Watumishi wa Umma: Sehemu Sahihi ya Kupeleka Malalamiko Ukifutwa Kazi

Apr 26, 2022
31
43
Kama ilivyowekwa bayana na Mahakama ya Rufaa kwenye kesi ya Tanzania Posts Corporation v Dominic A. Kalangi, Rufaa ya Madai na. 12, 2022.

Mwandishi: Zakaria
(Lawyer by profession)

MATERIAL FACTS (STORI YA KESI):

-Dominic A. Kalangi alikuwa ameajiriwa na Shirika la Posta Tanzania (Tanzania Posts Corporation) TPC, mkoa wa Lindi kama Meneja.

-Tarehe 10/07/2017 alifutwa kazi kwa madai ya utovu wa nidhamu uliokithiri (gross misconduct) na kukosa uaminifu (dishonesty).

-Dominic hakuridhia hicho kitendo cha kufutwa kazi, akaenda kushtaki au kulalamika kwenye Commission for Mediation and Arbitration (CMA) yaani Tume ya Usuluhishi na Uamuzi/Upatanishi.

MBELE YA TUME:

-Akashindwa mbele ya Tume (CMA).

-Tume baada ya kuwasikiliza ikasema kwamba mkataba wake wa ajira ulifutwa kihalali.

-Dominic hakuridhika. Akaenda Mahakama Kuu kuomba maamuzi ya Tume yapitiwe upya (Revision).

MAHAKAMA KUU:

-Akashindwa Mahakama Kuu lakini ikaamuliwa alipwe fidia.

-Kwamba, ingawa maombi yake yalitupiliwa mbali na Mahakama Kuu ikasema alifutwa kazi kihalali, hapo hapo ikasema mwajiri alishindwa kuzingatia urefu wa muda ambao Dominic amemfanyia kazi pasipo kusababisha hasara yoyote au kuvunja utaratibu wowote wa mwajiri. Na kwa hilo tu, Mahakama ikasema mwajiri amlipe fidia ya mshahara wa miezi sita (6).

-Hapo ndipo Shirika la Posta Tanzania (Tanzania Posts Corporation) TPC, lilipokereka na kuamua kukata rufaa kwenda Mahakama ya Rufaa.

MAHAKAMA YA RUFAA:

-Kesi ilisikilizwa na Majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa.

- Kwenye rufaa, TPC ililalamika kwamba, kwa kuwa tayari Mahakama Kuu iliona Dominic alifutwa kazi kihalali, basi haikutakiwa tena kuamuru alipwe fidia ya mshahara wa miezi sita (6) bila msingi wowote kisheria.

-TPC iliwakilishwa na Mawakili watano.

-Wakili mmoja wa TPC (Mr. Mtae) akaibua hoja kwamba, kwanza Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) na Mahakama Kuu walikosea kusikiliza na kuamua mgogoro wa kazi ambao mlalamikaji alikuwa ni MTUMISHI WA UMMA (public servant).

-Kwa lugha nyingine, Wakili alikuwa anawaomba Majaji wa Mahakama ya Rufaa kujibu swali la je, Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) ilikuwa na mamlaka ya kusikiliza na kuamua mgogoro wa kazi (ajira) unaohusu MTUMISHI WA UMMA?

-Wakili mwingine wa TPC (Miss Kinyasi) akawasilisha kwa niaba ya wenzake kwamba, CMA haikuwa na mamlaka ya kuamua hii kesi.

-Wakili akairejesha Mahakama kwenye sheria iliyoanzisha Shirika la Posta Tanzania (Tanzania Posts Corporation Act (Cap 303 R.E 2019)).

-Wakili akasema Shirika la Posta Tanzania ni shirika la umma (public corporation) ambalo mwenyekiti wake wa bodi ya wakurugenzi huchaguliwa na Rais na majukumu yake yanasimamiwa na Wizara inayohusika na mambo ya Posta.

-Kwa hiyo kabla ya kufutwa kazi, Dominic alikuwa mtumishi wa umma.

-Na Dominic mwenyewe akakubali alikuwa mtumishi wa umma.

-Wakili akaendelea kuiambia Mahakama kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 25 cha sheria ya Utumishi wa Umma, kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2016, Dominic alipaswa kupeleka malalamiko yake kwenye Public Service Commission kwa njia ya rufaa .

-Pia kifungu namba 32A kilicholetwa na marekebisho hayo ya mwaka 2016, kinamtaka mtumishi wa umma kupitia kwanza kwenye mifumo ya kutatua migogoro iliyopo kwenye Sheria ya Utumishi wa umma.

-Kwa hiyo mlalamikaji (Dominic) alitakiwa kwanza apeleke malalamiko yake mbele ya Public Service Commission kabla ya kukimbilia CMA.

-Kabla ya marekebisho hayo ya Sheria ya mwaka 2016, migogoro yote ya kazi inayowahusu watumishi wa umma ilikuwa inapelekwa CMA.

