Wazazi hii tabia si njema hata kidogo....

Tatizo linakua kwa hawa wanawake wa siku hizi wanajidai na wao wanakibezi!! anasahau kuwa baba ni kicha cha familia akikoroma inatakiwa nyumba nzima ikae kimya siyo mwanamke nae kuleta kibezi!! ......angepiga kabisa.
MP.
 
Tatizo linakua kwa hawa wanawake wa siku hizi wanajidai na wao wanakibezi!! anasahau kuwa baba ni kicha cha familia akikoroma inatakiwa nyumba nzima ikae kimya siyo mwanamke nae kuleta kibezi!! ......angepiga kabisa.
MP.

Kibezi ndio nini Maprosoo..
Harafu pia kumbuka ugomvi sio mzuri kwa nini ukorome?
 
Kiukweli hii ni tabia mbaya sana kwa wazazi............
Tena mwingine hata kama mko chumbani yeye anaita kabisa watoto njooni
niwaambie mama alivyofanya ujinga wake aahhh
wajameni tuwe na staha kwenye ndoa zetu
 
Pale wazazi mnapoamua kuporomosheana maneno mazito mazito mbele ya watoto wenu..
inasikitisha sana na haijengi maadili katika makuzi ya watoto wetu
kwani wanajifunza kupitia sisi wazazi.
..
Jana nikiwa napita nyumba ya jirani
baba wa familia moja alikuwa anamporomoshea mama watoto wake maneno mazito
sana ambayo mwenyewe nikajihisi kuona aibu .
watoto age 8,6 nadhani na mdogo kabisa ana 4yrs ,wamesimama wanalia
mbaya zaidi yule mdogo amemshika mama miguu kwa uchungu machozi yanatililika
Sijui alikuwa anaelewa kinachoendelea...
Huyu baba nikamsalimia tu salama jirani...
Akaanza ooh si huyu mama Fulani ananiletea ujinga jinga wake
..akili kama za Mbuzi mie sizitaki
sijui huyu mbuzi anaakili zipi mpaka amfananishie mama watoto wake.
Nikaona na mie ndo naanza kuingizwa kwanye ugomvi....
Kweli nilijitahidi kurudisha amani ingawa yule wife alinambia nilipoondoka zogo lilianza tena.

: Nionavyo mie kama kuna tofauti basi tujifungie room
tumalize kasheshe zetu na si kuwakwaza watoto wasio na hatia.
Tuache haka katabia sio kazuri hata kidogo

Kweli kabisa mkuu wala hujakosea, lingine ni hili la zile nyumba za kupanga linapoanza zogo kati ya mpangaji na mpangaji mh! Hayo matusi ni zaidi ya kumvua mtu nguo na kumwacha mtupu
 
Kwa kweli ni vibaya sana kutukanana mbele ya watoto. Na ni mbaya zaidi kama hao watoto wako kwenye formative years kama hao uliowaelezea maana hizo taswira na sauti huwa zinaganda vichwani mwao kwa muda mrefu sana na huweza kuwaathiri pia.

Hata kama ni wakubwa bado siyo nzuri maana haitawawia vigumu nao siku moja nao kuwatukama wazazi jambo ambalo litawasababishia kuachiwa laana na wazazi wao
 
Well said
Wengi wanajisahau na kuanza kuporomosha matusi mazito sana mbele ya watoto
Hata kaam watoto hawaelewi kinachoendelea ila wanapoona ile sauti ya baba iko juu na mama analia wanaelewa kuwa hapa si kwema kabisa
Kuna tatizo

ni kweli kwani hata mtoto mchanga kabisa huwa anahisi kitu kama hicho na kumfanya alie
 
Mama, nyanyua watoto wako kawahifadhi popote au baba kakodishe guest umpeleke mkeo huko ukamporomoshee maneno kama huwa hajali.

Halafu we mama/baba inakuwaje hadi kuanza kumporomoshewa matusi mbele ya watoto wako? Kwa kosa gani hasa ulilofanya (wewe mtu mzima mwenye kujua baya na zuri) hadi ukubali kusimama tuli na kusikiliza wewe na wanao maneno machafu toka kwa mtu mnayemwamini?
 
Hekima na busara za wazazi ndizo zitawakuza watotn wao ktk maadili mema pamoja na kuwa na heshima, urithi ambao utawajengea future nzuri
 
Hili jambo c jema,linaathiri tabia za watoto.Mzee Kandoro aliwahi sema kwenye diwani yake"WATOTO NI KM VITABU VINAVYOANDIKWA NDIVYO VITAVYOSOMEKA"hivyo tuwalee vizuri wawe mema
 
Kati ya mambo nisiyo yapenda ni maugomvi gomvi tena mbele ya kids, haifai kabisa! Kitu kimoja tunachotakiwa kujifunza ni kwamba unapoona mwenzio kakukosea sio unaendelea kuchoooooooooooooonga hadi mkosaji naye anfika mahali anaona ni heri ku-react pamoja na kukosa kwake na inapofika hapo ndo unakuta miropoko inapelekwa hewani hadi kids nao wanajua kinachoendelea kati ya baba na mama!
 
Ni kukosa kujiheshimu kwa hao wazazi manake ni watu wazima wanaelewa baya na zuri, kuporomosheana matusi mbele ya watoto ni makosa makubwa sana, hamuwatendei haki manake mnawajaza mioyo yao mambo makubwa wasiyoyastahili, wanapata hasira, chuki, woga na wasiwasi mda wote! Kumwita mama/baba mbuzi, paka, mbwa, ng'ombe n.k mbele ya watoto sio vizuri manake unadhani hao watoto watamwonaje siku zijazo!... Tuache kuharibu watoto wetu jamani...

Hakuna kitu kinawaathiri watoto kama ugomvi wa baba na mama, wanakosa amani/furaha sana wasikiapo wazazi wakirushiana maneno. Sio vizuri kabisa.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom