TAHLISO wanapaswa kusimama na kupigania haki za Wanafunzi kuhusu Mikopo

Sep 27, 2023
7
23
Naitwa Abdul-Aziz Carter Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM):
download.png
Octoba 20,2023 Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya mikopo (HESLB) Abdul-Razaq Badru aliishukuru serikali kwa kutenga Bilioni 731 kwa ajili mikopo ya wanafunzi 220,376 wa Elimu ya juu, lakini pia alitangaza awamu ya kwanza ya wanufaika wa mkopo (first batch) ambapo alisema Bilioni 159.7 zimetumika kuwanufaisha wanafunzi 56,132.

Taarifa hii inatia mashaka kwa sababu ukiangalia akaunti za wanafunzi (students individual permanent account) maarufu kama SIPA wanafunzi wengi wa mwaka wa 1 wamepata chini ya 20% .

Kiwango cha pesa kilichotengwa (Bilioni 159.7) hakiendani na 20% ambayo wanafunzi wengi wamepewa.

TAHLISO wanapaswa kusimama na kupigania haki za Wanafunzi kwani ndio lengo la kuundwa kwake, Bodi ya mikopo inapaswa kutoa ufafanuzi kwa kuwa Kuna wanafunzi walikua na sifa na vigezo vilivyoainishwa na bodi ya mikopo,licha ya kuweka viambatanisho katika maombi yao bado wamepata chini ya 20% na mwisho serikali kupitia wizara ya Elimu wanapaswa kufanya uchunguzi ili kubaini na kuitafutia suluhu changamoto hii.

=============

UFAFANUZI WA BODI YA MIKOPO: MKOPO UNATEGEMEA NA UHITAJI WA MUOMBAJI KWA ALIVYOOMBA

Mkuu wa Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Tanzania (HESLB), Omega Ngole anafafanua:

“Upangaji wa viwango vya mikopo kwa Wanafunzi wanufaika unatokana na uhitaji wa muombaji kulingana na nyaraka alizowasilisha HESLB wakati wa maombi yake, mfano muombaji akisema ana ulemavu, yatima, historia yake kimasomo n.k inaweza kuchangia kiwango anachotakiwa kukipata.

“Hali hiyo inafanya viwango vitofautiane, kuna makundi yanayopewa kipaumbele mfano yatima, wenye ulemavu au waliofanya vizuri zaidi katika mitihani n.k

"Hao wanaolalamika wanatakiwa kujua kiwango cha mkopo kinatokana na nyaraka zao wenyewe.

"Kiwango cha mkopo hakiwezi kulingana kwa kila Mwanafunzi na ndio maana kila mmoja anaingiziwa fedha kwenye akaunti yake binafsi, hilo ni suala la mtu mmoja mmoja kulingana na mahitaji na ndio maana wapo ambao wamepata mkopo kwa kiwango cha 100%."
 
Naitwa Abdul-Aziz Carter Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM):
View attachment 2788445Octoba 20,2023 Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya mikopo (HESLB) Abdul-Razaq Badru aliishukuru serikali kwa kutenga Bilioni 731 kwa ajili mikopo ya wanafunzi 220,376 wa Elimu ya juu, lakini pia alitangaza awamu ya kwanza ya wanufaika wa mkopo (first batch) ambapo alisema Bilioni 159.7 zimetumika kuwanufaisha wanafunzi 56,132.

Taarifa hii inatia mashaka kwa sababu ukiangalia akaunti za wanafunzi (students individual permanent account) maarufu kama SIPA wanafunzi wengi wa mwaka wa 1 wamepata chini ya 20% .

Kiwango cha pesa kilichotengwa (Bilioni 159.7) hakiendani na 20% ambayo wanafunzi wengi wamepewa.

TAHLISO wanapaswa kusimama na kupigania haki za Wanafunzi kwani ndio lengo la kuundwa kwake, Bodi ya mikopo inapaswa kutoa ufafanuzi kwa kuwa Kuna wanafunzi walikua na sifa na vigezo vilivyoainishwa na bodi ya mikopo,licha ya kuweka viambatanisho katika maombi yao bado wamepata chini ya 20% na mwisho serikali kupitia wizara ya Elimu wanapaswa kufanya uchunguzi ili kubaini na kuitafutia suluhu changamoto hii.
Ina maana baada ya mkurugenzi mtendaji wa bodi ya mikopo kutangaza idadi ya wanufaika wa mikopo kwa awamu ya kwanza kwa sasa tayari kupitia SIPA kila mnufaika ameshafahamu kiasi cha mkopo aliopewa? Maana kuna watu watatu hivi wakifungua kwenye status ya SIPA wanadai inasomeka "congratulations! You application is verified complete. Please wait for allocation process". Au hiyo ndiyo status mpya iliyowekwa baada ya allocation na sasa itakuja kusomeka kiasi halisi alichokopeshwa kila mmoja?
 
