Waziri Bashe hakutakiwa kuukataa msaada wa mchele kutoka Marekani na kama alikuwa na mashaka yoyote angewatumia TBS

Daaaah, kweli kilimo cha BONGO kinahitaji mabadiliko.

Kwamba hawajaleta mbegu , wameleta mchele.

Ila lile la SUKARI ndio lilimuhusu sio ? Kwa kuwa SUKARI ni mbegu, ama ??
Sukari hawagawi mashuleni itauzwa madukani hilo linamhusu
 
Huyu waziri anakwama sana hicho kigezo alichotumia sio sahihi,maana Tanzania bado ni nchi masikini sana tukubali huu ukweli na Kuna watu wanauhitaji na huo msaada
 
Kwa mambo mengi ya hovyo yanayoendelea nchini mwetu,si kawaida na haikubaliki Marekani kutupa msaada wa chakula.Kwanza wameweka nini humo,hasa ukizingatia kuwa Marekani ni taifa la kishetani?
 

Attachments

  • VID-20240319-WA0001.mp4
    12.4 MB
Inaonyesha wazi hakuwa ameshirikishwa katika mpango huo tangu hatua za awali.
Ni vizuri, amekuwa na msimamo wa kiume. Mwanaume halii bali utautambua uso wake.
Kwa nafasi yake ni sawa kabisa alichokifanya.
Huyo msanii tu!! Kwani chombo kinachopima ubora wa vitu si kipo? Na kilishirikishwa, ni siasa tu, na kwa taarifa yako, hutamsikia tena, na huo mchele utaliwa.
 
Watanzania wanakataa msaada wa msosi kwa hofu huku dawa kutoka huko wakizifakamia, kuna mapombe ya vichupa wanakunywa na wala hawana hofu na pombe hizo
Mchele wanapewa watoto, usishange kama wilaya nzima au kituo cha wazee kingekuwa na shida hiyo wasingepewa huo msaada na pombe wanakunywa watu wazima sio watoto, dawa kupita huko haitokolea.
 
Mada hii ni kuelezea mashaka makubwa niliyonayo kwa Waziri wetu wa kilimo namna maamuzi yake yanavyoweza kuharibu mahusiano ya kimataifa kama asipojirekebisha.

Kwanza kabisa nianze Kwa 'declare interest' ,Sina mahusiano ya aina yoyote na NGO iliyoleta mchele wa msaada wenye virutubisho kutoka nchini Marekani chini ya kampeni ya wizara ya kilimo ya Marekani inayoitwa "Pamoja tuwalishe" na 'interest' pekee niliyonayo ni Kwa maslahi mapana ya nchi yangu .

Siku zote mjumbe hauawi na hiyo NGO inabaki kuwa ni mjumbe tu wa wizara ya kilimo ya Marekani ,kitendo Cha Waziri kuonesha kukasirishwa na kitendo Cha mjumbe kinaleta picha isiyopendeza.

Kwa mtazamo wangu badala ya Waziri Bashe kuonesha kukasirishwa na kuletwa Kwa mchele na hiyo NGO angetumia nafasi hiyo kufanya "formal communication" na wizara ya kilimo ya Marekani juu ya mambo tunayohitaji.

Kwa kuwa mchele huo ni msaada sikuona ulazima wowote wa Waziri kusema kwamba mchele tunao ,Kwa kuwa lengo la kampeni hiyo ni zuri ,tunatakiwa kuupokea msaada huo na kushukuru na wizara ingetumia TBS kuchunguza ubora wa mchele huo kimya kimya kabla haujaanza kutumika na kama kungekuwa na mashaka yoyote Serikali ingekataa baada ya kufanyika Kwa uchunguzi na ubora na sio Kwa hoja za Waziri.

Mashaka niliyonayo kwa Waziri Bashe ni kuwa:

Kama Waziri hajui athari za kimahusiano zinazoweza kuibuka kutokana na kauli tu. Kitendo Cha Waziri Bashe kudai Kwa nini wasingeleta virutubisho wachanganye tukiwaona ,sio rafiki Kwa afya ya diplomasia. Kitendo hicho kinaweza kufikirika kama tuhuma ya usalama. Kabla ya kauli hiyo alitakiwa kuwatumia TBS kuuchunguza mchele.

Marekani ni Moja ya nchi zinazozalisha nataka ( mchele na mahindi) Kwa wingi duniani na kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa ,nchi yetu inaweza kukumbwa na baa la njaa na tukahitaji msaada wa Chakula kutoka nje. Je, tutapata wapi nguvu za kuomba msaada kutoka Marekani kama tumeamua kukataa msaada Sasa ?

Pengine kulikuwa na Cha zaidi ambacho hatukijui lakini kama ni hiki kilichopo ,ni vema Waziri Bashe angeliendea suala Hilo Kwa busara, angejiridhisha kwanza na angejua hatua Kwa busara ili tuendelee kuimarisha mahusiano na nchi nyingine.

Kila siku Rais anasisitiza mifumo kusomana ili kuepusha migogoro , na kama mifumo ingekuwa inasomana kusingekuwa na kauli za namna Ile kutoka Kwa Waziri.

Ahsante
Kwa ufahamu tu, hiyo NGO imesajliwa kuhusika na mambo haya ya vyakula? Je, hiyo NGO ina hizo nguvu za kuweza ku-deal na nchi ya Marekani kw "niaba ya nchi, bila wizara husika kuwa na taarifa"? Je, hivyo virutubisho vlivowekwa ktk mchele vinafahamika? ni vp? Vnaeleweka? Nafkiri kulkuwa na wkt, kama sjasahau, nlisikia shehena ya mchele ilimwagwa baharini kw sbb fulani, je palkuwa hapana mahitaji? Walengwa ni shle 300, je baada ya hizo kpata msaada, hitaji ltakwisha? Haya mahitaji ya misaada, je kila mtu anaruhsiwa ku-deal na serikal yyte kuomba misaada ya chakula? Nafkiri, ktk nyakati hz za tech za kidigitali, maamuz kuh vyakula ni ya kuchukliwa kw tahdhari - watu wasijejikuta "kizazi kinatowekeshwa" ...nk
 
Mchele wanapewa watoto, usishange kama wilaya nzima au kituo cha wazee kingekuwa na shida hiyo wasingepewa huo msaada na pombe wanakunywa watu wazima sio watoto, dawa kupita huko haitokolea.
kama vipi huo mchele wapewe watu wazima wale
 
Back
Top Bottom