Sekta ya Afya na mitatu ya Samia Suluhu Hassan

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Jan 3, 2013
2,161
1,493
Takwimu ziongee, Kila Mtaa, Kijiji, Kata, Tarafa, Wilaya, Mkoa, Kanda na hatimaye Tanzania nzima imefikiwa.

1. Zimejenga nankuendelezwa Hospital Mpya za Halmashauri 127

2. Yamejengwa majengo 83 ya kutolea huduma za dharura na yote yanafanya kazi

3. Zimejengwa nyumba 270 za Watumish wa sekta ya Afya na zote zinatumika ( 3 in 1 then piga mara 270)

4. Zimekarabatiwa zaidi ya hospital Kongwe 50 za Halmashauri.

5. Yamejengwa majengo zaidi ya 28 ya huduma kwa Wagonjwa Mahututi.

6. Vinejengwa Vituo vya Afya vipya zaidi ya 367 na vyote vina Vifaa na Wataalam wa kutosha .

7. Kimejengwa kituo cha kutibu magonjwa ya mlipuko.

8. Maboma ya Zahanati zaidi 880 yamemaliziwa na sasa yanafanya kazi, dawa zipo na Wataalam wapo.

9.Imejengwa mitambo 21 ya kuzalishia hewa Tiba ya Oksijeni.

10. Zimejengwa hospital za Mikoa na Rufaa, hospital za Kanda etc..

11. Yamenunuliwa magari ya kubebea wagonjwa, mgari ya ufuatiliaji etc

12. Watumishi zaidi ya 17,137 wameajiriwa katika kipindi hiki.

13. Watumishi wenye sifa ya kupanda vyeo wamepanda, wale walio kuwa miaka mingi hawajapanda ilipigwa mseleleko.

14. Maelfu ya Watumishi wamepelekwa nje kwenye mafunzo ya umahiri katika Sekta ya Afya..

15. Vifaa vya kisasa kabisa vimenunuliwa katika hospital ya Mhimbili, kwa sasa upasuaji ulio kuwa unafnyika India unafanyika Tanzania .

16. Ndani ya Miaka 3 hii Mataifa mengi yameleta Watalaam wao katika Sekta ya Afua kuja kujifunza Tanzania

17. Itaendelea

Pongezi za dhati kwa Mh. M. Mchengerwa (MMK) na Ummy Mwalimu kwa kumsaidia kwa dhati Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha Afya za Watanzania ziko salama

Mwenyezi Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mungu ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom