Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,340
- 51,903
Kwema Wakuu!
Tukio la kupigwa kwa mchungaji na wanakijiji kisa Watoa uchawi maarufu kama Kamchape limezidi kudhihirisha dini na uchawi kwa sehemu kubwa ni utapeli.
Hakukuwa na sababu ya Mchungaji kuwazuia hao waganga kuja kutoa Uchawi. Zaidi hakukuwa na sababu hata moja ya kupiga simu polisi. Nguvu za kiroho hazipelekani Polisi.
Ilikuwa ni ishu ya Mchungaji kuonyesha nguvu za Mungu (miungu) anayoiamini na kuwahubiria watu kila siku. Mchungaji kama mwakilishi wa mungu wake katika eneo hilo alipaswa afanye jambo ambalo lingekuwa ushuhuda mzuri kwa haohao Kamchape na wasioamini katika imani na mungu wake.
Ilikuwa ni ishu ya kumuuliza mganga kuwa anafanya mambo hayo kwa Mamlaka ipi(mungu yupi) kisha aombe waonyeshane uwezo. Kwamba yupi ni mwenye nguvu.
Watu wa Kigoma wanayohaki ya kuamini mambo ya Uganga kwa sababu huenda ndio wenye nguvu na ndio unaowasaidia. Huwezi kumwambia mchungaji ambaye hakusaidii chochote. Yeye kila siku anadai anamtumikia mungu lakini nguvu za huyo mungu wake hajawahi kuzidhihirisha.
Mchungaji au Kuhani au nabii hawezi peleka mashtaka serikalini. Kama ilivyo Mganga, mchawi, mlozi hawa hawawezi peleka mashtaka Polisi au mahakamani. Wakati wanatumikia falme za kiroho.
Kitendo cha mchungaji wako au mganga wako kupeleka mashtaka mahakamani au polisi ni udhihirisho wa wazi kuwa huyo Mungu (miungu) yake haina nguvu.
Ukimkosea mchawi yeye atadili na wewe kichawi na shtaka lake atapeleka uchawini kama akikushindwa. Manabii, Makuhani, mitume ukiwakosea ni aidha wadili na wewe kwa uwezo wao au wakushtaki kwa miungu yao. Ili uhenyeshwe.
Serikali za kidunia ndio hupeleka mashtaka kwa miungu ikiwemo waganga na wachawi, au miungu lakini ukiona miungu inahitaji msaada wa serikali jua hapo kuna utapeli Mkubwa. Watu wanafanyiwa ulaghai.
Karibuni.