Waziri Lukuvi apiga marufuku madalali kulipwa posho ya mwezi mmoja na wapangaji. Asema ni ujambazi

Mara zote Kwenye hii biashara Mpangaji ndiye anamatafuta Dalali kumuomba amtafutie sehemu
Watuache kabisa sisi ma landlords
Basi mimi ni mtakatifu ram, mimi huwa tunachangia nusu kwa nusu landlord na mpangaji :) :) :)
 
Basi mimi ni mtakatifu ram, mimi huwa tunachangia nusu kwa nusu landlord na mpangaji :) :) :)

Kwangu hapana aisee Mimi ninachojali ni kodi yangu tu , ukilinilipa kadri ya makubaliano unahamia .
Dalali utajuana naye wewe mwenyewe ukiweza kumdhulumu sawa .
Kuna Dalali alileta Mpangaji kwangu Dalali mwenyewe hata simjui nadhani alipewa taarifa na madalali wenzake.
Mpangaji akapenda akalipa nikampa funguo akaja kuhamia alikuwa binti.
Siku mbili tatu Dalali ananifata eti nimrudishie yule binti hajamlipa. Atanitafutia mtu mwingine nikamkatalia nikamwambia fedha nishatumia akiweza atafute fedha arudishie yeye apangishe .
Sikumbili tatu nakutana na kale kajamaa kakaniambia yule binti alimpa hela nusu na pia alimpa papuchi so wamemalizana.
Ni kwangu madalali wanajua kabisa sanasana Kama nakujua nimekupa kaziimi mwenyewe umeniletea Mpangaji katoa kodi miezi 6 na kuendelea hata Kama kodi kwa mwezi laki 2 sanasana nampa elfu 10 au 20 ya soda.
Ni madalali wa kitaa siwashobokei kabisa nawapa kazi nawaambia wakichelewa tu natoa kazi mtandaoni hawapati hata shilingi.
Nilishatangaza napangisha sehemu yangu hapa JF na nikapata Mpangaji hakumlipa dalali yeyote .
Sipendi kutumia mitandao kutokana sipendi kujiexpose
 
Ila mpangaji ndio humtafuta dalali ili apate huduma yake na wakati mwengine mwenye nyumba hata hamjui huyo dalali, sasa kwa mazingira hayo iweje mwenye nyumba ndio amlipe dalali?
Malipo makubwa kwa madalali yanaleta madhara ya watu kukosa nyumba au chumba, na wamiliki kukosa wapangaji.
 
Nilikua namaanisha suala la udalali angeongelea hata mkuu wa wilaya au mtendaji ili waziri aangalie yale nyeti zaidi
Hawana uwezo wa kushughulikia mambo nyeti zaidi ya kurukia haya madogo. Hili swala linaumiza watafuta vyumba, lakini si la ngazi ya kushughulikia na waziri. Matokeo ndio miaka 60 ya uhuru mkuu wa nchi anaongelea madawati, madarasa, vyoo vya shule, visima vya maji, mikopo ya wanafunzi heslb nk.
 
Kwani lile la Wapangaji wasilipishwe kodi ya zaidi ya mwezi mmoja lilishapata ufumbuzi?.
Tatizo ni matamshi ambayo wakati mwingi hayana msingi wa kisheria. Matokeo ni washikwao inakuwa ni ulaji kwa polisi kwani hayapelekwi mahakamani. Rejea katazo la Magufuli kufungua bar mchana, sikuwahi sikia aliepelekwa mahakamani.
 
Wapangaji ndio huenda kuwaomba madalali wawatafutie nyumba za kupanga Sasa unataka mwenye nyumba amlipe kwa lipi?

Wewe unaenda kuomba huduma ya dalali halafu eti ohh mwenye nyumba amlipe kwa lipi wakati mkataba wa kikazi Ni wewe mtafuta nyumba ya kupanga mumeingia na dalali wako uliyemkuta kijiweni au popote kuwa nitafutie nyumba.Wewe ndio umlipe kwa hiyo huduma aliyokupa

IIeleweke wazi contract ya kikazi ya kutafuta nyumba Ni yako wewe na dalali wako sio mwenye nyumba

Waziri alivyoliweka haliko sawa kisheria .Watu wanaenda wenyewe kwa madalali kwa hiari yao bila shuruti na kuingia mikataba nao ya kutafuta nyumba at a fee of course ambayo Ni Kodi ya mwezi mmoja
Vyovyote ilivyo tukubaliane kuwa haiko kisheria na sasa tunahitaji utaratibu mzuri utakaolinda wateja wote wa pande mbili. Huduma ya kupanga ni kubwa mno iko kila mahali penye jamii ya watu.
 
Back
Top Bottom