Mbeya: Mume amuua mkewe kwa kumchinja na kutenganisha kichwa na kiwiliwili

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
Simanzi na vilio vimetawala kwa wakazi wa kitongoji cha Masista kijiji cha Lusese Kata ya Igurusi baada ya Omben Kilawa mkazi wa kijiji hicho wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kumuua mke wake Happness Mwinuka kwa kumchinja na kutenganisha kichwa na Kiwiliwili.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 7.00 usiku wa kuamkia leo Machi 13, 2024 ambapo jirani amesema alisikia kelele kama watu wanagombana lakini baada ya nusu saa kukawa kimya na kuamua kupiga yowe ndipo watu walipojitokeza na polisi kufika wamelibomoa mlango wa chumbani kwao na baada ya kuingia Kilawa alikuwa ameshatekeleza mauaji kwa kumchinja mke wake na kwa kutenganisha kichwa na kiwiliwili.

Ombeni.png

==================

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Ombeni Manase Kilawa [43] mkazi wa Lusese Wilaya ya Mbarali anayetuhumiwa kumuua mke wake aitwaye Happynes Gervas Mwinuka [40] mkazi wa Kijiji cha Lusese kwa kumkata na kitu chenye ncha kali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP Benjamin Kuzaga amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Machi 13, 2024 Kitongoji cha Masista, Kijiji cha Lusese, Wilaya ya Mbarali baada ya kutokea ugomvi baina ya wana ndoa hao wakiwa nyumbani kwao na kupelekea mtuhumiwa Ombeni Kilawa kuchukua kisu na kumkata mke wake shingoni.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi baada ya mtuhumiwa kumhisi na kumtuhumu mke wake kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Wanaume wengine.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, linatoa wito kwa jamii kuwa pindi wanapopatwa na tatizo au changamoto katika ndoa zao isiwe suluhisho lake kujichukulia sheria mkononi bali ni kutafuta ushauri kwa wazazi, walezi, wasimamizi wa ndoa, viongozi wa dini, katika madawati ya jinsia na watoto waliopo kila Wilaya ya Kipolisi, katika ofisi za halmashauri au kutafuta haki kwenye Mahakama ili kuepuka madhara.
 
Simanzi na vilio vimetawala kwa wakazi wa kitongoji cha Masista kijiji cha Lusese Kata ya Igurusi baada ya Omben Kilawa mkazi wa kijiji hicho wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kumuua mke wake Happness Mwinuka kwa kumchinja na kutenganisha kichwa na Kiwiliwili.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 7.00 usiku wa kuamkia leo Machi 13, 2024 ambapo jirani amesema alisikia kelele kama watu wanagombana lakini baada ya nusu saa kukawa kimya na kuamua kupiga yowe ndipo watu walipojitokeza na polisi kufika wamelibomoa mlango wa chumbani kwao na baada ya kuingia Kilawa alikuwa ameshatekeleza mauaji kwa kumchinja mke wake na kwa kutenganisha kichwa na kiwiliwili.

Hatari sana.
Taasisi ya Ndoa inazidi kupata pigo kubwa sana karibu kila siku, inazidi kuelekea kibra.
Kupitia matukio kama haya, Watu wa 'Kataa Ndoa' wanazidi kupata Credits za kutosha, wanakaribia kupata ushindi siku siyo nyingi.
 
Watu hua wanadharau wasomi na Elimu, lakini kuna uhusiano mkubwa sana kati ya matukio ya ajabu ajabu na Elimu ndogo. Ni nadra sana, narudia tena ni nadra sana kwa wasomi wa Elimu angalau ya Chuo kusikia wanafanya matukio ya namna hii. Lakini pia kuna uhusiano mkubwa sana kati ya hali duni ya kimaisha na matukio ya ajabu ajabu. Sijawahi kusikia mtu mwenye ukwasi anaanguka majini, kupandisha mashetani ama anaenda kushinda kwa Mwamposa ili aombewe apate rizki bila kufanya kazi. Umaskini, ufukara, hali duni za kimaisha, kipato duni na kukosa elimu hivi vitu vinaleta msongo wa mawazo (stress) na kupelekea watu kufanya matukio ya ajabu ajabu kama haya. Katika hali ya kawaida huwezi kua unafikiria kuua ua ama kuuana uana tu kama ndo solution ya matatizo yako na mwenzako
 
Hawa jamaa wa Mbeya bwana, kila kitu kibaya kinatoka kwao...kuanzia kuchunana ngozi miaka ya 90 huko.
Kuna kipindi Rfa kilikua kinaitwa Matukio, kilikua asubuhimida ya saa 1. 70% ya matukio yaliyokua yanalipotiwa yalikua yanatoka mbeya. Uchawi, ujambazi, Kuchuna ngozi, mauaji, wizi, nk nk. Matapeli wote wa kidini 60%wanatoka mbeya.

Hawa jamaa kwenye uhalifu wanaongoza aisee...
 
Back
Top Bottom