-Lakini, kwa vile mkataba wa kazi wa mlalamikaji ulifutwa tarehe 10/07/2017, baada ya kutungwa kwa sheria mpya, hivyo ilikuwa ni makosa kwa mlalamikaji kupeleka malalamiko yake Tume (CMA) tarehe 27/07/2017 kinyume cha sheria mpya.

-Wakili (Miss. Kinyasi) akamalizia kwa kuiomba Mahakama iridhie hayo maelezo na kisha itupilie mbali na kuweka kando mwenendo na maamuzi ya Tume (CMA) na Mahakama Kuu, kwa kuwa walisikiliza kesi ambayo hawana mamlaka.

-Mlalamikaji (Dominic) yeye hakuwa na Wakili, hivyo hakuwa na mambo mengi ya kusema.

-Akajibu tu kwamba, baada ya kufutwa kazi alikata rufaa kwa Mkuu wa Shirika la Posta (Post Master General) ambapo alishauriwa kupeleka malalamiko yake kwenye Tume (CMA).

-Hivyo anaona kitendo cha Shirika la Posta kurudi na kusema kwamba alitakiwa akate rufaa kwenye Public Service Commission, wakati wao ndio waliomshauri aende kwenye Tume (CMA), huko ni kuwa ndumila kuwili.

-Mlalamikaji akaiomba Mahakama iendelee tu kusikiliza kesi (rufaa) na kutoa uamuzi.

MAAMUZI YA MAHAKAMA YA RUFANI:

-Mahakama ya Rufani ikasema kwamba, Wakili wa TPC ( Miss Kinyasi) ametoa hoja zilizonyooka na zenye nguvu kuthibitisha kwamba Tume (CMA) haikuwa na mamlaka ya kusikiliza hii kesi.

-Kwa kuongezea, Mahakama ya Rufaa ikasema kabla haijahitimisha na kuchukua maamuzi sawasawa na maelezo ya Wakili Miss Kinyasi, inabidi kwanza itoe somo kuhusu hii mada.

-Na njia bora kabisa ya kutufikisha kwenye hitimisho husika ni kuainisha na kuchambua vifungu vyote vya sheria ambavyo vinatoa mwanga kuhusu hii mada.

-Kifungu cha kwanza ni kifungu namba tatu cha Sheria ya Utumishi wa Umma (section 3 of the Public Service Act) ambacho kinaeleza maana ya MTUMISHI WA UMMA (public servant) na maana ya OFISI YA UTUMISHI WA UMMA (public service office) - Sitakinukuu hapa (unaweza kusoma sheria husika).

-Pia, Shirika la Posta Tanzania (TPC) limeanzishwa na sheria ya Bunge na linamilikiwa lote au kwa sehemu kubwa na Serikali.

-Hivyo, Shirika la Posta Tanzania ni taasisi ya utumishi wa umma ambayo mojawapo ya Majukumu yake, ni kuupatia umma huduma za Posta kitaifa na Kimataifa na huduma zingine. Ukisoma kifungu namba nane (8) cha Sheria ya Shirika la Posta.

-Hii inawiana kabisa na kanuni za utumishi wa umma (Standing Orders for the Public Service, 2009 (GN No. 493 of 2009) ambazo zinaelezea maana ya UTUMISHI WA UMMA. (Sitanukuu).

-Vyote hivyo vinathibitisha kwamba, wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) ni watumishi wa umma.

-Kifungu cha 31(1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma kinasema watumishi kwenye mashirika na taasisi za Serikali, kama vile Shirika la Posta Tanzania, wanatakiwa kuongozwa na vifungu vya sheria vinavyoanzisha shirika au taasisi husika.

-Lakini kifungu kidogo cha pili 31(2) cha Sheria hiyo hiyo, kinasema ni lazima, watumishi wa umma waliotajwa kwenye kifungu cha 31 kuongozwa na vifungu vya sheria ya utumishi wa umma.

-Hivyo katika mazingira ya hii kesi, Tume (CMA) haina Mamlaka ya kusikiliza na kuamua migogoro ya ajira (kazi) inayowahusu watumishi wa umma, kwa mujibu wa kifungu cha 32A kilichorejewa na Wakili wa TPC (Miss Kinyasi).

Kifungu hicho cha 32A (cha Sheria ya Utumishi wa umma) kinasema, mtumishi wa umma, kabla ya kutafuta nafuu (suluhu) zilizotolewa kwenye sheria za ajira, lazima atafute kwanza suluhu (nafuu) zilizopo kwenye sheria hii (Public service Act).

-(Nafuu au suluhu au remedies zenyewe zipo kifungu cha 25(1)(a) na (b) cha Sheria ya Utumishi wa Umma yaan Public Service Act).

-Mahakama ya Rufaa ikasema, Mlalamikaji kwenye hii kesi alikuwa mtumishi wa umma, kwa hiyo baada ya mkataba wake wa ajira kufutwa, ikiwa amekereka, alitakiwa afate kifungu cha 25(1)(a) na (b) cha Sheria ya Utumishi wa Umma.

-Kifungu hicho kinasema kwamba mtumishi wa umma akishushwa cheo au kupunguziwa mshahara au kufutwa kazi, anatakiwa kukata rufaa kwenye Public Service Commission.

-Kama mtumishi wa umma hataridhika tena, atakata rufaa kwa Rais ambaye uamuzi wake utakuwa wa mwisho.

-Mahakama ya Rufaa ikamalizia kwa kusema, kwa mujibu wa kifungu hicho, migogoro yote ya utovu wa nidhamu au migogoro yote inayohusu watumishi wa umma, iko ndani ya mamlaka ya Public Service Commission ambayo maamuzi yake yanakatiwa rufaa kwa Rais.

-Nanukuu “all disciplinary matters or disputes involving public servants are exclusively within the domain of the Public Service Commission whose decision is appelable to the President.”

-Kwa hiyo Commission for Mediation and Arbitration (CMA) yaani Tume ya Usuluhishi na Uamuzi/Upatanishi haina mamlaka ya kusikiliza na kuamua migogoro ya ajira inayohusu watumishi wa umma.

-Shirika la Posta Tanzania likashinda kesi.

-Mahakama ikasema rufaa ina mashiko.

-Mwenendo na maamuzi ya Tume (CMA) na Mahakama Kuu vikatupiliwa mbali na kuwekwa kando.

Kesi nzima ipo mtandaoni (website ya tanzlii) kwa lugha ya kiingereza. Andika “Tanzania Posts Corporation v Dominic A Kalangi, Civil Appeal No. 12 of 2022.”

Zingatia: Hii Hukumu ilitolewa tarehe 28/03/2022. Hivyo unaposoma leo andiko hili, angalia kama kuna kesi nyingine au sheria mpya ambayo imepindua huu uamuzi.

Imeandaliwa na kutafsiriwa kwa kiswahili nami Zakaria. (0754575246 - WhatsApp).

Hoby: Strong legal research, writing and organizational skills.

Unaruhisiwa ku-share ila usibadili content (yaliyomo).

Nawasilisha.
 
sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,647
2,311

Safi sana mkuu, tafsiri nzuri kufanya jambo lieleweke kwa urahisi kabisa
 
Myhope

Senior Member
Jul 20, 2017
152
65
Kama mgogoro ulitokea 2017 kabla ya mabadiliko ya hiyo sheria mwaka 2019 je?
 
sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,647
2,311
Kama mgogoro ulitokea 2017 kabla ya mabadiliko ya hiyo sheria mwaka 2019 je?
Utaambiwa uende tume ya utumishi wa umma. Wao wanasema baada ya 2017 CMA haina mamlaka ya kupokea na kusikiliza migogoro ihusuyo watumishi wa umma. Hivyo ishu sio mgogoro kutokea kabla au baada ya 2017, ishu wanayoikomalia ni kuwa baada ya 2017 huwezi kwenda CMA hata kama mgogoro ulikuwa ni wa 2015.
 
Myhope

Senior Member
Jul 20, 2017
152
65
Utaambiwa uende tume ya utumishi wa umma. Wao wanasema baada ya 2017 CMA haina mamlaka ya kupokea na kusikiliza migogoro ihusuyo watumishi wa umma. Hivyo ishu sio mgogoro kutokea kabla au baada ya 2017, ishu wanayoikomalia ni kuwa baada ya 2017 huwezi kwenda CMA hata kama mgogoro ulikuwa ni wa 2015.
Na huko Tume ya utumishi wa umma huo mgogoro kama Mahakama imeamuru uende huko utapokelewa au utakuwa nje ya muda?
 
sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,647
2,311
Na huko Tume ya utumishi wa umma huo mgogoro kama Mahakama imeamuru uende huko utapokelewa au utakuwa nje ya muda?
Utakuwa nje ya muda, kwa hiyo utatakiwa kuomba uruhusiwe kupokelewa nje ya muda. Suala la msingi ni kuwa huko tume ya utumishi hawasikilizi migogoro ikiwa mipya bali wanasikiliza rufaa zitokanazo na maamuzi ya mamlaka za nidhamu. Kwa hiyo utaenda kupoteza muda tu
 
ikiumasema

JF-Expert Member
Oct 9, 2015
740
884
Mimi nilifutwa kazi baada ya utoro wa siku 56.....lakini sikupewa nafasi ya kusikilizwa Wala barua ya kufutwa kazi mpaka leo sijapewa nasikia tu ipo kwa mkuu wa shule....huu ni mwaka wa pili je hapa Kuna uwezekano wa kukata rufaa?
 
Uwezekano upo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

4 Reactions
Reply
Top Bottom