Baadhi ya Polisi nchini ni waongo na wauaji

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Hii sio taarifa ya tukio bali ni tathmini ya utendaji wa jeshi letu la Polisi katika kukiuka haki za wananchi wa Tanzania, binadamu walioapa kuwalinda.

Hivi karibuni huko Kibaha kumetokea tukio la mtu kuuwawa kwa risasi, na mwili wake "kuokotwa" na wananchi. Ndugu wa mtu alieuwawa wanasema mtu huyo aliuwawa na Polisi wakiwashambilia kwa risasi wauza mkaa. Polisi, japo wanakiri kulikuwa na "mapambano" kati yao na wauza mkaa, wanajaribu kuonyesha sio wao waliomuua mtu huyo - naona wakimaanisha kwamba katika mpambano ule wauza mkaa wote walikwepa risasi zao!

Nitaweka hapa sehemu ya habari kuhusu muuza mkaa anaedaiwa kuwawa na Polisi huko Kibaha, halafu watu mtafakari kuhusu hizi kauli zinazotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo

1710227646517.png

Sasa Lutumo anasema waliwasimamisha wakiwa na boda boda zao, wakakaidi, na tunajua unaposema bodaboda alisimamishwa akakaidi ina maana alikimbia na bodaboda yake. Sasa suala la kupambana na askari linakujaje?

Sasa cha ajabu, mwili wa muuza mkaa unapatikana akiwa amepigwa risasi, polisi wanasema "umeokotwa na wananchi" kama vile wao hawahusiki na kuuwawa kwa mtu huyo, ambae ni mmuuza mkaa, na huku wakikiri waliwarushia risasi wauza mkaa. Hivi kweli, tumefikia mahali polisi anamfyatulia raia risasi, kosa likiwa kuuza mkaa isivyo halali?

Kama Polisi waliona ni halali kuwaua wauza mkaa kwa risasi, basi kwa nini angalau wasichukue mwili wa mtu waliemuua na kumpeleka hospitali kwa kuhifadhiwa? Kitendo cha kwenda kumlaza mahali na wao kuondoka ni wazi walijua wamefanya makosa, halafu wanakuja kutoa hadithi zisizo na pua wala mdomo kwa wananchi.

Tuseme ukweli, baadhi ya Polisi wetu ni wauaji, katili na waongo!
 
Nitashangaa sana kama Samia alakaa kimya kuhusu hili. Wauza mkaa ni mojawapo ya watu wanaohangaika na maisha magumu ya Tanzania, hawauzi mkaa kwa kuwa wamechagua kuuza mkaa dhidi ya kazi nyingine. Polisi waliohusika na hili wanapaswa kuwekwa ndani wote. Risasi kwa ajili ya mkaa tu?
 
Yaani samia awazingue watu wanaomfanya kuendelea kua ikulu,sahau hilo mkuu. Swala la uwajibikaji kwa nchi yetu ni mpaka raia wote tuamue.
 
Tatizo ndio liko hapo. Ndio maana nchi za wenzetu uongozi wa juu wa Polisi ni wa kuchaguliwa
 
Hii sio taarifa ya tukio bali ni tathmini ya utendaji wa jeshi letu la Polisi katika kukiuka haki za wananchi wa Tanzania, binadamu walioapa kuwalinda.

Hivi karibuni huko Kibaha kumetokea tukio la mtu kuuwawa kwa risasi, na mwili wake "kuokotwa" na wananchi. Ndugu wa mtu alieuwawa wanasema mtu huyo aliuwawa na Polisi wakiwashambilia kwa risasi wauza mkaa. Polisi, japo wanakiri kulikuwa na "mapambano" kati yao na wauza mkaa, wanajaribu kuonyesha sio wao waliomuua mtu huyo - naona wakimaanisha kwamba katika mpambano ule wauza mkaa wote walikwepa risasi zao!

