Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 5,897
- 10,358
Naona Wabunge na Mawaziri kutoka chama cha mapinduzi bado wanapeleka moto kwa Luhaga Mpina baada ya kuonesha kuwa-challenge kwenye masuala mbalimbali.
Akichangia Bungeni, Waziri wa Mifugo na Uvuvi ametupa dongo kwa Boss wake wa zamani kwenye Wizara hiyo kuwa hakutumia busara kupima samaki ambao washapikwa.
---
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema alishindwa kupinga maamuzi ya aliyekuwa Boss wake Luhaga Mpina baada ya Viongozi wa Wizara hiyo kwenda kupima kwa rula samaki waliopikwa kwenye mgahawa wa Bunge.
Ulega amesema hayo wakati akijibu hoja ya Mpina aliyoiibua Bungeni wakati akichangia mjadala wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambapo alimtaka Waziri aeleze kanuni iliyotumika kutekeleza zoezi hilo.
“Wakati mwingine tunakaa kimya maana kukaa kimya nayo ni busara, samaki akishapikwa anapoteza shape anapoteza size sayansi ya samaki haielekei huko , samaki yule aliyepimwa na Boss wangu wa zamani (Mpina) Mheshimiwa alikuwa amekaangwa kapita katika nyuzijoto nyingi sana alipoteza uhalisia sasa alitaka wakati ule nimwambie Mzee unakosea hapa”
Pia soma