Kuna watu wana tabia nyeusi, akiwa jirani yako unatamani kuhama umpishe

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,115
Kuna mtu kahamia jirani nyumba ya pili, ana wiki ya 3 tu tangu ahamie ila nishajutia ujio wake kwa tabia zake, sijui katoka wapi huyu mtu jamani natamani hata kuhama nimpishe maana kumhamisha siwezi.

Ana tabia nyeusi sana, hata sijui niziitaje maana anaongea lugha ya matusi sijapa kuona huyu Mama, anaongea kwa sauti kubwa kama anatangaza na anaongea kutwa nzima Kuanzia saa 11 anaanza kuongea na watoto wake na mume wake mbaya zaidi anaongea mambo ya ovyo mwanzo mwisho mpaka saa 5 usiku akilala ndio kunakuwa shwari.

Ana waita watoto majina ya matusi na kuwatukana matusi mazito ( We kifulani chako njoo hapa, hapo kinatajwa kuingo cha siri cha mtoto chochote) ambayo hata mimi naona aibu, kwa sauti anayotumia kuongea unasikia kila kitu hadi naamua kufungulia mziki ili kukwepa matusi yake.

Hali hiyo hata kwa mumewe pia Mfano leo kamwambia mumewe hivi wewe baba M una akili timamu kweli, unaenda kununua Kvant ndogo hujui nami nataka kunywa we K......m Ny zako, kalisha hayo map...u yako hapo badala ya kurudia nyingine, mume naye kajibu tusi zito pia mbaya zaidi watoto wao wapo.

Nawaza hao watoto wao watakuwa watu wa aina gani hapo baadaye au ndio watakuwa wanatukana matusi mazito zaidi ya wazazi maana watakuwa washayazoea mno, kwanza kutwa wanasikiliza kelele za Mama yao, maadili kwao ni fumbo hakuna msamiati huo kwenye hiyo familia, sijui wameokotana wapi wazazi hawa masikini wanawapa mzigo watoto kuwabebesha matusi kutwa kucha!

Napata huruma kwa hao majirani zake wanaochangia nyumba sijui wana hali gani, mimi niko nyumba ya pili nishakereka na ndio sikai sana nyumbani kwa siku chache kama wiki nimekaa nyumbani kwa dharura nimejutia ujio wao hao wanaoshinda nao wana hali gani, hiyo ni siri yao maana mimi si mtu wa kwenda kwa watu ivyo sijui japo nadhani watakuwa wanakerwa pia maana nyumba ile kabla ya huyu jamaa na mkewe ilikuwa imegubikwa na ukimya.

Sina budi kuhama kunusuru afya maadili ya familia yangu maana kwa sasa wanashiba matusi kuanzia saa 11 aljajiri mpaka saa 5 na kero ya sauti za mtu anaongea kama kafungwa spika za matangazo ya bishara zile za machinga.

Jirani huyu anapaswa kukaa mtaa wa peke yake au akae na watu wa kariba yake na si watu waliostaarabika. Ama hakika anachosha na kukera sana.
 
Umenichekesha na kunikumbusha mambo ya nyuma kidogo.

Mtaa wetu una background nzuri sana ya ziwa. Majirani zangu walijenga nyumba zao kikamilifu tangu mwanzo lakini mimi nilijenga kwa awamu nne, huenda kwa sababu ya njaa. Sasa kuna kipindi nilipokuwa najenga backyard yangu, yaani deck, patio na shed, jirani yangu mmoja akaja kwa hasira kunimabia kuwa kwa nini ninajenga shed, hasa kwa vile shed niliyokuwa ninajenga ilikuwa inamzibia view ya ziwa.

Hakujua kuwa nilikuwa nimepeleka ramani zangu zote kule City zikaidhinishwa kabla kuanza ujenzi na kila hatua ya ujenzi ilikuwa inaidhinshwa na inspector wa city. Nikamumbia kuwa akiendelea kuniingilia katika plans zangu nitajenga uzio wa ukuta kuzungka uwanja wangu ili assingile mambo yangu, na ukuta huo utamzuia kabisa kuona ziwa.

Inspector alipokuja kukagua maendelo ya ujenzi wangu nikamuambia kuhusu malalamiko ya jirani yangu huyo. Insepctor huyo aliniambia tu kuwa "There are many people who cannot concentrate on their own business; they just want to sniff around what their neighbors do, and you cannot prevent them from doing that, just ignore them."
 
Unesoma nilichoandika? Nimeandika megi kahamia ndio ana wiki 3 hajafikisha hata mwezi.

Pili sijaandika neno ushuani ila nakataa kuwa ni uswazi.
 
Back
Top Bottom