Waziri Bashe hakutakiwa kuukataa msaada wa mchele kutoka Marekani na kama alikuwa na mashaka yoyote angewatumia TBS

Marekani sio wajinga kutaka kuwamaliza Kwa mbinu za kishamba hivyo. Huo mchele ni salama 100% hawawezi kutumia kitu ambacho kitaacha alama mwilini mwako
Ndo maana nasema Watz huwa hatuna hoja sisi tunarushwa kama maharagwe
 
Waziri bashe ni mchanga sana kidiplomasia na hajui namna dunia inavyoendeshwa. Huwa anajifanya mjuaji lakini kichwani ni mweupe kama theluji.

Hivi wazungu wana shida gani ya kuwaua waafrika kupitia kwenye chakula wakati tayari tumeishajiua wenyewe? Bashe anapswa kufahamu kuwa chanjo zote zinazotumika hapa nchini zimetoka Marekani. Kama wamarekani wangekuwa na nia ya kutuua sisi waafrika (maiti) wangekwisha fanya hivyo kitambo kupitia chanjo na misaada mingine waliyowahi kutuletea.

Huyu msomali amelewa madaraka. Ni wakati muafaka sasa Rais Samia amteue mtanzania kuongoza wizara ya kilimo. Msomali kafeli big time.
Ahsante sana, kumbe kuna watu wenye busara kama wewe wapo nchini, wewe ni IQ kubwa, hao wanaobisha wana usiwalaumu ndiyo kikomo chao. Hawa watu huwa hawajui kuwa hata hao wazungu 90% hawajui neno Tanzania. Muulize Trump neno Tanzania wala hawezi kupoteza muda. Kuna watu wana vichaa hizi nchi zetu. Watu kwenye AI wanacompete kwenda mars halafu wafikirie kuwaua Tanzania? Dawa zote za ukimwi zinatolewa na hao hao ili tusife mbona hamkatai? Budget yenu nayo iko subsidized na wao mbona hamkatai? Midomo mirefu vichwa vitupu! Shenzi taipu
 
Mada hii ni kuelezea mashaka makubwa niliyonayo kwa Waziri wetu wa kilimo namna maamuzi yake yanavyoweza kuharibu mahusiano ya kimataifa kama asipojirekebisha.

Kwanza kabisa nianze Kwa 'declare interest' ,Sina mahusiano ya aina yoyote na NGO iliyoleta mchele wa msaada wenye virutubisho kutoka nchini Marekani chini ya kampeni ya wizara ya kilimo ya Marekani inayoitwa "Pamoja tuwalishe" na 'interest' pekee niliyonayo ni Kwa maslahi mapana ya nchi yangu .

Siku zote mjumbe hauawi na hiyo NGO inabaki kuwa ni mjumbe tu wa wizara ya kilimo ya Marekani ,kitendo Cha Waziri kuonesha kukasirishwa na kitendo Cha mjumbe kinaleta picha isiyopendeza.

Kwa mtazamo wangu badala ya Waziri Bashe kuonesha kukasirishwa na kuletwa Kwa mchele na hiyo NGO angetumia nafasi hiyo kufanya "formal communication" na wizara ya kilimo ya Marekani juu ya mambo tunayohitaji.

Kwa kuwa mchele huo ni msaada sikuona ulazima wowote wa Waziri kusema kwamba mchele tunao ,Kwa kuwa lengo la kampeni hiyo ni zuri ,tunatakiwa kuupokea msaada huo na kushukuru na wizara ingetumia TBS kuchunguza ubora wa mchele huo kimya kimya kabla haujaanza kutumika na kama kungekuwa na mashaka yoyote Serikali ingekataa baada ya kufanyika Kwa uchunguzi na ubora na sio Kwa hoja za Waziri.

Mashaka niliyonayo kwa Waziri Bashe ni kuwa:

Kama Waziri hajui athari za kimahusiano zinazoweza kuibuka kutokana na kauli tu. Kitendo Cha Waziri Bashe kudai Kwa nini wasingeleta virutubisho wachanganye tukiwaona ,sio rafiki Kwa afya ya diplomasia. Kitendo hicho kinaweza kufikirika kama tuhuma ya usalama. Kabla ya kauli hiyo alitakiwa kuwatumia TBS kuuchunguza mchele.

Marekani ni Moja ya nchi zinazozalisha nataka ( mchele na mahindi) Kwa wingi duniani na kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa ,nchi yetu inaweza kukumbwa na baa la njaa na tukahitaji msaada wa Chakula kutoka nje. Je, tutapata wapi nguvu za kuomba msaada kutoka Marekani kama tumeamua kukataa msaada Sasa ?

Pengine kulikuwa na Cha zaidi ambacho hatukijui lakini kama ni hiki kilichopo ,ni vema Waziri Bashe angeliendea suala Hilo Kwa busara, angejiridhisha kwanza na angejua hatua Kwa busara ili tuendelee kuimarisha mahusiano na nchi nyingine.

Kila siku Rais anasisitiza mifumo kusomana ili kuepusha migogoro , na kama mifumo ingekuwa inasomana kusingekuwa na kauli za namna Ile kutoka Kwa Waziri.

Ahsante
Kwa hiyo ameukataa?? kwa hiyo hatupati tena msaada wa huo mchele wa Marekani?

Lakini kuna mambo yanayochekesha kama siyo kufurahisha, ndiyo maana Raisi Trump aliwahi kusema waziwazi kuwa Africa inahitaji kutawaliwa tena. Hivi kati ya Africa na Marekani ni nani anayestahili kumsaidia mwenzake Mchele??

Marekani kule kila sehemu karibu ardhi yote inakaribia kutawaliwa na majengo na barabara, Ardhi ya kilimo ni ndogo sana ukilinganisha na Africa, lakini cha kushangaza wao tena ndyo wanaotusaidia sisi chakula kama huo mchele. Poor Africa
 
Hivi huo mchele mpaka sasa huko wapi? Bandarini? Au tayari ulishasambazwa mashuleni? Je Bashe amechukua hatua gani mpaka sasa, sio atwambie maneno tu na imekuwaje jambo nyeti kama hilo lingie nchini bila kibari maalumu?
 
Ahsante sana, kumbe kuna watu wenye busara kama wewe wapo nchini, wewe ni IQ kubwa, hao wanaobisha wana usiwalaumu ndiyo kikomo chao. Hawa watu huwa hawajui kuwa hata hao wazungu 90% hawajui neno Tanzania. Muulize Trump neno Tanzania wala hawezi kupoteza muda. Kuna watu wana vichaa hizi nchi zetu. Watu kwenye AI wanacompete kwenda mars halafu wafikirie kuwaua Tanzania? Dawa zote za ukimwi zinatolewa na hao hao ili tusife mbona hamkatai? Budget yenu nayo iko subsidized na wao mbona hamkatai? Midomo mirefu vichwa vitupu! Shenzi taipu
Wewe utakuwa mwajiriwa wa hiyo NGO, point ni kuwa tunacho chakula cha kutosha nchini hakuna sababu ya kupewa msaada wa chakula hata wewe kama kwenu kuna njaa muone mkuu wa wilaya yako atakupa maelekezo.Katika maisha yangu sipendi mtu wa kunilazimisha chakula au kinywaji, pereka huo mchele Somalia, Sudan, Hait, Ethiopia huko kote watu wanakufa kwa ukame kuanzia mifugo mpaka binadamu.
 
Wamarekani wameiba wazo la CHAUMA. Mzee Rungwe hajafurahi kabisa!

IMG-20240317-WA0102.jpg
 
Hongera Bashe. Pinga Kwa nguvu zote hatuhitaji kuharibiwa watoto wetu
Tanzania si nchi ya kusaidiwa chakula
Kwa nini wasiisaidie Sudan kusini watu wanakufa njaa. Kuna kitu nyuma ya pazia
 
Kwa hiyo ameukataa?? kwa hiyo hatupati tena msaada wa huo mchele wa Marekani?

Lakini kuna mambo yanayochekesha kama siyo kufurahisha, ndiyo maana Raisi Trump aliwahi kusema waziwazi kuwa Africa inahitaji kutawaliwa tena. Hivi kati ya Africa na Marekani ni nani anayestahili kumsaidia mwenzake Mchele??

Marekani kule kila sehemu karibu ardhi yote inakaribia kutawaliwa na majengo na barabara, Ardhi ya kilimo ni ndogo sana ukilinganisha na Africa, lakini cha kushangaza wao tena ndyo wanaotusaidia sisi chakula kama huo mchele. Poor Africa
Marekani wana ardhi kubwa sana ya chakula na wanalima kwa Teknolojia ambayo imetuacha nyuma miaka kama 20.
 
Hongera Bashe. Pinga Kwa nguvu zote hatuhitaji kuharibiwa watoto wetu
Ni maskini wa kufikiri pekee anayefikiri Marekani itatumia jambo dogo hivi kutekeleza mipango yake. Marekani anatumia mambo ambayo yanaumiza lakini huwezi kuacha kuyatumia kama vile teknolojia. Tumeambiwa mara nyingi ya teknolojia ya 5G kwamba inasababisha mionzi hatari lakini watu hawaelewi wanatumia, mambo kama hayo ndio Marekani anatumia Kwa sababu anajua teknolojia inakuwa basi ni lazima mtatumia tu
 
Mada hii ni kuelezea mashaka makubwa niliyonayo kwa Waziri wetu wa kilimo namna maamuzi yake yanavyoweza kuharibu mahusiano ya kimataifa kama asipojirekebisha.

Kwanza kabisa nianze Kwa 'declare interest' ,Sina mahusiano ya aina yoyote na NGO iliyoleta mchele wa msaada wenye virutubisho kutoka nchini Marekani chini ya kampeni ya wizara ya kilimo ya Marekani inayoitwa "Pamoja tuwalishe" na 'interest' pekee niliyonayo ni Kwa maslahi mapana ya nchi yangu .

Siku zote mjumbe hauawi na hiyo NGO inabaki kuwa ni mjumbe tu wa wizara ya kilimo ya Marekani ,kitendo Cha Waziri kuonesha kukasirishwa na kitendo Cha mjumbe kinaleta picha isiyopendeza.

Kwa mtazamo wangu badala ya Waziri Bashe kuonesha kukasirishwa na kuletwa Kwa mchele na hiyo NGO angetumia nafasi hiyo kufanya "formal communication" na wizara ya kilimo ya Marekani juu ya mambo tunayohitaji.

Kwa kuwa mchele huo ni msaada sikuona ulazima wowote wa Waziri kusema kwamba mchele tunao ,Kwa kuwa lengo la kampeni hiyo ni zuri ,tunatakiwa kuupokea msaada huo na kushukuru na wizara ingetumia TBS kuchunguza ubora wa mchele huo kimya kimya kabla haujaanza kutumika na kama kungekuwa na mashaka yoyote Serikali ingekataa baada ya kufanyika Kwa uchunguzi na ubora na sio Kwa hoja za Waziri.

Mashaka niliyonayo kwa Waziri Bashe ni kuwa:

Kama Waziri hajui athari za kimahusiano zinazoweza kuibuka kutokana na kauli tu. Kitendo Cha Waziri Bashe kudai Kwa nini wasingeleta virutubisho wachanganye tukiwaona ,sio rafiki Kwa afya ya diplomasia. Kitendo hicho kinaweza kufikirika kama tuhuma ya usalama. Kabla ya kauli hiyo alitakiwa kuwatumia TBS kuuchunguza mchele.

