Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 12,279
- 10,378
Joint venture ili kumpata mwekezaji wa Bongo. Ndio mtindo wa kisasa Serikali yetu imejiwekea inapoingia kwenye mradi na makampuni ya kigeni.
Sasa hii ndiyo mbaya zaidi. Ikiwa joint venture ni local company na ameshindwa kuwasilisha makaratasi yake ( ikiwa pamoja na power of attorney) inawezekana tenda bodi imeogopa isiwe kampuni yenyewe ni kanya boya. Huu mradi umejaa shutuma kibao kuwa wakubwa wanautaka sana. Kwa nini isiwe imewekwa kampuni kanya boya ili baada ya kuingia mkataba mpira, kampuni hiyo itolewe na iingizwe ambayo ingeingia mwanzo watu wangeona kuwa kuna kamchezo kanataka kufanyika?
Huyo anayedai kuwa hii kampuni imeshinda mradi kwa wadachi, hiyo si hoja. Si wadachi hao hao waliotuletea Aduco watujengee barabara ya Ilala? Tumesahau kilichotokea?
Kama hii tenda bodi iko makini nadhani ni bora wajiuzulu tu ili kuepuka lawama.
Amandla.........