Nitaweka hapa sehemu ya habari kuhusu muuza mkaa anaedaiwa kuwawa na Polisi huko Kibaha, halafu watu mtafakari kuhusu hizi kauli zinazotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo

Sasa Lutumo anasema waliwasimamisha wakiwa na boda boda zao, wakakaidi, na tunajua unaposema bodaboda alisimamishwa akakaidi ina maana alikimbia na bodaboda yake. Sasa suala la kupambana na askari linakujaje?

Sasa cha ajabu, mwili wa muuza mkaa unapatikana akiwa amepigwa risasi, polisi wanasema "umeokotwa na wananchi" kama vile wao hawahusiki na kuuwawa kwa mtu huyo, ambae ni mmuuza mkaa, na huku wakikiri waliwarushia risasi wauza mkaa. Hivi kweli, tumefikia mahali polisi anamfyatulia raia risasi, kosa likiwa kuuza mkaa isivyo halali?

Kama Polisi waliona ni halali kuwaua wauza mkaa kwa risasi, basi kwa nini angalau wasichukue mwili wa mtu waliemuua na kumpeleka hospitali kwa kuhifadhiwa? Kitendo cha kwenda kumlaza mahali na wao kuondoka ni wazi walijua wamefanya makosa, halafu wanakuja kutoa hadithi zisizo na pua wala mdomo kwa wananchi.

Tuseme ukweli, baadhi ya Polisi wetu ni wauaji, katili na waongo!
Bro mbona wapo hivyo siku zote,Hao ni majambazi yenye mamlaka,
Siku zote lazima, yata twist Mambo ili kujilinda, au kulinda wenzao, rejea kifo cha mwangosi!
Rejea kesi ya, mauaji, ya wafanyabiashara wa madini dar, polisi wakasema majambazi, kumbe wapi jamaa walikamatwa hotelini, wakapelekwa sinza wakachapwa risasi!
Thank God, ilikuja Kugundulika, baadhi ya polisi walihukumiwa kunyongwa mpaka kufa. Siku zote, usiingie kwenye kumi na nane za hawa wajomba! Utapotea,
Usijifanye mjuaji mbele ya hawa wajomba,
Wanaweza kukukamata, ukawekwa sero, ukala kipigo cha mbwa Koko! Kama hufi, utapata kilema cha maisha.
Nilishuhudia, masumbwe, mbogwe, kijana yupo lockup kwa kubaka na kuua,
Afande mmoja, akiwa, kavaa kiraia tu, ilikuwa, jmosi, akafungua lockup, akaanza kumpa kichspo jamaa, kwa, kutumia rungu, jamaa akakimbilia ndani ya kituo, kichapo kikaendelea, dk tano nyingi, jamaa anavuja damu kichwani, akarudishwa, lockup! Polisi, wakati wote huo, polisi wanaendelea na, mishe mishe zao, kama vile anayepigwa ni kuku!
 
Labda tatizo ni sisi wananchi. Hivi kweli hakuna tunaloweza kufanya kwa uharamia huu unaofanywa na baadhi ya askari wa jeshi la Polisi? Mie kwa kweli, japo JF wanasema ni baadhi ya Polisi, naona ni wote tu,kwa sababu IGP anaona na kuyasikia lakini yupo tu hachukui hatua, kazi yake kubwa kujipendekeza kwa raisi na viongozi wa CCM

Sasa hawa Polisi wakiona IGP hachukui hatua wanapofanya haya,wataacha ujambazi kweli? Na Samia je, yeye anaona akishasema hili nalo mkalitazame ndio kamaliza?
 
Polisi wenyewe wote makada hata kwa unafki.
Polisi wengi Tanzania wanapotaka kuficha uovu waliofanya wanatoa maelezo kama wana mtindio wa ubongo. Yaleyale ya tulipiga risasi hewani moja ikampata huyu dada alikuwa kwenye basi. Kulikuwa na vita kali ya kurushiana risasi na majambazi tukawaua wote hakuna Polisi alieuwawa wala kujeruhiwa.

Sasa tunataka kusikia kama kulikuwa na vita kali ya kurushiana risasi na majambazi angalau tusikie polisi watatu walidunguliwa risasi na majambazi, hapo ndio tutaamini kulikuwa na vita kali
 
Back
Top Bottom