Waziri Mkuu Majaliwa, kweli tangu awamu ya tano iingie madarakani gharama za maisha hazijapanda? Kuwa na huruma kwa Watumishi wa Umma

Bora ukuje na ID ingine unanichefua.

Nashindwa kabisa kusoma bandiko la watu dizaini ya wewe.
 
Yaani watumishi ni watu wa ajabu sana wanajisahau na viposho vya laki mbili wanauza future ya ndugu jamaa na marafiki zao kisa tamaa ndogo ndogo. Acha tuyapate maumivu
Kwa aina ya ubabe uliotumika kutoka kwa policcm na uvccm walio jipachika jukumu la utiss, hata ungekuwa ni wewe ungekuwa tu mpole! Na usingefanya lolote.

Mbaya zaidi walipozwa na posho nene ya laki tatu na ushee!! Jambo ambalo halikuwa la kawaida. Ukichukulia hiyo fedha haikutoka kwa Mabeberu! . Ilikuwa ni fedha ya ndani kwa maelezo ya mwenye nchi na wapambe wake.

Hii ni taarifa niliyopewa na mtu wangu wa karibu aliyekuwa ni mmoja wa wasimamizi.
 
Kwa aina ya ubabe uliotumika kutoka kwa policcm na uvccm walio jipachika jukumu la utiss, hata ungekuwa ni wewe ungekuwa tu mpole! Na usingefanya lolote.

Mbaya zaidi walipozwa na posho nene ya laki tatu na ushee!! Jambo ambalo halikuwa la kawaida. Ukichukulia hiyo fedha haikutoka kwa Mabeberu! . Ilikuwa ni fedha ya ndani kwa maelezo ya mwenye nchi na wapambe wake.

Hii ni taarifa niliyopewa na mtu wangu wa karibu aliyekuwa ni mmoja wa wasimamizi.
Ndo wanapaswa watulie sasa wasilielie waendelee kula pensheni ya usimamizi wa kura
 
Sisi tumeelewa means hawana pesa za nyongeza, watumishi wafanye kama wametoa sadaka tu.
Cement, mafuta kula,nondo, sukari, vifurushi bei juu lini ulipanda mshahara.
Walitumia uhakiki Kama kichaka cha kuwanyima watumishi haki zao,leo wanajifichia kwenye eti bidhaa zitapanda,kesho corona.
 
Tumhurumie PM!!
Sasa angejibu nini kwa mfano!!
Amefunika kombe!!!
 
Huwezi kuelewa uhusiano wa wizi wa kura na behaviours za viongozi wanaopatikana kwa kura. Utaelewa taratibu. Hapo awali ulikuwa ukitetea hata hili unalolilalamikia kwa sasa.
Jipe muda tu utaelewa, kwani siyo lazima wote tuelewe kwa wakati mmoja.
Ahaaa, kwamba mimi nilitetea watumishi kutokuongezwa mishahara tena kwa sababu zisizo na mashiko kama hizi? Pitia record zako.
 
Mleta mada hajadili masuala ya wizi wa kura.
Jambo la msingi ambalo mchangiaji ametaka ufahamu ni kuwa, kiongoza ambaye amepata madaraka bila ya kutegemea maamuzi ya wananchi, hana hofu ya kutenda au kutotenda lolote, kwa maana anajua hawana uwezo wa kumfanya chochote. Hamkumchagua, ameingia madarakani kwa mbinu zake za kuiba kura, ana sababu gani ya kukufikiria wewe?

Watu watulie, wawe tayari kutendewa chochote kile. Ukitendewa vizuri shukuru sana maana ni kama hisani, ukiumizwa, vumilia kama ulivyovumilia na kukubali kutawaliwa na watu waliojipachika wenyewe, na wakagawana na nafasi kama walivyopanga.

Dalili ni kuwa kuna magumu zaidi yanakuja, endeleeni kuvumilia.

Adhabu ya wenye akili kutokupigania haki, ni kutawaliwa na watu wajinga.
 
Ikiwa wewe chagu wa malunde unalalamika leo. Mbona ulikuwa ukijisikia vibaya haya haya wakikosoa akina Cdm ?! Huu utakuwa ni unafiki. Wakikosoa wapinzani mnawaka Ila ukikosoa wewe tuone kawaida.

Serikali hii ya awamu ya tano, vipaumbele vyake hata nyinyi makada hamvielewi. Na wala masilahi ya wananchi si vipaumbele vyao. Akili ya hao ni jinsi gani watakavyodumu madarakani . Hata kama mshahara usiongezwe . They don't care . Wanavyo vyombo vya dola na vya maamuzi.
Utafiiti wa TWAWEZA uliwrka wazi kuwa wanaoshabikia CCM ni ni watu wajinga. Na hilo lipo dhahiri.

Na wenzao wachache wajanja wanawatumia kama milunda ya kujengea maghorofa. Maghorofa yakikamilika, milunda inatakiwa kutupwa jalalani au kupelekwa kwa mama nitilie waitumie kama kuni.