Marekani ni Moja ya nchi zinazozalisha nataka ( mchele na mahindi) Kwa wingi duniani na kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa ,nchi yetu inaweza kukumbwa na baa la njaa na tukahitaji msaada wa Chakula kutoka nje. Je, tutapata wapi nguvu za kuomba msaada kutoka Marekani kama tumeamua kukataa msaada Sasa ?

Pengine kulikuwa na Cha zaidi ambacho hatukijui lakini kama ni hiki kilichopo ,ni vema Waziri Bashe angeliendea suala Hilo Kwa busara, angejiridhisha kwanza na angejua hatua Kwa busara ili tuendelee kuimarisha mahusiano na nchi nyingine.

Kila siku Rais anasisitiza mifumo kusomana ili kuepusha migogoro , na kama mifumo ingekuwa inasomana kusingekuwa na kauli za namna Ile kutoka Kwa Waziri.

Ahsante
Ukombozi wa Tanzania upo Mikononi mwa Watanzania wenyewe.
Ukombozi wa African upo Mikononi mwa waafrika Wenyewe.
"Ee Mungu tusaidie kufungua frikra zetu tuondokane na uvivu wa kufikiri na utupatie moyo wa kizalendo kwa kufanya kazi kwa bidii pasipo kunufaisha matumbo yetu iwe kwaajili ya ustawi wa vizazi vyetu vya baadae wapate kuishi Tanzania iliyo Salama" Amina.
 
Kwani mmeambiwa huo mchele utaingizwa sokoni kuuzwa kwa mtu yeyote au ni msaada maalum kwa shule takriban 300 zenye uhitaji wa lishe?
 
Kwa hili Bashe nampa pongezi kama waziri wa kilimo, wapeleke Congo, na Palestina kuna njaa wasitufanye kama dumper
Bashe yupo sahihi sana

Hata mimi nampongeza sana tena sana

ULe mchele una madhara makubwa sana hasa kwa sisi watoto wa kiume

Anaye claime ni mjonga wa kwanza
 
Bashe alikuwa sahihi kabisa tusicheze na Maisha ya Vivazi vyetu. hao TBS wengi Vihiyo hao.
 
MAREKANI NDO NCHI AMBAYO KWAO HUWEZI KUKURUPKA kutoa MSAADA, Bashe anaweza kuwa Yuko sahihi na yawezekana naye ana inteligensia iliyo MPA alert kuwa asipokee...tumeshuhudia baadh ya NGO ikiwa chambo cha kuleta maadili mabaya, pia tumekuwa na baadha ya mawakala wa hovyo kutangaza vibaya TZ kama vile ni MASKINI Sana kitu ambacho sio kweli ili wapate pesa. Naunga mkono kukataa Kwa BASHE..wasiwas ni Bora kuliko kutibu ugonjwa.. TBS nayo ni zero brains mara ngapi tumeona udhaifu wao kwenye bidhaa..feki?. Cosmetics, madawa,condom, pombe, nguo za mitumba, magari, nk...tufike paala tuwaze hili TAIFA na kizazi kijacho...pia tusiaubiri ketuletea kitu nchini ndo tbs iingilie kati..maana wakati mwingine inakuwa DUMPING CENTER.
 
Attachments

  • FB_IMG_1709544780045.jpg
    FB_IMG_1709544780045.jpg
    92 KB · Views: 1
Nani aliwaomba msaada wa mchele hao marekani? Wanaleta msaada wa nini wakati hawajaombwa?
 
ULe mchele una madhara makubwa sana hasa kwa sisi watoto wa kiume
Mara Mahanithi wameongezeka ghafla baada ya Watoto wetu kulishwa hivyo virutubisho.

Waziri Bashe ana Support yangu. Vivaa!! Bashe Viivaa!!!
 
Back
Top Bottom