Waziri Lukuvi apiga marufuku madalali kulipwa posho ya mwezi mmoja na wapangaji. Asema ni ujambazi

Shida huwa wanaishia kuongea tu lakin hakuna ufuatiliaji!
ni Lukuvi huyuhuyu aliagiza wakurugenzi kutoa vibali vya ujenzi ndani ya wiki moja lakinmpaka sasa bado kuna usumbufu kwenye viali hivyo!
ni Lukuvi huyuhuyu aliagiza wakurugenzi kuwalipa fidia wananchi wote ambao miradi imewafuata kwenye ardhi zao , lakini hakuna utekelezaji wowote!
So wakati mwingine hata wanaoagizwa wakimsikia wanampuuza tu!
 
Waziri wa Ardhi, William Lukuvi amepiga marufuku Madalali kuwadai Wapangaji Fedha ya Mwezi Mmoja, akiita kitendo hicho kuwa ni ujambazi.

Amesema, "Kuna baadhi ya Madalali wanapangisha nyumba halafu wanachukua kwa Wapangaji Kodi ya mwezi. Hawa wanaochukua pesa za wapangaji waache mchezo huo kwasababu ni wizi wa mchana kabisa. Wewe umeajiriwa na mwenye nyumba, yeye lazima akulipe wewe"

View attachment 2011900

anakurupuka, angelifanyia utafiti hili swala kujua namna ya kulitatua, sio kusoma maoni ya Mange na kukurupuka kutoa matamko.
 
Waziri wa Ardhi, William Lukuvi amepiga marufuku Madalali kuwadai Wapangaji Fedha ya Mwezi Mmoja, akiita kitendo hicho kuwa ni ujambazi.

Amesema, "Kuna baadhi ya Madalali wanapangisha nyumba halafu wanachukua kwa Wapangaji Kodi ya mwezi. Hawa wanaochukua pesa za wapangaji waache mchezo huo kwasababu ni wizi wa mchana kabisa. Wewe umeajiriwa na mwenye nyumba, yeye lazima akulipe wewe"

View attachment 2011900
Hiyo ni amri iliyofeli kama ile ya kuondoa Machinga ilivyofeli. Ukileta huo utaratibu watu hawatapata nyumba. Ujuwe 99% ya wafanyakazi wa serikali ni wateja wa wenye nyumba na madalali. Dawa ya huo ugonjwa ni serikali kujenga nyumba nyingi na kuwakopesha wasio na nyumba (ipigwe marufuku kwa aliye na nyumba tayari kununua nyumba hizi vinginevyo ataifishwe). Mandela aliweza huu mpango (alivyomuachia Mbeki akashindwa kuuendeleza), Abeid Karume aliweza mpango huu pia (waliofuata wakautelekeza). Waziri Lukuvi anatakiwa aufishe mzimu wa NHC kujenga nyumba za bei nafuu na kuwauzia matajiri kwa bei kubwa ambayo masikini hawezi. NHC inawauzia matajiri nyumba ambao tayari ni makabaila wa majumba. Serikali yenyewe iliuza nyumba za wafanyakazi alizojenga Mwl Nyerere na uuzaji huo ulipendelea wafanyakazi wenye mapato makubwa kazini na wengine wakanunua na kuwauzia matajiri tena kwa bei kubwa. Wapo wafanyakazi wa chini ambao uamuzi huu ulipotangazwa na serikali mabosi wao wakawaondoa kwenye nyumba hizo na wao kuzinunua. Mashirika ya umma pia yalifanya biashara hii haramu yakiwemo Bandari, Reli, Bima, NDC, Sigara, Msajili wa Majumba, ATC, Mifuko ya Hifadhi za Jamii nk nk. Serikali ifanye sensa ya majumba nchini kubaini wamiliki wake na nyumba za bei nafuu zikijengwa basi waangalie kwenye orodha ya sensa hiyo ili wauziwe wale tu ambao bado hawana nyumba (ambao hawamo kwenye hiyo orodha). Nadhani Waziri ajipange arudi kiupya.
 
Hawalipi,
Labda wale wenye leseni
Kama kina yono na majembe

Hawalipi,
Labda wale wenye leseni
Kama kina yono na majembe
Tanzania ni rahisi sana kutajirika. Imagine madalali wenyewe tu wakajipangia jinsi ya kutengeneza pesa. Na wanapata kipato ambacho hawalipii kodi ya serikali. Imagine kodi za million moja kwa mwezi. Anadalalisha nyumba kumi. Na kateka sehemu nyingi. Ndo maana page za madalali ni nyingi Instagram.
 
Waziri wa Ardhi, William Lukuvi amepiga marufuku Madalali kuwadai Wapangaji Fedha ya Mwezi Mmoja, akiita kitendo hicho kuwa ni ujambazi.

