SoC03 Madalali wa Nyumba Kikwazo kwa Wapangaji

Stories of Change - 2023 Competition

fipa queen

New Member
May 3, 2023
1
1
Utangulizi: MADALALI WA nyumba ni watu maalumu wanaoingia makubaliano na mmiliki wa nyumba kwa ajili ya kutafuta wapangaji. Katika makubaliano hayo mpangaji atatakiwa amlipe dalali pesa ya kodi ya mwezi mmoja na kisha kulipa kodi ya kawaida ya nyumba kwa mwenye nyumba kulingana na makubaliano ya muda wa kulipia, kama ni mwezi mmoja, miezi mitatu au miezi sita mpaka mwaka na kuendelea.

Madalali wanasaidia sana katika kuwafanya watu wapate nyumba za machaguo yao, lakini kikwanzo kinaanzia pale ambapo mpangaji ukishaipenda nyumba unatakiwa umlipe kwanza dalali pesa ambayo ni sawa na kodi ya nyumba hiyo ya mwezi mmoja ndipo uruhisiwe kumlipa mwenyenyumba na uanze kuishi kwenye nyumba hiyo. Hali hii inamuuimiza sana mpangaji kwasababu ukiangalia katika uhalisia unapomtafutia muuzaji (mwenyenyumba) mteja (mpangaji) akaipenda bidhaa na kuinunua anamlipa muuzaji kisha muuzaji ndo anatakiwa akulipe kwa kumletea mteja.

Kama mtafutaji wa mteja wako akipandisha bei lazima mteja atashindwa kununua, na ndicho kinachowatokea wapangaji wengi kwasababu wamekuwa wakishindwa kupata nyumba zinazokidhi mahitaji yao kwaajili tu ya kodi ya mwezi mmoja inayotakiwa ilipwe kwa dalali. Kwa mfano mpangaji anataka chumba cha elfu sabini na pesa aliyonayo ni ya miezi sita kamili, hapo anapata mawazo ni wapi atapata shilingi elfu sabini nyingine ya kumlipa dalali ili aweze kumpa chumba, badala yake inamlazimu kupanga chumba cha shilingi elfu sitini kinyume na mahitaji yake ili tu kupata elfu sitini nyingine ya kumlipa dalali.

Mbali na kumlipa dalali kiasi hicho cha pesa lakini pia utatakiwa umlipe pesa ya kukupeleka kuona nyumba ya chaguo lako ambapo kila dalali ana kiasi chake cha pesa, Kuna wengine ni shilingi elfu tano, elfu kumi mpaka elfu ishirini.

Kuna wakati serikali chini ya waziri wa nyumba na makzi Mh. William Lukuvi iliingilia kati swala hili la madalali na wakapigwa marufuku kuwepo, lakini halikutiliwa mkazo sana kwani waliendelea kuwepo na mpaka sasa bado wapo na ukandamizwaji wa wapangaji unaendelea.

Mwisho kabisa, sikatai kwamba madalali wanasaidia katika kuwafanya watu wapate nyumba za machaguo yao lakini swala la malipo yao ya kwamba ni nani awalipe kati ya mwenyenyumba au mpangaji linatakiwa kuangaliwa upya na kwa maoni yangu ningependa kuishauri serikali ilitilie mkazo swala hili na iunde sheria itakayowapa haki wapangaji, ili mwisho wa siku mtu aweze kuishi kwenye nyumba ya gharama aliyonayo.
 
Back
Top Bottom