwa ajili ya mazingira ni la mwenye kiwanda au mlaji? Mwenye kiwanda anahitajika kulipa hii kutoka kwenye faida ya biashara ya mwenye kiwanda sio kwa kuongeza bei ya mfuko wa cementi?

2. Je, wizara haifahamu kuwa serikali kutokana kuwa na miradi mingi ya barabara, afya, elimu na ya kimkakati ndiyo wanunuzi wakubwa wa cementi hivyo ndiyo waathirika wakubwa wa ongezeko la hiyo kodi?

3. Madhumuni ya hiyo kodi itakuwa ni kwa ajili ya utunzaji wa mazingira na kudhibiti athari za uzalishaji wa cement kwanini tufikiri kama chanzo cha kibajeti kwa shughuli nyingine?

4. Wizara lazima itambue umuhimu wa kuhakikisha unafuu wa vifaa vya ujenzi kwa maendeleo ya nchi na watu wake.

5. Tutaendelea kusikia TRA inavunja rekodi ya ukusanyaji wakati huo huo serikali inaonekana ina matatizo ya kifedha na hivyo deni la nje kukua kumbe ni kwa sababu TRA inakusanya kodi kubwa kutoka kwenye serikali yenyewe. Ni wakati muafaka hawa watu wa wizara ya fedha wafikirie nje ya box au rais awaondoe ndani ya box, kuanzisha chanzo cha mapato kikasurvive ndani ya mwaka mmoja ni failure.
 
Back
Top Bottom