Ngoja waje wenyewe , maana kuna watu wanawasifia humu hadi Bendera zao kujaa kila mahali kuliko kupenda ndugu zao weusi.
Kuna Mambo mengi sana ya kujifunza kupitia ubaguzi wao pia, Waafrika hatupendi ukweli maana ni mchungu kuusikia, Ni aibu Afrika kuwa Maskini, na miongoni mwa sababu kuu ni kutowekeza katika kufikiri,kujifunza; kujithamini na kupoteza muda.
Hawa wenzetu hukatwa fedha zao (KODI) kwa ajili ya kusaidia Afrika hupata uchungu sana misaada hiyo inapotumika vibaya, maana kwa wengine ni wanufaika wa hii missada (WAPIGA DILI) na mwisho malengo kutotimia,
Africa tuna wasomi wengi wa ngazi mbalimbali lakini hawatamani kufanya kazi nyumbani sababu kuu ukiwauliza utajibiwa mazingira ya kufanya kazi nyumbani Africa ni magumu sana..! Wanataka ulaya kwa weupe, Lazima watuchukuie tu.
Afrika ni wachache wa kuhesabika wenye utajiri usio shaka kiasi hata Nchi zao zinajivunia kuwa nao kwamba wanapenda nchi zao wanalipa kodi zao kwa usahihi lakini Waafrika walio wengi Utajiri unapatikana kwa uchawi na mazingaombwe na kafara na hufulisika ghafla kwa kuwa walikosea masharti ya matunguli yao. hatuwezi kuendelea kwa namna hii lazima tuchukiwe tu na weupe, Demokrasia kwa wenzetu weupe inajengwakwa hoja lakini Afrika ni kutukanana hadharani, uongo, uzushi, matusi ya kuvuana nguo ,uadui, machafuko ni lazima tuchukiwe tu.
Tunapenda kupoteza muda kwa mambo ambayo yanazidi kutia umaskini kabisa mfano leo hii Tamaduni na mila za mikusanyiko ya ngoma, ambayo sehemu kubwa humalizika au hufanyika zinaa zisizo na mfano maana watu hawajithamini kabisa tunategemea weupe wakatwe fedha zao ili zinunue madawa ya kupunguza makali ya maambukizi ya ukimwi kwa kujitakia kabisa lazima watuchukie tu'
Afrika kuna rutuba nzuri sana yenye kuzalisha aina karbu zote za mazao tangu ya chakula hata ya viwandani lakini kuna njaa na umaskini wa kutupwa unaotuzunguka,
Ni Afrika tu tunazungumzia ukabila udini na kujitenga sisi kwa sisi na mapigano ya wenyewew kwa wenyewe hii ndio Afrika , kwa ujumla wake lazima tuonekane kaqma tumelaaniwa mbele za weupe.