Ridhiwani Kikwete awaasa Watumishi wa Umma kutokuwa na hofu na mfumo mpya wa tathimini ya Watumishi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,988
Snapinsta.app_409726581_18079525939419322_7331547905545557381_n_1080.jpg
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma, Ridhiwani Kikwete amesema Mfumo Mpya wa Tathimini ya Watumishi wa Umma (SAU) hauna lengo la kumuondoa kazini ama kuwaonea watumishi wa umma hivyo hawana sababu ya kuuhofia mfumo huo.

Kikwete amebainisha hayo leo Desemba, 13, 2023 wakati wa ufungaji wa mafunzo ya siku tatu kwa watumishi wa umma kutoka Taasisi ya Tiba ya Mufupa na Ubongo Muhimbili (MOI) Shirika la Masoko Kariakoo na Bodi ya Sukari Tanzania yaliyofanyika MOI.
Snapinsta.app_409724552_18079525966419322_6212528756456784644_n_1080.jpg

Snapinsta.app_409716441_18079525993419322_2235682711296340309_n_1080.jpg
Amesema lengo la mfumo huo ni kuiwezesha kupima utendaji wa watumishi wake kwa njia rahisi na kuongeza ufanisi wenye tija kazini.

“Mfumo hauna lengo la kukomoa watu, tutakuwa na utumishi wa umma unaotimiza majukumu, utawezesha kupamga utumishi wenye tija, huna sababu ya kuhofia” amesema Mhe: Kikwete

Aidha aliipongeza MOI kwa kutoa huduma bora kwa Watanzania na kuitaka kuendelea na kasi hiyo kwa maslahi ya umma.

“MOI inaendelea kuwa bora hii yote ni juhudi zako Profesa Makubi na timu yako, hongera sana, tunahitaji utumishi wenye tija” amesema.

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Prof. Abel Makubi akimkaribisha Naibu Waziri huyo alimpongeza kwa kuitembelea MOI mara kwa mara na kwamba htua hiyo inaongeza ari kwa watumishi kufanya kazi kwa umahiri.
Snapinsta.app_409741259_18079525975419322_646630836916824774_n_1080.jpg
 
Professor alikuwa na haja Gani ya kuvaa hicho kidude shingoni na Yuko mkutanoni tena na mwanasiasa kama Ridhimoko au ndio nidhamu ya uoga?

Back
Top Bottom