Wawili akiwemo mchungaji washikiliwa na polisi kwa kulaghai mchawi kadondoka na ungo kanisani kwenye mkesha

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
F42SWqFXQAAggJh.jpg
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linawashilika watu wawili akiwemo Emanuel Paul Karata (35) mchungaji wa kanisa la PENTEKOSTE GOSPEL MISSION lililopo Kibaha kwa ulaghai wa kutaka kupata waumini kwa kusingizia mchawi amedondoka kwenye maombi ya mkesha wake na waumini.

Wamewashikilia kwa mahojiano kutokana na taarifa za mtu mmoja jinsia ya kiume Basenga Silvester Matheo (59) kudondoka kanisani akiwa anasafiri kwa ungo wa kichawi au kishirikina.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Kibaha mkoani Pwani, Kamanda wa Polisi ACP Pius Lutumo amesema, tarehe 24 mwezi huu majira ya saa 09:00hrs huko katika kituo cha polisi Kibaha Mkoa wa Pwani alitoa taarifa za mtu mmoja ambaye alifahamika kwa jina la Basenga Silvester Matheo (59) mkazi wa Miswe wilaya ya Kibaha akiwa amesafiri kwa ungo wa kishirikina na kudondoka kanisani hapo na kuleta taharuki kubwa kwa waumini.

Katika uchunguzi, jeshi la polisi lilibaini kuwa tukio hilo ni tukio la kutengeneza kwa lengo la kuwalaghai au kuwahadaa waumini na wananchi kwa ujumla kwa lengo la kupata waumini zaidi na kujipatia kipato.

"Ilielezwa kwamba siku ya tukio kulikuwa na ibada ya mkesha ambapo mtuhumiwa akiwa na wenzake sita alidondoshwa kwa sala za maombi ya waumini na mchungaji wao na wenzake wakafanikiwa kutoroka kichawi".

"ili kudhibiti taharuki hiyo mchungaji alimchukua mtu huyo na vifaa vyake vya kishirikina na kumuweka ofisini kwake hadi asubuhi polisi walipofika na kumchukua."

Bwana BUSENGAS/OSILVESTER MATHEO alijinisibu kuwa yeye na wenzake walifika kanisani hapo kishirikina kwa lengo la kupima imani ya waumini hao kwa Mwenyezi Mungu.

Aidha mtuhumiwa aliahidiwa kulipwa Shilingi 50,000/= baada ya kutimiza lengo lao la kilaghai.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linatoa onyo na tahadhari kwa watu wenye tamaa ya kupata kipato cha haraka kwa kufanya ulaghai kuacha mara moja.

Aidha linatoa wito kwa waumini kuwa makini na watu wachache wanaotaka kuharibu imani za kidini kwa tamaa ya kipato.
 
Mchungaji huyo wa kanisa kanisa binafsi la mabati lililoko Kibaha lijulikanalo kama Pentecoste Gospel mission alitengeneza tukio la mchawi kuanguka kanisani kwake.

Mchawi feki huyo aliyefikishwa kituo cha polisi Kibaha mwanzoni akijidai yeye na wenzake sita ni wachawi toka Msata.. Sio kule kilingeni kwangu.

Kwamba nguvu ya maombi kanisani hapo palipokuwa na mkesha ndio ilimwangusha na wenzake kufanikiwa kutotoka, ilikuja kugundulika alitengeneza tukio hilo pamoja na mchungaji huyo kwa makubaliano ya malipo ya elfu hamsini tasilimu na kwamba alikuwa hajalipwa bado.


View: https://youtu.be/mIfGeNGff54?si=2CYMJci8LEBknGxw
 
Hamna kesi hapo

Kila mtu anasema kivyake.... Inawezekana
A) pastor katengeneza mchongo kweli kwa makubaliano
B) jamaa ni mchawi kweli ila alivyoona kayakoroga anamsingizia mchungaji kua walifanya mchongo

Words against words, ushahidi sifuri

Wakienda mahakamani wanafukuzwa hao
 
Miaka minne mbele jamaa anakua mchungaji maarufu na AKA ya Kiboko ya Wachawi.

Anatokea mtu kuonyesha jamaa aliwahi stage tukio ila wabongo utatuambia nini tukishaamini mtu?
 
Back
Top Bottom