Watoto wa vigogo na ajira BoT

Watoto wa vigogo na ajira BoT

TRA nilitoka 2010 nikajiunga na BoT. Unadhani ni long sana kamaunavyotaka kuaminisha watu hapa? Sema tu watu wakiitwa kwenye interviewswakapiga zile Aptitude Tests na kuchemsha wanaanza mbwembwe, mara "ooh, paleBoT/TRA huwezi kupata kama wewe siyo mtotowa kigogo au labda una ki-memo kutoka kwa kigogo". Aaaah wapi?! Mi sikuwa naki-memo na wala simjui mtu yeyote. Mi ni mtoto wa mkulima wa kawaida kabisa.Ndio maana nikamuuliza mleta uzi, hao anaowasema ni asilimia ngapi ya wafanyakaziwote wa Benki Kuu? Au mnadhani hao mliowataja ndio watoto pekee wa vigogo wotemnaowajua nchi hii? Porojo zingine zinafaa kupelekwa kwenye vijiwe vya kahawana wala siyo hapa kwa Great Thinkers!

Mkuu uwe unatumwagia fasta vacancies zikitoka BOT, one day yes nataka nifanye kazi hapo. Mbona hamna nafasi za kazi mara kwa mara? natembelea sana website yenu..
 
No, hata kama wana qualifications, sikubali kuwa hii ni coincidence.
 
Hapo kwenye red ni kama umejichanganya.

Kama wanaqualify na wanamudu kazi zao na walishindanishwa sioni ubaya BUT kama ni upendeleo shame on them.

hapo ndio mwisho wako wa kufikiri.
 
Watanzania acheni uvivu wa kufikri na kuishia kulalamika SOMENI kwani lazima uajiriwe BoT na TRA? Pigeni shule za maana (business, Accounts, Economics, Engineering) sio BA Kiswahili, au BA Archeology, BA Korean Language halafu utegemee utaajiriwa taasisi nyeti zenye kulipa mshahara wa aina ya BoT na TRA
 
Kama wana-Qualify wacha wapige kazi kwani hamjui kazi za siku hizi si za umesoma nini ila ni unamjua nani?
Na hii ipo hata kwenye mashirika binafsi na hata wewe ukipata nafasi utafanya vivyo vivyo.
Shida hapa tunalalama sababu hatuna nafasi.PERIOD.
,kweli ndugu yangu ester karamagi.vipi bado uko colombia university?wewe nafasi yako ni ile aliyokuwa nayo january makamba,katibu wa rais.hongereni,unasubiriwa kwa hamu
 
Tatizo kubwa la waafrika hawajui kulea watoto, unakuta mtu kalea watoto kama mayai na hawafunzwi ukweli wa maisha.

Utasikia fulani baba ama mama yake hana hela lakini akiondoka 'breadwinner' all of a sudden na hile hela haipo tena.

Inaamanisha wengi tunao waita vigogo leo (except kwa wachache) ni kwa sababu wapo kwenye system tu iliyojaa ubadhirifu na kuweza ku sustain ka lifestyle fulani. Akiondoka muhusika ni kasheshe, ndio maana kuna wanauona ulazima wa kuwapachika watoto zao kwenye system.

Lakini kiongozi yeyote ambae kalea m/wanawe vizuri na kumpa/wapa misingi imara ya maisha na ukweli wa maisha hana sababu hizo za kumpachika mwanawe.

Tanzania is pretty much an open canvas. Kama wakenya wanaililia, waganda wanaivamia na wazungu wanaiombea ibakie chini ya CCM, then you know the potential is there.

Point ni kwamba viongozi wanaopachika watoto zao kwa asilimia kubwa hawakulea vizuri watoto, except for those who gained their position with merit.

Binafsi siono sababu ya kudandia treni wakati nchi imejaa mali, why even be employed.
 
Kuwa mtoto wa kigogo siyo recipe ya kunyimwa fursa. Kama kuna ushahidi wa mtu kupendelewa leteni tujadili, lakini kujadili majina tu ni too low!!!
 
Ona nchi yetu ilivyo
FILBART SUMAYE, PAMELA LOWASA, ZARIA KAWAWA,HERIETH LUMBANGA, SALAMA MWINYI,RECHAL MUGANDA, SALMA MAHITA,JUSTINA MUNGAI, KENETH NCHIMBI, BLASIA W. MKAPA, VAOLETH LUHANJO, LIKU KATE KAMBA, THOMAS MONGELA NA JABIRI KIGODA.
HIYO NI TIMU YA WATOTO WA VIGOGO WALIOAJIRIWA BOT BADO KATIKA BALOZI ZETU NJE YA NCHI.NCHI YETU INAFISADIWA NANI WA KUTUOKOA WENGI WAO WAMEGHUSHI ELIMU ZAO
HII MESEJI IMEZAGAA MITAANI KWA SANA SASA SIJUI KWAMBA NI KUJIVUNIA VIONGOZI WETU KUTUONYESHA KUWA ELIMU NI MSINGI WA MAISHA KWA KUWAPA WATOTO WAO ELIMU BORA AU
NI WANANCHI KUONA HUKO NI KUPENDELEANA KATIKA AJIRA ZENYE MASLAHI MAZURI AU
NI WIVU WA WATANZANIA TU?
umesahau na ile kesiya watoto wa vigogo waliofoji vyeti na kuajiliwa bot mmoja wao nimtoto wa mungai haiingii akilini mtoto wa kiongozi aliepata kuwa waziri wa elimu anafoji vyeti na mpaka sasa hii kesi wameizima kimya kimya
 
