Sioni wivu wala sina haja ya kuajiriwa huko. Nimeshangazwa na mawazo yako uliyotoa eti ''hata kama tungekuwa sisi tungefanya hivyo hivyo''. Mawazo yako yanapotosha na ni ya enzi za mawe. Huwezi kuhalalisha ''uki-gogonization'' eti kwa vile hata sisi tungefanya hivyo. Mazee nakuapia hata mwenyekiti wa kijiji chetu ambae hajasoma hawezi kutoa mawazo kama hayo. Yaani tuache wakuu wa idara za serikali wafanya wanavyotaka kwa kuwa eti hata kama tungekuwa sisi tungefanya hivyo?? La haula .... nimelewa bila kunywa kilevi. Na mtu mwenye mawazo kama haya unaweza kuta amemaliza chuo kikukuu!!!!!Kwa hiyo ulitaka nani aajiliwe? Kama vipi soma kozi zinazohusiana na mambo ya BOT ili ukaombe ajira huko kama unaona wivu kwa kuajiriwakwa watoto wa vigogo huko.
Mkumbuke prof. Sarungi aliacha udakitari akawa mwanasiasa
Hakuna mtu aliyesema ukiwa mtoto wa kigogo huna haki ya kuajiriwa BOT. Hiyo ni conclusion yako uliyofikia na inaonekana huelewi watu wanahoji nini). Sisi tunashangazwa na ''coincedence'' ya watoto 14 wote wa vigogo kuajiriwa sehemu moja (nyeti na yenye malipo nzuri). Mbona hatuioni ''coincidence'' hii ikitokea sehemu nyingine...!!!!!!!hivi ukiwa mtoto wa kigogo ndiyo huna haki ya kuajiriwa BKT??? Tufanye utafiti kwanza...tujue taasisi inawaajiriwa wangapi??? kati yao watoto wa "vigogo" ni wangapi??.....walipata ajira kihalali??na tujue pia "kigogo" ni nani?? sio tuna kuja na mada za kulalamika tu....tukiwatunalalamika tu mwishowe tutazoea kulalamika...
Umeguswa nini Mkuu? Anyway ishu ni hapo kwenye red! Hao vijana wa wakubwa ukifuatilia hata academic records history wengi ni vilaza maana tumesoma nao na wengine tunawajua vichwani ni 'empty heard'. Mtu anapata Division IV Form six lakini kwa vile Baba yake anapesa anamrusha nje kusoma digrii. Within five years laiter unashangaa yumo ndani ya 'Twin Towers'.
Ona nchi yetu ilivyo
FILBART SUMAYE, PAMELA LOWASA, ZARIA KAWAWA,HERIETH LUMBANGA, SALAMA MWINYI,RECHAL MUGANDA, SALMA MAHITA,JUSTINA MUNGAI, KENETH NCHIMBI, BLASIA W. MKAPA, VAOLETH LUHANJO, LIKU KATE KAMBA, THOMAS MONGELA NA JABIRI KIGODA.
HIYO NI TIMU YA WATOTO WA VIGOGO WALIOAJIRIWA BOT BADO KATIKA BALOZI ZETU NJE YA NCHI.NCHI YETU INAFISADIWA NANI WA KUTUOKOA WENGI WAO WAMEGHUSHI ELIMU ZAO
HII MESEJI IMEZAGAA MITAANI KWA SANA SASA SIJUI KWAMBA NI KUJIVUNIA VIONGOZI WETU KUTUONYESHA KUWA ELIMU NI MSINGI WA MAISHA KWA KUWAPA WATOTO WAO ELIMU BORA AU
NI WANANCHI KUONA HUKO NI KUPENDELEANA KATIKA AJIRA ZENYE MASLAHI MAZURI AU
NI WIVU WA WATANZANIA TU?
Samahani kwa kuchakachua uzi
hivi Jabir Kigoda yupo B.O.T bado?
