Watoto wa vigogo na ajira BoT | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watoto wa vigogo na ajira BoT

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by izihaka, Jan 31, 2008.

 1. i

  izihaka Member

  #1
  Jan 31, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mtawala wa forum hii na wote kwa ujumla napenda kuwapa mada hii iwe kama ni ushahidi mojawapo wa sakata la BoT. Hili suala la watoto wa vigogo kuajiriwa Bot si la uongo kwani

  1. Rogers Sumaye alipata ajira hata kabla hajamaliza shule Uk kwani kuna watu walianza kufanya interview za kumsindikiza.
  2. Kigoda naye the same
  3. Lowasa's the same
  4. And many others who have brothers there or relatives

  Ishu hapa sio kuwa na sifa za kufanya kazi Bot bali je walipitia usahili na taratibu za ajira serikalini?

  Je, ni watu wangapi wenye sifa walifanya interview na kushinda na bado wakapigwa chini?

  Inasikitisha kuona kuwa hata Gavana mpya anatetea maovu akiwa ofisini hata mwezi haujaisha ni SHIDA hii

  May 30, 2008:
  =======
  Baadae: Watoto wa vigogo BoT wasafishwa
  =======

  Oktoba 07, 2012
  Oktoba 23, 2012
   
 2. M

  Mwakilishi JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2008
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 484
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Weka wazi hayo maovu anayotetea gavana mpya basi, hapa ni JF mkuu, where we dare talk openly...toa dukuduku lako.

  To borrow from the old mikingamo radio show "tuambie nani yuko wapi na anafanya nini kulihujumu taifa"
   
 3. F

  Fisadi Mtoto JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2008
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 639
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  KAKA ACHA MAPEPE,UNAJITUNGIA HABARI TU HAPA,KAMA HUNA KIPYA KAA PEMBENI.KWANZA SUMAYE HANA MTOTO ANAEITWA ROGERS,BALI ANA WATOTO WAWILI AMBAO NI FILBERT NA FRANK,PILI FILBERT ALIRUDI NCHINI BAADA YA KUMALIZA MASTERS YAKE YA COMPUTER SCIENCE.NA ALIPORUDI ALIKAA MIEZI NANE AKIFANYA KAZI KTK KAMPUNI BINAFSI NDIO AKAAJILIWA.HUO UZUSHI UMETOA WAPI KAKA?ATA UKIULIZA WATU ALIOSOMA NAO TOSAMAGANGA F 5&6 WATAKWAMBIA JINSI ALIVYO MTU SIMPLE NA WAKUJITUMA.KAZINI KWAKE WANAMTEGEMEA MTAFUTE BOSI WAKE MZEE MASAWE ATAKWAMBIA.PIA WAPO WENYE CPA NA
  NK.WIVUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU MBAYA JAMANI
   
 4. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nyie teteaneni, mkizani hiyo nchi Mungu aliwapa nyie na babazenu hao mafisadi, ila patageuka siku moja hapo mtatafuta pa kujificha mtakosa, maana manyumba, migari yenu watu watachoma, msione kam nyie ndo mmebarikiwa kumbe wezi wakubwa na baba zenu, iko siku tu, itafika, sijui utayazungumza haya??
  Hongera sana kwa kuwa mtoto wa Fisadi, Umebarikiwa sana
   
 5. DMussa

  DMussa JF-Expert Member

  #5
  Jan 31, 2008
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 1,301
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Nimekuwa nikizifuatilia kwa karibu hizi mada zinazohusiana na watoto wa vigogo kupata ajira BOT ila kuna wakati inafikia wachangiaji aidha wanachukua haya masuala kuwa personal. Nadhani hii yote ni kutokana na kukosekana kwa vidhibiti vya kutosha kuhusiana na hii ishu kwa ujumla.

  Mimi binafsi natambua wazi kwamba hakuna ambae angependa mtoto wake apate shida katika dunia hii wakati yeye kama mzazi anao uwezo mkubwa tu wa kumsaidia > Huu ni ubinafsi ambao upo katika kila binadamu (inherent) kinachogomba hapa nadhani ni procedures na appropriateness ya ajira za hawa watoto wa vigogo kuingia BOT kwa wingi kama inavyoonekana. Na je ni kwa nini walimwagwa BOT pekee kwa sababu nina uhakika hii sio bahati mbaya!?

  Kuna mchangiaji mmoja aliwahi kuomba kama kuna mtu anazo data (CV na Position wanazohold BOT) juu ya hawa watu azimwage hapa JF lakini sina uhakika kama kuna mtu alirespond may be hakuna aliyekuwa na access ya hizo data.