Mimi ninafamily friend amemaliza masters ya marketing Uingereza miaka mitatu iliyopita tena baba yake kajinyima kamsomesha lakini hadi leo hajapata kazi. kaomba miaka yote hiyo hajaweza kufanikiwa.

Shahada ya kwanza ni ya UDSM. Anatia huruma anaaply kila leo nafasi zinazotoka kwenye magazeti yetu bila kujibiwa. yote hii ni kwa kuwa wazazi wake sio wazito. Naomba km kuna anayeweza kumsaidia tuwasiliane.

Natanguliza shukrani.
 
Sio tu BOT, kuanzia kwenye scholership, Kwenye chama, mawizarani na idara zote nyeti za serikali.Ndio maana mambo mengi sana nchi hii hayaendagi sawa kwenye idara na taasisi zote za serikali.Haiwezekani iwe ni coinsidence kulundikana watoto wa wakubwa pamoja.Sijui wananchi watalalamika kwa nani, manake hata hao wakuwalalamikia ndio walewale...

"Halafu ni wanoko ile mbaya".....pamoja na exposure walizo nazo .....wao bado wanaendeleza zile business as usual ili kulinda maslahi ya wazazi wao.......lol
 
Kama Waliqualify sawa ...kama walingia Kwa Memo ...that's Problem

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
Hata kama waliqualify bado yapo mashaka kwamba ulikuwepo upendeleo wa dhahiri. Hakika nchi hii ina wenyewe. Ningekuwa rais ningeoverhaul mfumo mzima na kuweka timu mpya.
 
Poor families v. Rich families. NADHANI TITLE INGEKAA HIVI INGEVUTIA NA KULETA MAANA XANA.
 
Ninacho jiuliza na sipati majibu mpaka sasa ni hiki, kama imetokea coincidence BOT ikaajiri watoto 14 wa vigogo je, coincidence hiyohiyo inaweza kutokea kwenye wizara ya elimu watoto wenye majina kama hayohayo wakapangwa kwenda kufundisha shule za kata vijijini ambako hakuna maji wala umeme na wakaendelea kuifanya kazi hiyo kwa moyo wa kizalendo bila kujalisha kuwa mishahara imechelewa na hawaja pandishwa vyeo na wakati huohuo wakiidai serikali sikivu malikimbizo?!

Hivi kweli binadamu wote ni sawa kwa maana ya fursa za ajira bila kuangaliana usoni?! Hasa BOT?


Thubutuuu!!!! Kwani wenyewe wanasomeaga Ualimu???
 
"Halafu ni wanoko ile mbaya".....pamoja na exposure walizo nazo .....wao bado wanaendeleza zile business as usual ili kulinda maslahi ya wazazi wao.......lol


Hata ingekuwa wewe Baba yako akikuweka sehemu lazima ungelinda maslahi yake.....Au wewe unaweza Kumchinja baba yako???
 
Chuo cha Taifa cha Uongozi! Kuna matatizo makubwa sana! Haujaona mambo yalivyo?

Comment ni muhimu kwetu!

Sikaona aisee ila nimeona tu ila ninachoona hapa tatizo lililopo ni jopo la watu waliokosa kazi na kianza kuwaonea wivu wenye kazi...
 
uzuri au ubaya wa vita ya wenyewe kwa wenyewe ni kwamba hao wanaobebwa hawata dhurika hata kidogo kwani watakuwa wakwanza kupanda ndege! Nyie mnaopiga makelele na kuombea vita ndio mtakao chinjana mwanzo mwisho!

wauulize mtoto wa ghadafi na utawala wao
 
Pigeni kazi na msome kwa bidii, hatukatai kuwa upendeleo upo sana BOT, lakini jiulizeni watoto wa wakubwa ni % ngapi pale? Watoto wa maskini wapo kibao tu, waliofanya vizuri Economisc wengi tu wameajiriwa, kuanzia mwaka 2005 wimbi la kuajiri watoto wa vigogo BOT limepungua sana kwani kwa sasa wanafuata sana performance!
Ukitaka kulete hoja kama hizi, tueleze uzoefu wao, elimu yao pia, na si kulalamika kwa kuona wivu!

Tuongee ukweli, sidhani hata kama ni wewe una nafasi fulani halafu mtoto wako kamaliza shule eti unamuacha ahangaike wakati unaweka kutumia mafasi yako kumpatia kazi. Maisha hayako sawa, hata enzi za Mitume wote, mtalalamika wee, wenzenu wanakula maisha, pigeni kazi!
 
Back
Top Bottom