ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,017
- 7,220
[watu wnazungumza kuwa eti wana sifa? sawa, lakini je taratibu zilifuatwa? je walipambanishwa na wenye sifa wengine kwa njia ya usaili? kwa kuwa kuwa na sifa ni kitu kingine na kushinda usaili ni kitu kingine, na kwa nini watoto wa akina mwinyi, mkapa, mramba etc peke yao ndo wana sifa? hivyo vyuo wamesoma peke yao?
la msingi.
10 wale wote walioajiriwa bila kufanyiwa usaili wasimamishwe mara moja, iitwe kampuni kama price water house au yenye kuheshimika, nafasi zao zitangazwe upya, wafanyiwe usaili na kama kwa kushindanishwa na wengine wtashinda, MIYE SANA NOMA
2 WALE wengine ambao itabainika kuwa wameajiriwa kwa vimemo, na kuwa hawnan sifa, wafukuzwe na kuchuliwa hatua. waLE wote waliohusika katika kufanikisha mpango huu haramu wa ajira za upendeleo, wakiwemo maafisa utumishi, nk, yaani watimuliwe bila haya na hatua kali dhidi yao.SIJAONA MAHALI GANI KATIKA HILI KUNAHITAJI UCHUNGUZI, KAMA NI MAFAILI YA INTERVIEW YAPO HAPO OFISINI, KAMA NI CV ZIPO, UCHUNGUZI WA NINI?
Tutafute vigezo vingine vya kuwashughulikia lakini sio usaili kwa sababu wote hao wamefanya usaili.
Pale BoT kuna usanii sana, ngoja nikupe mfano huu.
Kuna jamaa mmoja mhandisi alienda kuomba kazi iliyotangazwa na BoT. Alipofika pale siku ya usaili akaambiwa usaili siku hiyo umeahirishwa mpaka utakapotangazwa tena. Baadae akapata taarifa kuwa usaili siku ile ulifanyika na kila mtu aliyekuwepo kwenye usaili aliajiriwa kwa sababu walikuja watu 11 na waliohitajika ni 11 !!! Ukweli ni kwamba sehemu competitive kama BoT idadi ya walioomba kazi haiwezi kuwa eactly the same na idadi ya wanaohitajika.
Tatizo lingine Tanzania ni kwamba watu hawaitumii mahakama ipasavyo, swala kama hili nilitarajia kuwe na kesi kibao mahakamani za wale wanaoamini kuwa hawajatendewa haki katika mchakato wa kuomba kazi BoT na mashirika mengine, lakini hakuna kesi! kila mtu anaishia kulalamika mitaani tu.
Ukiona haujatendewa haki nenda mahakamani mara moja.