Wazazi hii tabia si njema hata kidogo....

FirstLady1

JF-Expert Member
Jul 29, 2009
16,792
5,375
Pale wazazi mnapoamua kuporomosheana maneno mazito mazito mbele ya watoto wenu..
inasikitisha sana na haijengi maadili katika makuzi ya watoto wetu
kwani wanajifunza kupitia sisi wazazi.
..
Jana nikiwa napita nyumba ya jirani
baba wa familia moja alikuwa anamporomoshea mama watoto wake maneno mazito
sana ambayo mwenyewe nikajihisi kuona aibu .
watoto age 8,6 nadhani na mdogo kabisa ana 4yrs ,wamesimama wanalia
mbaya zaidi yule mdogo amemshika mama miguu kwa uchungu machozi yanatililika
Sijui alikuwa anaelewa kinachoendelea...
Huyu baba nikamsalimia tu salama jirani...
Akaanza ooh si huyu mama Fulani ananiletea ujinga jinga wake
..akili kama za Mbuzi mie sizitaki
sijui huyu mbuzi anaakili zipi mpaka amfananishie mama watoto wake.
Nikaona na mie ndo naanza kuingizwa kwanye ugomvi....
Kweli nilijitahidi kurudisha amani ingawa yule wife alinambia nilipoondoka zogo lilianza tena.

: Nionavyo mie kama kuna tofauti basi tujifungie room
tumalize kasheshe zetu na si kuwakwaza watoto wasio na hatia.
Tuache haka katabia sio kazuri hata kidogo
 
Pale wazazi mnapoamua kuporomosheana maneno mazito mazito mbele ya watoto wenu..
inasikitisha sana na haijengi maadili katika makuzi ya watoto wetu
kwani wanajifunza kupitia sisi wazazi.
..
Jana nikiwa napita nyumba ya jirani
baba wa familia moja alikuwa anamporomoshea mama watoto wake maneno mazito
sana ambayo mwenyewe nikajihisi kuona aibu .
watoto age 8,6 nadhani na mdogo kabisa ana 4yrs ,wamesimama wanalia
mbaya zaidi yule mdogo amemshika mama miguu kwa uchungu machozi yanatililika
Sijui alikuwa anaelewa kinachoendelea...
Huyu baba nikamsalimia tu salama jirani...
Akaanza ooh si huyu mama Fulani ananiletea ujinga jinga wake
..akili kama za Mbuzi mie sizitaki
sijui huyu mbuzi anaakili zipi mpaka amfananishie mama watoto wake.
Nikaona na mie ndo naanza kuingizwa kwanye ugomvii....
Kweli nilijitahidi kurudisha amani ingawa yule wife alinambia nilipoondoka zogo lilianza tena.

: Nionavyo mie kama kuna tofauti basi tujifungie room
tumalize kasheshe zetu na si kuwakwanza watoto wasio na hatia.
Tuache haka katabia sio kazuri hata kidogo

itakuwa unakaa uswazi F1 , njoo Upanga
 
Kwa kweli ni vibaya sana kutukanana mbele ya watoto. Na ni mbaya zaidi kama hao watoto wako kwenye formative years kama hao uliowaelezea maana hizo taswira na sauti huwa zinaganda vichwani mwao kwa muda mrefu sana na huweza kuwaathiri pia.
 
Well said
Wengi wanajisahau na kuanza kuporomosha matusi mazito sana mbele ya watoto
Hata kaam watoto hawaelewi kinachoendelea ila wanapoona ile sauti ya baba iko juu na mama analia wanaelewa kuwa hapa si kwema kabisa
Kuna tatizo
 
Boflo nimependa signature yako ..good
Hurt me with the TRUTH...But don't comfort me with a LIE!
 
Kwa kweli ni vibaya sana kutukanana mbele ya watoto. Na ni mbaya zaidi kama hao watoto wako kwenye formative years kama hao uliowaelezea maana hizo taswira na sauti huwa zinaganda vichwani mwao kwa muda mrefu sana na huweza kuwaathiri pia.

Asante sana NN kwa kuliona hili ,kweli haipendezi hata kidogo kweli mnashindwa kumaliza tofauti chumbani mnaamua kuzianika mbele ya watoto wasio na hatia.Ili iweje?
 
Well said
Wengi wanajisahau na kuanza kuporomosha matusi mazito sana mbele ya watoto
Hata kaam watoto hawaelewi kinachoendelea ila wanapoona ile sauti ya baba iko juu na mama analia wanaelewa kuwa hapa si kwema kabisa
Kuna tatizo

huu unakuwa ni ukosefu wa hekima ,mie naamini mwanamme ni kichwa cha familia anapaswa kutumia hekima kubwa akishilikiana na mke kuiendesha familia ..
 
Hapa ndipo watoto wanapoanza kujenga matabaka kwa wazazi wao na kuchagua wa kumpenda/wakumchukia.....aidha baba au mama!!
 
Na hii ipo sana kwenye baadhi ya familia zetu na huwa inawaathiri sana watoto, mie kijijin kwetu jiran yetu alikuwa na tabia hiyo hadi watoto wakawa wanamchukia baba yao
 
Ni kweli hii tabia haifai unamkuta mbaba na msuri tumbo nje anatukana utadhani anamsuta mkewe
tabia mbaya hii na tena haifai
 
Umegusia swala la muhimu saana FL1, Saa ingine lakini hata wanawake tunaendekeza huu upuzi, Mumeo akutukane mbele za watoto na kukuita mbuzi, yaani kwa kweli inasikitisha na you have to bring your Claws out to end it once and for all!! Kwmba watu wamechukia alafu hao wanachukuana kwa amani wakagombane chumbani inategemea saana na ustahimilivu wa kila mmoja aisee.... It is not that simple. Kikubwa wazazi woote akina mama na baba wajue kabisa kua wanapo gombana na kutuka nana mbele ya watoto ina waathiri sana hasa Psychologically na kukimbiza upendo kabisa ndani ya nyumba.
 
Ni sahihi kabisa Ndugu zangu kuna Wazazi sijui wanategemea nini juu ya watoto wao coz wanafanya mambo mengi mabaya afu watoto wao wanangalia baadae watoto wanahalibika wanaanza kusema watoto hawa hawana adabu.mmmmmmmm.....hapana inakela wazazi tuwape makuzi mazuri watoto wetu pamoja na maadili mazuri.
 
Back
Top Bottom