Hawajampiga chini?
ukweli hata iweje wewe umesoma shule za walimu 2 kingereza cha kubahatisha, leo hii ukafanye competition na watoto hawa watakushinda maana wao hawajasoma shule hizi za walimu njaa na wachache wenye uhaba wa vyoo, vitabu, hata nyumba za kuishi. mwalimu akiamka anawaza familia yake watakula nini lakini hawa wezetu wamesoma shule nzuri pengine nje ya nchi kwa system zote za shule
Ona nchi yetu ilivyo
FILBART SUMAYE, PAMELA LOWASA, ZARIA KAWAWA,HERIETH LUMBANGA, SALAMA MWINYI,RECHAL MUGANDA, SALMA MAHITA,JUSTINA MUNGAI, KENETH NCHIMBI, BLASIA W. MKAPA, VAOLETH LUHANJO, LIKU KATE KAMBA, THOMAS MONGELA NA JABIRI KIGODA.
HIYO NI TIMU YA WATOTO WA VIGOGO WALIOAJIRIWA BOT BADO KATIKA BALOZI ZETU NJE YA NCHI.NCHI YETU INAFISADIWA NANI WA KUTUOKOA WENGI WAO WAMEGHUSHI ELIMU ZAO
HII MESEJI IMEZAGAA MITAANI KWA SANA SASA SIJUI KWAMBA NI KUJIVUNIA VIONGOZI WETU KUTUONYESHA KUWA ELIMU NI MSINGI WA MAISHA KWA KUWAPA WATOTO WAO ELIMU BORA AU
NI WANANCHI KUONA HUKO NI KUPENDELEANA KATIKA AJIRA ZENYE MASLAHI MAZURI AU
NI WIVU WA WATANZANIA TU?
Mkuu, inawezekana na wala hakuna muujiza. Usikate tamaa. BoT na TRA ni moja ya Taasisi zinazosemekana kuwanyima fursa watanzania wa kawaida na kuajiri watoto wa vigogo. Hili si kweli, na kama wapo ni asilimia chache tu. Lakini pia tusisahau hata watoto wa vigogo wamesoma, na kama wana sifa zinazotakiwa kwanini wasiajiriwe? Mbona mimi ni mtoto wa mlalahoi asiyejulikana lakini nimebahatika kufanya kazi kwenye Taasisi zote hizi? Haya ni majungu tu. Kwani hao aliowataja ni asilimia ngapi ya wafanyakazi wote wa BoT?
Tangu nikiwa mdogo nimekuwa na ndoto kuja kuwa mfanyakazi wa BOT sikati tamaa! Najua iko siku milango ya watoto wa wakesha hoi itakuwa wazi japo hata kwa kumuokotea gavana kalamu zikidondoka!inshaallah
Tuambie mkuu mara ya mwisho kabisa kufanya kazi kwenye taasisi hizo ilikuwa ni lini?
Lingekuwa ni jambo la busara endapo ungeletwa uchambuzi wa sifa zao hawa wenzetu kiasi cha kuweza kuajiriwa hapo BOT na sio vijana wengine wenye sifa pengine kama za kwao ambao hawakuweza kuajiriwa mahala hapo.
Kwa mfano Filbert Sumaye ionyeshwe kabla ya kwenda UK kusomea Degree yake ya computer science alisoma wapi kabla ya hapo hadi kuwa na sifa za kwenda UK university na kulipa maelfu ya paundi za uingereza, ana baada ya hapo awe na uhakika kwamba akirudi Tanzania anaingia BOT moja kwa moja bila kuchakarika kidogo.
Kwahio anaefahamu au mwenye details za uhakika huu ndio wakati wa kusema.
Pia BOT walitumia utaratibu gani wa kufanya usaili kiasi kwamba watoto 14 wa viongozi mbalimbali wa serikali ya CCM wamepata nafasi za kazi katika idara hiyo nyeti, huku vijana wengine wakitupwa nje.