Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Rais Magufuli ni mzima na anachapa kazi. Wanataka atoke, atoke aende wapi? Kariakoo au Magomeni?

Kwa kipindi hiki vipi mkuu?
Kama ningekuwa na nafasi ya kumshauri Mhe. Majaliwa. ningemwambia anyamaze kuhusu suala la kutoonekana Mhe. Makamu wa Rais. Watanzania bado hatujasahau jinsi alivyotudanganya suala la JPM - kwamba ni mzima na anachapa kazi! Tunatamani Mh Mpango awe ni mzima na anachapa kazi lakini Majaliwa haaminiki. Alishajiptotezea imani kwa watanzania1
 
Hivi, waziri mkuu ndo hua msemaji wa serikali? Na je,anaweza akaamua hivi hivi kutoa taarifa au kuna kamati inakaa ndo inatoa go ahead ya nini kisemwe,nini kisisemwe.

Sidhani kama hata rais mwenyewe ana huo ubavu wa kuamua kusema au kufanya anachokitaka.
Hapo naona anaonewa tu.
 
Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, amewataka watanzania wawapuuze Wapotoshaji wa mitandaoni wanaotaka kuleta taharuki juu ya Afya ya Rais Magufuli "Rais ana shughuli nyingi, Wanataka atoke aende wapi, Kariakoo au Magomeni tangu lini?"

Leo asubuhi wakati nakuja huku nimeongea naye kwa simu na ameniagiza niwaambie wana Njombe kuwa anawapenda sana na anawashukuru sana kwa kura nyingi mlizompigia

Kuna wenzetu hawaishi hapa nchini, wao kazi yao ni kutuombea mabaya tu, kupandikiza chuki tu. Sasa unamuombea mwenzako kufa hiyo ni akili kweli? Nawatoa hofu watanzania, Rais wenu yuko imara anafanya kazi zake kama kawaida za ofisini.

Tuhakikishe tunamuabudu Mungu, tunamuomba Mungu katika kila jambo, tunamtegemea Mungu katika kila jambo, hata asubuhi nilivyokuwa natoka Dodoma nimempigia kumjulisha ratiba yangu, hata juzi alikuwa anajua ninakuja akanituma, wasalimie wana Njombe na nilitoa Salamu.

Naomba nirudie, kwa salam alizotupa leo kweli wana Njombe, mheshimiwa Rais anawasalimia sana wana Njombe, mheshimiwa Rais anawashukuru wana Njombe.

12/03/2021 >>>> 12/03/2024

Leo ni miaka mitatu kamili tangu kauli hii itolewe
 
Back
Top Bottom