  Kwa jinsi hii ninavyoona hapa sidhani kama hii mada itaweza kuadd value kama hakuna Evidence ya kutosha kuthibitisha kinachosemekana. Tutakuwa kila siku tukiona watu wakirushiana maneno kwa kuhisi kwamba waanzisha mada wanasumbuliwa na wivu na sio kutaka uadilifu uwepo ktk serikali na vyombo vyake vyote.

  Let anyone with these data bring them forward for us to scrutinize!

  D
   
 6. F

  Fisadi Mtoto JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2008
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 639
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  NA HAPO NDIPO MTAKUFA NYINYI NA WAJUKUU ZENU WENGINE TUTAPAA KWENDA ZETU NG'AMBO KUENDELEA KULA MAISHA.NANI ALIEKWAMBIA VITA VYA KONY VINAMGUSA MUSEVEN NA FAMILIA YAKE?
   
 7. Sura-ya-Kwanza

  Sura-ya-Kwanza JF-Expert Member

  #7
  Jan 31, 2008
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 561
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hii kitu mbona imeshazungumziwa jamani. Mwanzishaji wa hii thread inabidi afanye kuperuzi kabla ya kumwaga hizi pumba, zimeshachambuliwa!
   
 8. K

  Kinabo Member

  #8
  Feb 1, 2008
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 75
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Kila mzazi angependa mtoto wake apate kazi nzuri na yenye heshima. Kinachotatanisha au kinachotakiwa ni kuwa huyu mtoto anazo sifa sinazotakiwa na anaimudu hiyo kazi?
   
 9. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #9
  Feb 23, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Vigogo watano BoT wasimamishwa kazi
  * Ni wanaodaiwa kuhusika na kashfa ya Richmond


  Na Ramadhan Semtawa


  SAFISHASAFISHA ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imeendelea kufuatia vigogo watano wa benki hiyo kusimamishwa kazi.


  Hatua hiyo imekuja mwezi mmoja baada ya Gavana mpya wa BoT Profesa Benno Ndulu, kufanya mabadiliko mengine katika ngazi za wakurugenzi wa benki hiyo yakiwamo matawi na makao makuu, isipokuwa Mwanza.


  Kwa mujibu wa taarifa zilizofikia gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, vigogo hao walisimamishwa kazi juzi.


  Taarifa hizo ziliongeza kwamba, uamuzi wa BoT kuwasimamisha watumishi hao ni sehemu ya mchakato wa kuisafisha taasisi hiyo nyeti ambayo imekumbwa na tuhuma za ufisadi.


  BoT chini ya aliyekuwa gavana wake, Daud Ballali imekumbwa na tuhuma mbalimbali za ufisadi, ikiwemo ujenzi wa majengo pacha (Twin Towers) ya benki hiyo na wizi wa zaidi ya Sh133 bilioni katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA).


  Taarifa hizo zilifafanua kwamba, kusimamishwa kwa wafanyakazi hao pia kunahusishwa na mapendekezo ya Bunge kuhusu malipo ya ziada ya Sh5 bilioni katika mkataba wa Richmond/Dowans.


  Hata hivyo, akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana jioni Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu alisema taarifa za hatua hiyo zimefikishwa kwenye vyombo husika.


  Profesa Ndulu ambaye hata hivyo alionekana kutotaka kuzungumza moja kwa moja kuhusu suala hilo alisema kwa sasa si sahihi kuanza kueleza majina na nafasi za waliosimamishwa.


  Profesa Ndulu alisema wafanyakazi hao wana haki zao za msingi, hivyo si sahihi kuanza kuwaanika hadharani kupitia vyombo vya habari.


  Hata hivyo, alikiri kufikisha ripoti ya wafanyakazi hao katika vyombo husika kwa kufuata mtiririko wa utendaji ndani ya serikali.


  "Kuna mambo mengine yanahusu watu, na wao wana haki zao, siwezi kufanya kila kitu na vyombo vya habari," alisema na kuongeza:


  "Lakini, tumepeleka ripoti katika vyombo husika kwa kuzingatia mtiririko wa mambo yanavyopaswa kuwa."


  Profesa Ndulu aliongeza kwamba, iwapo BoT itakuwa ikifanya kazi kwa kueleza kila kitu hadharani watumishi wanaoachishwa au kuchukuliwa hatua nyingine wanaweza kushitaki.


  Alipoulizwa zaidi kwamba, BoT ni taasisi nyeti ya umma ambayo Watanzania wanaifuatilia kwa makini baada ya kukumbwa na tuhuma hizo za ufisadi, sasa iweje, mabadiliko kama hayo umma usijue, alijibu: "Siyo kwamba tunaficha taarifa, isipokuwa ni taratibu na kulinda haki za kila mfanyakazi kama raia na binadamu."
   
