Je, Serikali imeamua kulea utapeli wa Madalali? Dhima ya kuwasajili iliishia wapi?

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Utapeli kwa katika ununuzi wa vitu au upangishaji wa nyuma unazidi mno kwa kipindi hiki hususan katika upangishaji wa nyumba, imefikia hatua Dalali anakuwa na Mwenye Nyumba wa mchongo na akaunti ya benki ya kitapeli kulipia pango. Serikali hebu saidia Wananchi katika hili.

Nakumbuka Lukuvi alivyokuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliahidi ya kuwa Madalali watatambulika kwa kupewa Vitambulisho maalumu na watakuwa wanajisajili, hili limeishia wapi? Au ndio kila Kitabu na zama zake? Kwamba alivyotoka Wizarani ajaye hayamuhusu anaanza na yake? Kama ndivyo nchi hii kuendelea itakuwa ngumu sana hususan kwa kipindi hiki ambapo Viongozi wanabadilishwa kila uchwao.

Au Serikali kwa namna moja au nyingine inanufaika na utapeli huu? Kwanini vitu vidogo namna hii kusaidia Wananchi inakuwa shida? Leo ndugu yangu alikuwa aliwe zaidi ya milioni 3 katika ulipaji wa pango kupitia namba ya akaunti aliyopewa na dalali na mwenye nyumba wa mchongo, jirani msamaria mwema ndio kamuokoa.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na makazi tafadhali fanyia kazi suala hili, kuwe na utaratibu mzuri wa kutambulika kwa hawa madalali na utambulisho mzuri wa namna watakavyopata commission yao.

Japo hata hapo kwenye commission Lukuvi alivyokuwa Waziri alisema ni ujambazi na kupiga marufuku Madalali kudai fedha hiyo kwa Wapangaji, lakini vyote hivi vimeendelea kama kawaida bila ya kuwepo mwongozo wowote ule. Ama kweli Serikali yetu ni Serikali ya matamko tu? Inang’ata pale ambapo itajilinda yenyewe ila sio pale itakaposadia Wananchi!

Nawasilisha.

Pia soma;
Serikali: Madalali kupewa vitambulisho maalumu kwa Ada ya tsh 20,000. Dalali atalipwa na mwenye nyumba tu siyo Mpangaji


 
Mwenye nyumba ama mwenye mali ndiye anastahili kumlipa dalali kwasababu katafutiwa mteja!!
 
Back
Top Bottom