Amesema, "Kuna baadhi ya Madalali wanapangisha nyumba halafu wanachukua kwa Wapangaji Kodi ya mwezi. Hawa wanaochukua pesa za wapangaji waache mchezo huo kwasababu ni wizi wa mchana kabisa. Wewe umeajiriwa na mwenye nyumba, yeye lazima akulipe wewe"

View attachment 2011900
Kauli hii haitasaidia chochote Tz ni nchi ambayo ina misingi mibovu sana, sasa kama dalali hatapewa posho na mpangishaji nani atajua? dalali akijua hatakuwa na posho mwisho wa mwezi na yeye kweli atakuonyesha chumba au nyumba?
 
Hiyo ni amri iliyofeli kama ile ya kuondoa Machinga ilivyofeli. Ukileta huo utaratibu watu hawatapata nyumba. Ujuwe 99% ya wafanyakazi wa serikali ni wateja wa wenye nyumba na madalali. Dawa ya huo ugonjwa ni serikali kujenga nyumba nyingi na kuwakopesha wasio na nyumba (ipigwe marufuku kwa aliye na nyumba tayari kununua nyumba hizi vinginevyo ataifishwe). Mandela aliweza huu mpango (alivyomuachia Mbeki akashindwa kuuendeleza), Abeid Karume aliweza mpango huu pia (waliofuata wakautelekeza). Waziri Lukuvi anatakiwa aufishe mzimu wa NHC kujenga nyumba za bei nafuu na kuwauzia matajiri kwa bei kubwa ambayo masikini hawezi. NHC inawauzia matajiri nyumba ambao tayari ni makabaila wa majumba. Serikali yenyewe iliuza nyumba za wafanyakazi alizojenga Mwl Nyerere na uuzaji huo ulipendelea wafanyakazi wenye mapato makubwa kazini na wengine wakanunua na kuwauzia matajiri tena kwa bei kubwa. Wapo wafanyakazi wa chini ambao uamuzi huu ulipotangazwa na serikali mabosi wao wakawaondoa kwenye nyumba hizo na wao kuzinunua. Mashirika ya umma pia yalifanya biashara hii haramu yakiwemo Bandari, Reli, Bima, NDC, Sigara, Msajili wa Majumba, ATC, Mifuko ya Hifadhi za Jamii nk nk. Serikali ifanye sensa ya majumba nchini kubaini wamiliki wake na nyumba za bei nafuu zikijengwa basi waangalie kwenye orodha ya sensa hiyo ili wauziwe wale tu ambao bado hawana nyumba (ambao hawamo kwenye hiyo orodha). Nadhani Waziri ajipange arudi kiupya.
Waziri Lukuvi hajajuwa huu ujambazi vizuri kumbe! Anashangaa ela ya kodi ya mwezi mmoja kupewa dalali wakati madalali wanachukuwa ela hiyo kwa kila mkataba unavyokuwa renewed hadi atakapohama mpangaji, Baghosha!
 
Yaan ina maana waziri kwa miaka zaidi ya 15 aliiuwa hajui kama madalali wana pokea iyo kodi ya mwezi mmoja hii ni kwelii ? Binafsi siamini hata kidogo
 
Waziri wa Ardhi, William Lukuvi amepiga marufuku Madalali kuwadai Wapangaji Fedha ya Mwezi Mmoja, akiita kitendo hicho kuwa ni ujambazi.

Amesema, "Kuna baadhi ya Madalali wanapangisha nyumba halafu wanachukua kwa Wapangaji Kodi ya mwezi. Hawa wanaochukua pesa za wapangaji waache mchezo huo kwasababu ni wizi wa mchana kabisa. Wewe umeajiriwa na mwenye nyumba, yeye lazima akulipe wewe"

View attachment 2011900
Nampenda sana huyu waziri nilitamanigi awe waziri mkuu. Madalali kwl ni majambazi yanavuna bila kupanda. Yapo ktk kila biashara. Hapa Arusha yapo kwenye biashara ya kila zao, yapo kwenye biashara ya materials za ujenzi kama mchanga, kokoto, kwarukwaru n.k Yapo kwenye matunda kila eneo la biashara. Na yana roho mbaya za kikatili yamejaza matumbo bila kufanya kazi huku mkulima akikondeana. Serikali hakuna jambo linashindwa kufanya waondolewe wakafanye kazi siyo kuvizia mali zilizotolewa jasho na wenzao. Serikali iweke masoko ya uhakika na yasimamiwe na vyombo vya dola asionekane dalali. Nawachukia sana lijitu linakua kupanga bei ya bidhaa za mwenzake. Serikali iwaunganishe wenye mali zao na wanunuzi kupitia masoko maalum yaliyoko maeneo yanayojulikana.
 