 10. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #10
  Feb 23, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mimi hizi naona kasi za sakafuni haziishi kuzimika.JK alianza na haya mata hivi mara vile leo anakimbia hata maamuzi yake na kujijitea kwamba hakumfukuza Lowasa ila maamuzi cha CC.So mimi sioni jipya . Majina nayo yako wapi ya walio panguliwa na kupigwa chini ?Saabu ni hizi hizi za kashfa ama ?
   
 11. i

  ilboru1995 JF-Expert Member

  #11
  Feb 24, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,331
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Kama kawaida JF mambo hadharani, waliotimuliwa BoT ni hawa hapa:
  1.Imani David Mwakosya
  2.Esta Mary Komu
  3.Isaack Hubert Kilato
  4.Bosco Ndimbo Kimela
  5.Elisa Peter Issangya
   
 12. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #12
  Feb 24, 2008
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Weka Job Title zao Mkuu!!!
   
 13. K

  Kizito Member

  #13
  Feb 24, 2008
  Joined: Feb 23, 2008
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa Tabia ya watanzania ilivyo hawa jamaa waliosimamishwa kazi watarudi tu maana haki na sheria ni tofauti sana (sheria inataka asimame na haki itamtaka arudi kazini) kama watu hawa wamesimamishwa kwa kesi ya EPA au ya RICHMOND wafukuzwe kama ni kesi tofauti na hiyo basi waendelee kusimama, vinginevyo tutumie hoja ya mhesh.Ndesambulo ambae anasema watu kama hawa China wananyongwa maana china hawataki michezo ya ajabuajabu kama hii ya ufisadiufisadi.
   
 14. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #14
  Feb 24, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Kizito you have saidi it all . Hapa sasa nashindwa kujua .Je wametimliwa kazi ama wamesimamisha kazi ? Maana mkanganyo huu .
   
 15. mashoo

  mashoo Member

  #15
  Feb 25, 2008
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kutimuliwa isiwe mwisho, lazima wawajibishwe; wafunguliwe kesi warudishe walichoiba na jela waende. Na wote wengine wafuate mkumbo huuhuu tukianzia na Balali, Lowassa, Karamagi etc. tuache "kulambwa kisogo" eti wamejiuzulu mara wamesimamishwa then giiiiiii hakuna linaloendelea,,,, wanazidi kupeta tu na pesa za wazalendo, is not fair!!!Inauma sana how the country is robbed kwa kasi ya ajabu!!!!kuna kilichobaki kweli??? I doubt.
   
 16. M

  Mugo"The Great" JF-Expert Member

  #16
  Feb 25, 2008
  Joined: Oct 7, 2007
  Messages: 263
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hivi hawa sio vidagaa kweli? Muungwana anachezea maisha ya walalahoi kwa ulaghai kuwa anachukua hatua huku akiendelea kuwapamba mafisadi. Ipo Siku.
   
 17. Nyangumi

  Nyangumi JF-Expert Member

  #17
  Feb 25, 2008
  Joined: Jan 4, 2007
  Messages: 508
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo ni kuwa Watanzania tumeshajionyesha kuwa tuko very cheap.They can buy us like a cup of coffee. That is why we are treated cheaply.Tunafanyiwa kidogo tunapiga makofi,lakini naamini tutakapojua thamani yetu na nini tunahitaji kukipata toka kwa watu tunaowachagua(ila sio wanaotununua)then naamini hawatatufanyia mambo nusu nusu.
   
 18. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #18
  Feb 25, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Hapa hakuna tulichoambiwa maana bado hatujui hawa watu wana nyadhifa gani na wanahusika vipi na hizo tuhuma za ufisadi.
   
 19. Shukurani

  Shukurani JF-Expert Member

  #19
  Feb 25, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 253
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kusimamishwa kazi sio hoja,hatua gani zinachukuliwa zaidi dhidi ya watu hawa. Hawa wamelitia taifa hasara kubwa na tunaimani mpaka wamesimamishwa kuna uchunguzi ambao tayari umefanyika na ndiyo maana hatua hiyo imefikiwa. Sioni sababu kwanini mpaka leo hatuwaoni mahakamani,maana hapa ukawihi kusikia kulitokea techniqual problems wakati wa maamuzi na mtu akarudishwa kazini
   
 20. Shukurani

  Shukurani JF-Expert Member

  #20
  Feb 25, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 253
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kusimamishwa kazi sio hoja,hatua gani zinachukuliwa zaidi dhidi ya watu hawa. Hawa wamelitia taifa hasara kubwa na tunaimani mpaka wamesimamishwa kuna uchunguzi ambao tayari umefanyika na ndiyo maana hatua hiyo imefikiwa. Sioni sababu kwanini mpaka leo hatuwaoni mahakamani,maana hapa ukawihi kusikia kulitokea techniqual problems wakati wa maamuzi na mtu akarudishwa kazini
   
Loading...