Waziri Mulamula: Tanzania kuanza kununua magari Rwanda

Waziri wa mambo ya nje mh Mulamula amesema Tanzania tutaanza kununua magari kutoka Rwanda kwa wale wanaopenda VW

Mulamula amesema hayo baada ya kutembelea kiwanda cha VW huko Rwanda akiwa na mh Rais Samia.

mwishowe ile nchi maskini tuliyoisaidia juzi nineties imekuwa tajiri na muha anapanua bakuli katiba mpya hapana corona uchumi x12 shameeeee
 
Waziri wa mambo ya nje mh Mulamula amesema Tanzania tutaanza kununua magari kutoka Rwanda kwa wale wanaopenda VW

Mulamula amesema hayo baada ya kutembelea kiwanda cha VW huko Rwanda akiwa na mh Rais Samia.

Tatizo wanapenda kuropoka ropoka ili magazeti yawaandike.
Nawahakikishia magari ya Rwanda yatakuwa bei kubwa kuliko kulitoa ujerumani.
Ccm ni mashetani.
Tra watataka kodi if umelitoa japan
 
Aise kwani si tulikuwa na mpango wa kuwa na kiwanda cha kuunda magari na sisi. Ni kwamba ni gharama sana au. Nchi hii yaani waziri mzima anaona raha kuagiza gari kutoka Rwanda wakati tungeweza na sisi unda ya kwetu tukatumia ya nyumbani. Anyway Mungu anihurumie. Tuna viongozi wa ajabu sana yaani
Kwaiyo kiwanda cha nyumbu tukifunge
 
Hatuna shida ya kununua magari kutoka Rwanda, hata kutoka Japan na kwingineko bei ni ndogo tunaweza tatizo kodi za ajabu bandarini.

Labda tuanzisha kiwanda hapa

Mkuu hata tukianzisha kiwanda pale Manzese bado swala la Kodi kwa Tanzania ni Maumivu sana,
Tunazo bidhaa ambazo zinazalishwa hapahapa na viwanda vyetu lakini bei zake zipo juu sana,lakini bidhaa Hizo Hizo nchi Jirani wanachukua hapa na bei kwakule Kwao zipo chini sana.
Mfano:Saruji,Sukari,Mafuta ya Kula,n.k
 
Nchi ambayo haikuwa na political stability enzi hizo inatuuzia magar lakini nchi ambayo ina rasilimali za kila aina haina kiwanda hata kimoja
 
Tanzania shamba la bibi, Rwanda inatushidaje....kwann wao waweze?
Hatuwezi kufanya kila kitu kwa wakati mmoja, na tuna priority zetu kwa sasa, miradi mikubwa ya maendeleo ambayo inakaribia kumalizika. Ikimalizika hiyo miradi, hatuendi kulala kitandani, tutafanya vingine tena na tayari vitakuwa vipo kwenye schedule, Mimi sivijui ila naamimi Mama pamoja na watu wake watakuwa wanavijua.
Ombea kitu kimoja tu kwamba wasitokee tena watu wa kuuhujumu utawala wa Mama mithili ya walivyokuwa wanauhujumu uliopita, halafu come 2030 utaona mambo mazito ambayo Mama atakuwa amefanya
Tumuombee Mungu.........
 
Meanwhile vipuri vyoote vinavyounda magari hayo vinapitia bandari ya DSM na kusombwa na malori yanayopita barabara za Tanzania.
Wabongo tunachonga sana maneno
 
heheeee heee heeeee kumbe imekuwa hivyo tena, nahisi apo tayari tumepigwaaa????
 
Nonsense, nilijua wanaleta kiwanda hapa TZ

Wanasema Wajerumani walitaka kuwekeza Tanzania katika uzalishaji wa magari type ya VW,lakini wakazungushwa wee na taasisi ya uwekezaji nchini mpaka wakakata tamaa, wakaona hisiwe taabu ndio wakakimbilia Rwanda ambako wawekezaji wanapokelewa kwa mikono miwili bila ya urasimu wa kijinga, ndani ya mwezi mmoja kila kitu kinakamilika - Kagame na uongozi wake wako dead serious kwenye masuala haya, akisikia mwekezaji anewekewa kauzibe anawatimuwa kazi wahusika on the spot na kifungo juu.


Mtu ungetegemea walao TTCL ingechangamkia kutafuta wabia wa kuwekeza kwenye ku-assemble simu janja nchini lakini wapi, hawataki kuchakalika Wachina walisha wajengea mkonga wa mawasiliano wa Taifa wamesambaza huduma mpaka nchi jirani wanaona ya nini kuangahika zaidi - ubunifu wa kumfikia the late mzee Mengi, hilo TTCL hawana kabisa!!
 
Back
Top Bottom