Muuza Kangala
JF-Expert Member
- Jul 21, 2021
- 1,238
- 4,807
Watu wawili akiwemo mke na mume wamekutwa wamefariki katika maeneo tofauti tofauti baada ya mume kudaiwa kumuua mkewe na kumtupa eneo la Mafisa kwa Mambi na yeye kukutwa amejiua katika eneo la Bigwa Manispaa ya Morogoro.
Akizungumzia tukio hilo lililotokea usiku wa kuamki leo, kamanda wa jeshi la polisi mkoani Morogoro Alex Mkama amesema chanzo cha mauaji hayo inasemekana kuwa ni wivu wa mapenzi.
Kamanda Mkama amesema kuwa mwili wa mwanamke huyo ulikutwa umetupwa katika eneo hilo majira ya saa moja asubuhi na mwanamke huyo alitambuliwa kwa jina la Devotha Gilbert na mwanaume huyo ambaye ametekeleza mauaji hayo ametambulika kwa jina la Boniface John mwenye umri wa miaka 26
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa Mafisa kwa Mambi amekiri kuwepo kwa matukio mbalimbali ya mauaji katika eneo hilo na hili ni tukio la tatu kutokea katika eneo lake
Jambo TV