Watu wawili wauawa kwa kuchinjwa kisa wivu wa mapenzi

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni wapenzi Katalina Juma (21) na Athanas Alyen ( 23) wakazi wa Kata ya Kabungu, Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi wamekutwa wakiwa wameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali, huku chanzo kikidiwa ni wivu wa mapenzi.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Oktoba 19, 2023 katika Kitongoji cha Imbambe, Kijiji Cha Kagwira, Kata ya Kabungu, ambapo marehemu hao wamekutwa wamefariki dunia kwa kuchinjwa na kutupwa pembezoni mwa barabara.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kagwira, Shila Benedicto amesema marehemu hao walikutwa na madhila hiyo wakiwa njiani kurudi nyumbani wakitokea Kijiji cha Kabungu walikokuwa wakifanyia shughuli zao.

Akithibitisha kutokea tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Kaster Ngonyani amesema wanawashikilia watu wawili kwa ajili ya mahojiano, huku akieleza kuwa tukio hilo lina sura ya wivu wa kimapenzi kwa kuwa wamebaini mmoja wa marehemu alikuwa akiwasiliana na watu ambao walikuwa wapenzi wake.

Kamanda ngonyani amesema Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi wa tukio hilo na mara utakapokamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani.
 
Watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni wapenzi Katalina Juma (21) na Athanas Alyen ( 23) wakazi wa Kata ya Kabungu, Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi wamekutwa wakiwa wameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali, huku chanzo kikidiwa ni wivu wa mapenzi...
Utelezi ni kitu mbaya Lakini tamu sana
 
Mi mwenyewe hapa nusura nihusishwe katika tukio la wivu wa kimapenzi wakati vijana wawili wakituangana makonde baada ya kijana mmoja anayedai kuwa ni mmiliki wa msichana kumtuhumu kijana mwenzake amemkuta akichati naye. Kijana mwenye binti ndiye aliyeshambuliwa zaidi japo yeye ndiye aliyeonesha wivu kwa kuanzisha ugomvi.

Mimi nilihusishwa kuwa huwa namtongoza binti huyo na tayari nilishapewa onyo kwa kutukanwa vibaya ila sikuacha kumtongoza huyo binti kwa kuwa alinieleza kuwa huyo jamaa yake mwenye wivu ni mpenzi tu na si mume anayetambulika, ndio na mimi nikaona nipambanie kumpata binti huyo. Ugomvi wa vijana hao ulinifanya nijitoe kumtaka binti huyo isiwe taabu.

Ni bora kama mtu ana mpenzi aseme wazi tu ana mtu na hakuna nafasi ya kuchepuka kwa mwingine itasaidia kuepusha wivu na kutokea madhara
 
Watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni wapenzi Katalina Juma (21) na Athanas Alyen ( 23) wakazi wa Kata ya Kabungu, Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi wamekutwa wakiwa wameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali, huku chanzo kikidiwa ni wivu wa mapenzi.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Oktoba 19, 2023 katika Kitongoji cha Imbambe, Kijiji Cha Kagwira, Kata ya Kabungu, ambapo marehemu hao wamekutwa wamefariki dunia kwa kuchinjwa na kutupwa pembezoni mwa barabara.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kagwira, Shila Benedicto amesema marehemu hao walikutwa na madhila hiyo wakiwa njiani kurudi nyumbani wakitokea Kijiji cha Kabungu walikokuwa wakifanyia shughuli zao.

Akithibitisha kutokea tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Kaster Ngonyani amesema wanawashikilia watu wawili kwa ajili ya mahojiano, huku akieleza kuwa tukio hilo lina sura ya wivu wa kimapenzi kwa kuwa wamebaini mmoja wa marehemu alikuwa akiwasiliana na watu ambao walikuwa wapenzi wake.

Kamanda ngonyani amesema Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi wa tukio hilo na mara utakapokamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani.
Sasa wote wawili iwe wivu hebu fuatilieni vzr
 
Back
Top Bottom