Rais Samia ampokea Dkt. Frank Walter Steinmeier, Rais wa Shirikisho la Ujerumani, Ikulu - Dar es Salaam, leo Oktoba 31, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpokea Mhe. Dkt. Frank Walter Steinmeier, Rais wa Shirikisho la Ujerumani katika Ukumbi wa Jakaya Kiwete Ikulu - Dar es Salaam leo tarehe 31 Oktoba, 2023

Tumezungumza mambo mengi ikiwemo ushirikiano wa kiuchumi na kijamii, uhusiano uliofikia miaka 60 sasa na katika kipindi chote hicho tumekuwa tunashirikiana vyema. Serikali ya Ujerumani imekuwa rafiki na mshirika mzuri katika mambo mengi.

Katika mazungumzo yetu tumesisitiza umuhimu wa kudumisha ushirikiano uliopo kwa manufaa ya watu wa pande zote 2.

Upande wa biashara na mahusiano ya uwekezaji, msisitizo kwenye mchango muhimu wa biashara katika kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi uliwekwa ambao kuna miradi zaidi ya 180 ya Ujerumani katika ngazi mbalimbali imewekezwa Tanzania.

Kwa upande wa utalii, wengi kutoka Ujerumani wamekuwa wanafika na upo uwezekano wa kupata wengi zaidi siku zijazo.

Demokkrasia, haki za binadamu na utawala bora, Rais wa Ujerumani ametoa pongezi kwa Tanzania kwa kuonesha utulivu kwenye maeneo hayo na ndio maana wafanyabiashara wamevutika kutoka Ujerumani kuja kuona fursa zilizopo nchini.

Rais wa Shirikisho la Ujerumani, Dkt. Frank Walter Steinmeier amezungumzia kuhusu kumbukumbu ya Vita ya Majimaji iliyotokea Mwaka 1905 – 1907.

Amesema “Ziara hii nimeiweka katika kuangalia yale yaliyotokea wakati wa Ukoloni na pia kuonana na walioathiriwa na vita ya Majimaji, kuzungumza na wahanga wa vita hiyo, najua walipitia kipindi kigumu ambacho si cha kupendeza, nitakayozungumza nayo nitayafikisha Ujerumani na ikiwezekana kuangalia namna ya kurusisha mabaki ya watu waliopigana vita.”

F9ve9PcWQAABLaA.jpg
F9vfCMJXkAAcYyY.jpg
 
Amuulize wao Ujerumani waliwezaje kuondoa ufisadi na umasikini? je kule kwao kuna chawa kama huku? pia kuna matumizi ya anasa ya serikali kama huku?
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpokea Mhe. Dkt. Frank Walter Steinmeier, Rais wa Shirikisho la Ujerumani katika Ukumbi wa Jakaya Kiwete Ikulu - Dar es Salaam leo tarehe 31 Oktoba, 2023

Tumezungumza mambo mengi ikiwemo ushirikiano wa kiuchumi na kijamii, uhusiano uliofikia miaka 60 sasa na katika kipindi chote hicho tumekuwa tunashirikiana vyema. Serikali ya Ujerumani imekuwa rafiki na mshirika mzuri katika mambo mengi.

Katika mazungumzo yetu tumesisitiza umuhimu wa kudumisha ushirikiano uliopo kwa manufaa ya watu wa pande zote 2.

Upande wa biashara na mahusiano ya uwekezaji, msisitizo kwenye mchango muhimu wa biashara katika kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi uliwekwa ambao kuna miradi zaidi ya 180 ya Ujerumani katika ngazi mbalimbali imewekezwa Tanzania.

Kwa upande wa utalii, wengi kutoka Ujerumani wamekuwa wanafika na upo uwezekano wa kupata wengi zaidi siku zijazo.

Demokkrasia, haki za binadamu na utawala bora, Rais wa Ujerumani ametoa pongezi kwa Tanzania kwa kuonesha utulivu kwenye maeneo hayo na ndio maana wafanyabiashara wamevutika kutoka Ujerumani kuja kuona fursa zilizopo nchini.

Rais wa Shirikisho la Ujerumani, Dkt. Frank Walter Steinmeier amezungumzia kuhusu kumbukumbu ya Vita ya Majimaji iliyotokea Mwaka 1905 – 1907.

Amesema “Ziara hii nimeiweka katika kuangalia yale yaliyotokea wakati wa Ukoloni na pia kuonana na walioathiriwa na vita ya Majimaji, kuzungumza na wahanga wa vita hiyo, najua walipitia kipindi kigumu ambacho si cha kupendeza, nitakayozungumza nayo nitayafikisha Ujerumani na ikiwezekana kuangalia namna ya kurusisha mabaki ya watu waliopigana vita.”

🙏
 
Hivi sisi hatuwezi kutoa misaada? Natamani nasisi rais akienda burundi atoe msaada wa ambulance mbili, hii inajenga mahusiano mema, museven alitujengea shule bukoba kagame alituzawadia ngombe,
 
Tumesaidiq wahanga wa tetemeko Uturuki
Tumesaidia Malawi
Nk
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom