Sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi inabagua watumishi wa umma na ambao sio watumishi wa umma

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,315
12,614
Bunge limepitisha mswada uliopelekwa bungeni na serikali kufanya mabadiliko ya katiba kwenye kipengele cha tume ya uchanguzi.

Sasa kwa sheria mpya iliyopitishwa na bunge wakurugenzi wa wilaya na mamea wataacha kuwa wasimamizi wa uchaguzi moja kwa moja kutokana na nafasi zao wilayani. Badala yake wasimamizi wa uchaguzi watatokana na watumishi wa umma; yaani walioajiliwa na serikali inayotawala na inayowalipa mishahara Yao na kuwapandisha vyeo (wako kwenye kanzidata ya serikali na payroll yao) tu.

Kama sheria inabagua raia wake kati ya watumishi wa umma na wasio watumishi wa umma sheria hiyo ni batiri, inatakiwa kuangaliwa upya. Watumishi wa umma ni kundi dogo sana dhidi ya kundi kubwa la wasiokuwa watumishi wa umma. Na Kuna watu wengi wenye sifa za kuwa watumishi wa umma lakini hawakupata nafasi ya kupata ajira kwenye utumishi wa umma. Na Kuna watu waadilifu na weledi walioko nje ya utumishi wa umma ambao wangeweza kufanya kazi kwenye tume ya uchanguzi vizuri sana kuliko walioko kwenye utumishi wa umma.

Sheria hii itizamwe upya.
 
Kwani wanashindwa nini kuweka sheria ambayo itaruhusu uwepo wa Maafisa wa Tume Huru ya Uchaguzi kwa ajili ya kusimamia tu uchaguzi mpaka ngazi ya Wilaya, na pia watu hao hao kutumika kwenye maboresho ya daftari la kupigia kura?
 
Hao watu waadilifu na weredi walioko nje mfumo Ndo hawatakiwi kusimamia wataleta uadilifu wao kuwatoa watawala
 
Kwani wanashindwa nini kuweka sheria ambayo itaruhusu uwepo wa Maafisa wa Tume Huru ya Uchaguzi kwa ajili ya kusimamia tu uchaguzi mpaka ngazi ya Wilaya, na pia watu hao hao kutumika kwenye maboresho ya daftari la kupigia kura?
Hivi hata kama wewe ungekuwa ccm huo ushauri ungeukubali kweli?
 
Wakurugenzi wa halmashauri ni watumishi wa umma pia :cool: .

Sheria hii haina tofauti na inayobatilishwa. Ile ya zamani ilokuwa inaruhusu pia kutumia watumishi wa umma tofauti na wakurugenzi lakini NEC walikuwa wanawatumia wakurugenzi mara zote.

Kwahiyo kwa sheria mpya sio lazima kuwatumia ma DED lakini inaruhusiwa, kwahiyo NEC wanaweza kuteua wengi kama sio wote wa wasimamizi wawe ma DED kwakua wao pia ni watumishi wa umma.

The devil is in the details.
 
Huwezi chukua mtu tuu kokote na huna taarifa ya uadilifu wake! Nisahihi kuchukuwa watumishi wa serikalini maana wengiwao wanauzalendo na wanauadilifu na uzoefu wa kazi za kiserikali.
 
Bunge limepitisha mswada uliopelekwa bungeni na serikali kufanya mabadiliko ya katiba kwenye kipengele cha tume ya uchanguzi.

Sasa kwa sheria mpya iliyopitishwa na bunge wakurugenzi wa wilaya na mamea wataacha kuwa wasimamizi wa uchaguzi moja kwa moja kutokana na nafasi zao wilayani. Badala yake wasimamizi wa uchaguzi watatokana na watumishi wa umma; yaani walioajiliwa na serikali inayotawala na inayowalipa mishahara Yao na kuwapandisha vyeo (wako kwenye kanzidata ya serikali na payroll yao) tu.

Kama sheria inabagua raia wake kati ya watumishi wa umma na wasio watumishi wa umma sheria hiyo ni batiri, inatakiwa kuangaliwa upya. Watumishi wa umma ni kundi dogo sana dhidi ya kundi kubwa la wasiokuwa watumishi wa umma. Na Kuna watu wengi wenye sifa za kuwa watumishi wa umma lakini hawakupata nafasi ya kupata ajira kwenye utumishi wa umma. Na Kuna watu waadilifu na weledi walioko nje ya utumishi wa umma ambao wangeweza kufanya kazi kwenye tume ya uchanguzi vizuri sana kuliko walioko kwenye utumishi wa umma.

Sheria hii itizamwe upya.
Kama siyo watumishi utawajuaje uadilifu wao.

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Kwamba uchaguzi usimamiwe na mtu yeyote yule ilimradi awe mtz..? 🤔🤔🤔
 
Bunge limepitisha mswada uliopelekwa bungeni na serikali kufanya mabadiliko ya katiba kwenye kipengele cha tume ya uchanguzi.

Sasa kwa sheria mpya iliyopitishwa na bunge wakurugenzi wa wilaya na mamea wataacha kuwa wasimamizi wa uchaguzi moja kwa moja kutokana na nafasi zao wilayani. Badala yake wasimamizi wa uchaguzi watatokana na watumishi wa umma; yaani walioajiliwa na serikali inayotawala na inayowalipa mishahara Yao na kuwapandisha vyeo (wako kwenye kanzidata ya serikali na payroll yao) tu.

Kama sheria inabagua raia wake kati ya watumishi wa umma na wasio watumishi wa umma sheria hiyo ni batiri, inatakiwa kuangaliwa upya. Watumishi wa umma ni kundi dogo sana dhidi ya kundi kubwa la wasiokuwa watumishi wa umma. Na Kuna watu wengi wenye sifa za kuwa watumishi wa umma lakini hawakupata nafasi ya kupata ajira kwenye utumishi wa umma. Na Kuna watu waadilifu na weledi walioko nje ya utumishi wa umma ambao wangeweza kufanya kazi kwenye tume ya uchanguzi vizuri sana kuliko walioko kwenye utumishi wa umma.

Sheria hii itizamwe upya.
Nilidhani unachohoji ni kuwa, je wakurugenzi wa halmashauri au wa mashirika ya umma siyo watumishi wa umma? Au sheria ilikusudia kutaja watumishi waandamizi katika Serikali Kuu (Civil Service)? Kumbe wewe unahoji kama mtu ye yote ambaye angeweza kuajiriwa kama mtumishi mwandamizi wa Umma?
 
Back
Top Bottom