Waziri wa Ardhi, William Lukuvi amepiga marufuku Madalali kuwadai Wapangaji Fedha ya Mwezi Mmoja, akiita kitendo hicho kuwa ni ujambazi.

Amesema, "Kuna baadhi ya Madalali wanapangisha nyumba halafu wanachukua kwa Wapangaji Kodi ya mwezi. Hawa wanaochukua pesa za wapangaji waache mchezo huo kwasababu ni wizi wa mchana kabisa. Wewe umeajiriwa na mwenye nyumba, yeye lazima akulipe wewe"

View attachment 2011900
NIJAMBO JEMA ILA KUHUSU 150,000tsh TULIZO LIPISHWA TOKEA MWAKA JANA ILI TUPEWE HATI ZA VIEANJA VYETU KWANI IMEKUWAJE TENA!?
 
Waziri wa Ardhi, William Lukuvi amepiga marufuku Madalali kuwadai Wapangaji Fedha ya Mwezi Mmoja, akiita kitendo hicho kuwa ni ujambazi.

Amesema, "Kuna baadhi ya Madalali wanapangisha nyumba halafu wanachukua kwa Wapangaji Kodi ya mwezi. Hawa wanaochukua pesa za wapangaji waache mchezo huo kwasababu ni wizi wa mchana kabisa. Wewe umeajiriwa na mwenye nyumba, yeye lazima akulipe wewe"

View attachment 2011900
Sawa je serikali imeweka njia gan mbadala ??bado adi sasa Kama unahitaji nyumba ya kupanga au chumba utapitia kwa dalali tu unless kama serikali itaweka utaratibu mzuuri yaani wenye nyumba za kupanga wote wapeleke taarifa za nyumba zao na gharama zake ofisi ya serikali ya mtaa mtu ukifika ofisi ya serikali ya mtaa ni kuchagua nyumba unayoitaka kuepuka madalali nadhan pia serikali itajipatia kipato ni kuwekwa mfumo mzuuri tu tatizo serikali yetu akili ndogo inatawala akili kubwa..
 
Hebu tumuelewe Dalali huyu
Sheria haipo kumbe na kwanini isiwepo?
IMG_3186.jpg
 
Haya ndio mambo tunataka kama serikali.
Wapangaji ndio huenda kuwaomba madalali wawatafutie nyumba za kupanga Sasa unataka mwenye nyumba amlipe kwa lipi?

Wewe unaenda kuomba huduma ya dalali halafu eti ohh mwenye nyumba amlipe kwa lipi wakati mkataba wa kikazi Ni wewe mtafuta nyumba ya kupanga mumeingia na dalali wako uliyemkuta kijiweni au popote kuwa nitafutie nyumba.Wewe ndio umlipe kwa hiyo huduma aliyokupa

IIeleweke wazi contract ya kikazi ya kutafuta nyumba Ni yako wewe na dalali wako sio mwenye nyumba

Waziri alivyoliweka haliko sawa kisheria .Watu wanaenda wenyewe kwa madalali kwa hiari yao bila shuruti na kuingia mikataba nao ya kutafuta nyumba at a fee of course ambayo Ni Kodi ya mwezi mmoja
 
Sawa na mtu anayeenda nyumba ya faragha na mwenzi wake wakimaliza wanamwambia mhudumu wa nyumba hiyo aende alipwe na mwenye nyumba hiyo ya starehe.
 
Sawa je serikali imeweka njia gan mbadala ??bado adi sasa Kama unahitaji nyumba ya kupanga au chumba utapitia kwa dalali tu unless kama serikali itaweka utaratibu mzuuri yaani wenye nyumba za kupanga wote wapeleke taarifa za nyumba zao na gharama zake ofisi ya serikali ya mtaa mtu ukifika ofisi ya serikali ya mtaa ni kuchagua nyumba unayoitaka kuepuka madalali nadhan pia serikali itajipatia kipato ni kuwekwa mfumo mzuuri tu tatizo serikali yetu akili ndogo inatawala akili kubwa..
Nadhani serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi iajiri Madalali wote nchini wawe wafanyakazi wa serikali ili kazi yao iwe ni hiyohiyo ya kudalalisha majumba, viwanja na mashamba kwa malipo ya mshahara wa mwezi kama wafanyakazi wengine wa serikali ila kamisheni wanayopokea kwa ama landlord au client waiingize kwenye hazina ya serikalini. Dalali anaweza kuingiza serikalini dola 10,000 ama za pango la nyumba Oysterbay, shamba, godown, kiwanja, kiwanda, equipment nk lakini mshahara wake wa mwezi ukawa ni 5K (lakini ana job security, pensheni, bima, mafao nk).
 
Back
Top Bottom