Waziri Mkuu Majaliwa, kweli tangu awamu ya tano iingie madarakani gharama za maisha hazijapanda? Kuwa na huruma kwa Watumishi wa Umma

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Ndugu zangu wana JF, majibu ya PM Kassim Majaliwa yanashangaza sana na kutia ukakasi. Majibu aliyotoa kwa mbunge wa Konde kuwa kuongeza mishahara huongez gharama za maisha ni fedheha kubwa kwa watumishi wa umma.

Hivi PM Majaliwa tokea umekuwa waziri mkuu wa Tanzania unataka kusema kuwa gharama za maisha hazijabadilika? Kwamba bei ya sukari ni ileile tangu mwaka 2015?

Vipi kuhusu gharama za matibabu nazo ni zilezile tangu mwaka 2015?

Gharama za kupanga majumba nazo zimepungua kisa tu serikali haijaongeza mshahara?

Mbona mkuu wa kaya alishanukuliwa akisema haongezi mishahara watumishi wa umma sababu anataka akamilishe mambo muhimu kwa taifa? Na akikamilisha ataongeza nyongeza kubwa. Hii ya kudai kuwa serikali inakwepa kusababisha gharama za maisha kuwa juu inatoka wapi?

Ukweli ni kuwa watumishi wa umma hawajapata nyongeza ya mishahara kwa miaka mitano,lakini gharama za maisha zimepanda. Majibu yako PM Majaliwa hayafai na sio mazuri kwa watumishi wa umma.
 
Back
Top Bottom