Ina maana baada ya mkurugenzi mtendaji wa bodi ya mikopo kutangaza idadi ya wanufaika wa mikopo kwa awamu ya kwanza kwa sasa tayari kupitia SIPA kila mnufaika ameshafahamu kiasi cha mkopo aliopewa?
Yaaah sababu body wanakujaga na document ya majina yote yanakuwa na percent wanazowapatia watu hata kama hela haijaingia bado, lazima ujue kwanza unapewa percent ngapi ndio ujue kiasi kilichobaki utalipa shs ngapi kama kuchangia, mkuu hata hili la percent mnataka liwe siri ? Anyways walichoganya hao madogo wameangalia nani kapewa percent ngapi then wakapiga hesabu zao tena hyo hesabu ni rahis sana man, ndio mana wamekuja ku argue kiivyo sababu kalukuleshen zimepigwa mkuu….
 
Pole sana kizazi kipya mna struggle na bodi ya mikopo na bado mpate elimu magumashi, hatimaye ukose ajira, kwa ushauri vijana jifunzeni kufanya biashara kwa kutumia boom mtaiona kesho yenu njema,
 
Upo sahihi wewe kijana una Akili Sana na utafika mbali katika career yako yakuisemea jamii huwa nakufatilia Sana makala zako na video zako kupitia YouTube
Nipe link au jina la Channel nikamfuatilie , kama ndio huyo pichani basi yuko vizuri nishawahi kuona clip yake moja akiwasemea wanafunzi kuhusu vyuo kutowapa refund zao.
 
Nipe link au jina la Channel nikamfuatilie , kama ndio huyo pichani basi yuko vizuri nishawahi kuona clip yake moja akiwasemea wanafunzi kuhusu vyuo kutowapa refund zao.
Yah kijana yupo smart anatumia Elimu yake vizuri kuwasemea vijana na Taifa kwa ujumla Unajua japo watu wengi hatuelewi kuhusu hii Siri ya kujitoa kwa jamii lakini ndo njia namba yakufika mbali nakuacha Legacy ukimtazama Bob Chacha wangwe , ukamtazama Abdul Nondo , Kumbusho Dawson na n.k wanaishi vzr sana Na kuwa na Legacy kubwa.

Kuhusu link Sina mkuu huwa natazama tu clip zake na makala
 
Wakati vijana Wenzako wakibishana kuhusu Simba na yanga wewe unatumia Elimu yako vizuri na siku unapata uteuzi wataanza kusema unapendelewa

Abdul Nondo wakati anaanza hustle zake ilikuwa hivi hivi ila Sasa hivi anacheza Golf.
 
Shukuruni wengine mmepata, kuna madogo wana one kali wamesoma gavoo na bado bila bila, kupata mkopo hapa bongo ni bahati sana.

chamuhimu pia tuendelee kuwapazia sauti, serikali na vyombo vya usalama viingilie kati kama haki imetendekaa
 
kuna kipindi dogo wali verify application yake kuwa ikopoa asubirie allocation process,later on wakamwabia kakosea sehemu .

bongo nyoso kweli
 
Attachments

  • Screenshot_20231025-210617.png
    Screenshot_20231025-210617.png
    20.8 KB · Views: 16
Jah abless madogo mnaopambania hii mikopo, mtafanikiwa ila mkomae. mikopo mbinde na ajira mbinde vilevile ,ila maza samia anawajali vijana sana
 
kuna kitu bodi hakiko sawa maana first year nilipata tuition fee 400,500/= lakini juzi naingia kwenye SIPA yangu naona wameongeza ada yangu na kunipa asilimia mia na wala nilikua sijawahi saini hiko kiasi kabisa hawako makini na kazi yao
 
Unaharbu mambo hujui tu
 
Back
Top Bottom