Wanatakiwa kutulia. Pole Pole amewauliza, wanailewa maV8? Ndizo wao wanaoztumia.
 
Jaduong kukosoa serikali kuwe kwa hoja,je Cdm walikosoa kwa hoja?
Hatima ya Ccm kukaa madarakani ipo mikononi mwa wananchi. Vyombo vya dola haviwezi kuzidi nguvu ya wananchi,masuala madogo kama nyongeza ya mishahara yanarekebishika.
Kama masula ya mishahara ni madogo, yanarekebishika, rekebisheni. Msilete malalamiko hapa.

Kama hujui, kushindwa kurekebisha mishahara ni matokeo ya kushindwa kwa sera za uchumi za Rais Magufuli. Anapenda apandishe mishahara, lakini hawezi. Hatapandisha mwaka huu wala mwaka kesho. Hataweza kutoa bima ya afya kwa watanzania wote mwaka huu wala mwakakeshokutwa. SGR haitafika Mwanza hata baada ya miaka 5. ATCL haitapata faida hata miaka 10 ijayo. Hataweza kutoa milioni 50 kwa kila kijiji milele.

Uchumi ni sayansi, ina kanuni zake. Usipofuata kanuni, hata uwe na mabavu kama kiboko, hutoboi.
 
Kwa aina ya ubabe uliotumika kutoka kwa policcm na uvccm walio jipachika jukumu la utiss, hata ungekuwa ni wewe ungekuwa tu mpole! Na usingefanya lolote.

Mbaya zaidi walipozwa na posho nene ya laki tatu na ushee!! Jambo ambalo halikuwa la kawaida. Ukichukulia hiyo fedha haikutoka kwa Mabeberu! . Ilikuwa ni fedha ya ndani kwa maelezo ya mwenye nchi na wapambe wake.

Hii ni taarifa niliyopewa na mtu wangu wa karibu aliyekuwa ni mmoja wa wasimamizi.
Pesa iliyotumika kuendesha uchaguzi ni pesa ambayo mabeberu waliitoa kwaajili ya kuwasaidia watanzania kupambana na corona. Yeye akaipeleka kwenye uchaguzi, na kuongea uwongo kuwa eti ni pesa yetu ya ndani. Ndiyo sababu, baada ya Bunge la Ulaya, kupata uhakika huo, waliomba taarifa ya pesa yao waliotoa kwaajili ya kupambana na corona, namna ilivyotumika. Mpaka leo Serikali imeshindwa kutoa taarifa ya matumizi.

Serikali yetu inaendesha mambo kwa hadaa.

Utakuwa mjinga hasa kuamini kuwa Serikali hii ina uwezo wa kuboresha mishahara ya wafanyakazi wa umma. Lakini ifahamike pia, imesababisha kupotea kwa ajira nyingi kwenye sejta binafsi, na hata kusababisha maslahi duni kwenye sekta binafsi. Matokeo ya kuua sekta binafsi yatamgusa kila mtu isipokuwa PolePole na wenzake wanaotembelea na maV8.

Maadamu bado kuna watanzania wengi ni wajinga, na ndio hasa wanaoiunga mkono CCM, ni vema kila mmoja akawa tayari kisaikolojia kuishi kwa namna hawa wevi wa kura watakavyopenda.

Suala la uchaguzi unaozingatia maamuzi ya wananchi lilitakiwa kuenziwa na kupiganiwa na kila mwananchi, bila ya kujali upo chama gani. Kama CCM, CJADEMA, ACT, au CUF, wanapata uongozi kwa njia ya hila, wakikengeuka, mimi mwananchi nitakuwa na nyenzo gani ya kumwadhibu?

Magufuli aliharibu uchaguzi kuanzia ndani ya CCM, akajichagulia anaowataka yeye, wanaCCM kimya. Hawa akina Katambi waliopata kura 3 halafu ni wabunge, watamsikiliza mwanaCCM au Magufuli?

Hawa akina Gwajima ambao wamepitishwa na Magufuli kuanzia kura za maoni mpaka kwenye uchaguzi mkuu kwa kura za kwenye mafuko myeusi, bungeni watawatetea wananchi au Magufuli?

Akina Halima, waliopewa ubunge na Ndugai, Ndugai aliyepewa ubunge na uspika na Magufuli, watawatetea nani?

Bunge sasa limejaa watu wa kumtetea na kumpamba Magufuli, wananchi hawana watetezi. Wananchi kika watakachotendewa, kama ni chema, ni kwa hisani ya Magufuli.

WANANCHI HAWANA WAWAKILISHI BUNGENI.
 
Wanasiasa wanawaona watumishi ni bogus tu..

Kura zenu laki 5, hata msipotupigia tutashinda.

Leo wanawaonea huruma kupandishiwa bei. Kweli sukari ianze tu kuwa tshs 4,000 kwa sababu ya mtumishi ameongezewa tshs 8,000?

Hawa viongozi wetu wanaelimu ya wapi?
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom