1. Quote: Nyani
Kukosoa kwa mtindo wa kutafuta kasoro bila tact na bila kutoa mapendekezo mbadala hakujengi chochote. Sana sana mtu utaishia kugombana na watu. Uwezekano wa kumkosoa mtu bila kumfanya yeye hajui kitu na kwa kutumia lugha ya kiungwana na si kejeli, upo. Malumbano yanakuja pale mmoja anapotafuta kasoro tu kama vile kuna kitu ambacho hakina kasoro. Hiyo tabia ya kutafuta kasoro kwa watu wengine na yenyewe inaweza ikawa kasoro vile vile. Hata kama mtu una hoja nzuri, unaweza kabisa kumkosoa mwingine kwa kutumia lugha ambayo haitamfanya mkosolewaji ajisikie vibaya. Au naongopa hapa?
2.
Quote: YRSMINE
Acha kuangalia mambo ki-Simba na Yanga buraza....kuHaNI ni nani? ni mwandishi wa habari, mwanasheria, muhasibu, mhandisi, daktari, nesi, mwalimu, injinia au ni nani hasa na kapata wapi hiyo authority ya kukosoa taaluma zote hizo na kila kitu kinachopita usoni pake? Huyo KuHaNi unayemshabikia ndio mpotoshaji nambari wani na ndio hasa mijitu kama yeye ndio mzizi wa fitina ktk maendeleo ya Tanzania......vinginevyo endelea kupiga chapuo!
Kitendo cha wewe kulumbana na FMES kinaonyesha wazi kuwa wewe ni mtu wa aina gani.....wajanja hawalumbani na mukulu FMES!! Kama ulikua hujui basi ndio umeshajua......LOL.
- Ahsante Mkulu Nyani na Mkulu wangu Yoursnameismine, tupo pamoja na kama kawaida tutaendelea kuwa pamoja katika kujaribu kutafuta sotuions za matatizo ya taifa letu, tuinatoka mbali sana na bado safari ni ndefu zaidi kuliko tulikokotoka.
- Masha is my friend, kama mlivyo nyinyi na wengine wengi hapa JF, na ndio maana nimewahi kuwapigania sana wakulu flani hapa walipokuwa mbele ya Pilato, ingawa sijawahi hata kuwaona machoni mwangu hata siku moja. Sasa mind you hata huko nilikokuwa ninawapigania nilirushiwa maneno kama haya ninayorushiwa hapa kwa kutetea ukweli ninaoujua. Ninaifahamu sana backogropund ya Masha, kuanzia elimu yake mpaka kazi zake kabla ya kua Mwanasiasa, sasa nina tatizo kubwa sana na mtu yoyote yule anayetaka kumchafua Masha katika level hiyo ya kabla ya kuingia siasa, na kwenye hili nitamtetea kwa nguvu zangu zote na wakati wowote bila kuogopa anything, kwa sababu Mungu ninayemuabudu anasema kwamba kumjua mwizi ukanyamza, kama ni dhambi inakuwa ni ile ile kwa mwizi na mimi niliyenyamaza, meaning kwamba kuona Masha anashambuliwa na tuhuma za uongo kuhusu elimu yake na kazi zake kabla ya kuingia kwenye siasa halafu nikanyamaza kimya kwa sababu nitaonekana tofauti na popular theme, au kuwaogopa wanaomshambulia, ninakuwa mnafiki mbele ya Mungu wangu ambaye ninamuogopa kuliko anything, kwa wale wanaonijua vizuri sana na kwa karibu sana wanajua kuwa huwa sio tabia yangu kukimbia ukweli, nitatetea to the last drop of my blood.
- Ninampa credit Masha kwa kuweza kulimaliza suala lake na Mengi kistaarabu na sasa ni watu walio karibu sana, ingawa wananchi wengi tusingependa iishie hivyo, lakini it is what it is. Habari za ndani sana nilizonazo kuhusu yeye na vitambulisho sio nzuri sana kwake, lakini kwa vile bado ishu inaendelea bungeni, tutasubiri kujua ukweli wote kwa sababu na yeye sasa amezungumza, tena very confident na ndicho hasa nilichokisema kuwa tunahitaji kusikia his side of this story kabla ya kurusha hukumu.
- Huwa sijali sana yaliyopita, maana kila siku mpya ya Mungu inaleta mapya tena mengi sana mazuri kuliko ya jana, kutoka Jumapili nimeona mashambulizi na nimeyajibu kama ninavyoweza, na given a chance ninaweza kurudia tena exactly the same na zaidi. Sina uhakika sana na moderation iliyofanyika katika hii mada, lakini status yangu hapa na nje ya hapa, inaniweka kwenye nafasi ngumu sana kuwashukia Mods kama nafsi yangu inavyotaka, mimi nikifanya hivyo nitabomoa majengo mengi ambayo nimehusika sana kuyajenga hapa JF, ndio maana huwa ninanyamaza hata ninapokuwa sijaridhika na moderation. Sio lazima kuwepo hapa, lakini ni uchungu wa taifa letu ndio unatuweka hapa, hakuna mwenye uchungu zaidi kuliko mwingine.
- Kuhusu suala la Masha na vitambulisho nimesikia so far side nne za habari, kwanza kwenye media, pili uchanbuzi wa hapa JF, tatu kutoka kwa wajumbe wa kamati ya bunge, na leo side ya Masha, sasa ni zamu ya kulisikia bunge na uchunguzi wake, kwa sababu maelezo ya Masha, yanazi-off balance hoja nyingi zilizotolewa huko nyuma kuhusu kuhusika kwake na hii ishu. Infact leo kuna habari mpya kwamba hiii ishu ni ya Membe na wenzake, ninasema hivi pole pole tutaufikia ukweli wote, unless kutokee mizengwe ya busara.
Tutaendelea kuichambua hii ishu kwa hoja mpaka kufikia ukweli ulipo.
Wazee wa sauti ya umeme - FMES!