Watoto wa vigogo na ajira BoT

Watoto wa vigogo na ajira BoT

Hapo kwenye blue! Mtoi unapenda kazi za kuinama mara kwa mara??

Moyo ulio jaa maovu huwaza maovu, sehemu pekee ya kupumzika moyo huyo ni motoni. Kama kweli mtu anaongea aliyo yajaza kifuani basi kifua chako kimebeba gunia la makaa ya moto. Nia yangu kwenye kauli yangu ni njema, itabaki hivyo hivyo bila kujali mawazo yako yanayo waza maaswi!

Kila jema na lenye kheri lisikuponyoke mkuu.
 
Mnatuonea wivu Jamani,

Nafanya kazi UN Newyork na my mother ametumikia serikali na msomi. Amekuwa Katibu mkuu for years na sasa ana cheo kingine (msije mkaniattach nikisema cheo chake) hata usingizi alikuwa hapati. Mshahara mdogo kuliko alipokuwa UN na world Bank.

Watanzania tuache wivu
 
Hapa mkombozi ni vita ya wenyewe kwa wenyewe na sio M4C wala M4D.....Hapa kitu kisanuke then tuanze moja kama congo na somalia huenda wapuuzi flan watajua kua kuna binadamu wengine pia...
MIE NIPO TAYARI KUJITOA MUHANGA KAMA HALI NDO IPO HIVI
Uzuri au ubaya wa vita ya wenyewe kwa wenyewe ni kwamba hao wanaobebwa hawata dhurika hata kidogo kwani watakuwa wakwanza kupanda ndege! nyie mnaopiga makelele na kuombea vita ndio mtakao chinjana mwanzo mwisho!
 
Tangu nikiwa mdogo nimekuwa na ndoto kuja kuwa mfanyakazi wa BOT sikati tamaa! Najua iko siku milango ya watoto wa wakesha hoi itakuwa wazi japo hata kwa kumuokotea gavana kalamu zikidondoka!inshaallah

kuna Mtoi mmoja alikuwa ikulu.....kwa jina lako utakuja kupata......vuta subira....uongeze orodha ya watoto wa vigogo.....
 
Ujumbe kama huu jana nilitumiwa kwa njia ya sms na ukanishangaza sana kwa ufinyu wa akili wa wabongo. Ni nani asiyetaka kuacha wanawe wakiwa katika mazingira mazuri? mkimaliza kuuliza juu ya hao vigogo fuatilieni na vigogo wngine ili mjipunguzie siku za kuihi kwa kukaa munaongelea maisha ya wengine.

Haya sasa hawa ndio wanaitwa wasomi wa Tanzania....wanatoa mawazo mgando afadhali mkulima ambae hajaenda shule.... tutafika??
 
Hii kitu mliitembeza sana kwenye msg kupitia simu za mkononi naona leo kwa kuwa hakuna la maana hapa jukwaani mmeamua kujifurahisha kidogo na old stories.
 
Tupige moyo konde bila kukata tamaa, hatima ya nchi ni mikononi mwetu wapigania haki.

hivi ukiwa mtoto wa kigogo ndiyo huna haki ya kuajiriwa BKT??? Tufanye utafiti kwanza...tujue taasisi inawaajiriwa wangapi??? kati yao watoto wa "vigogo" ni wangapi??.....walipata ajira kihalali??na tujue pia "kigogo" ni nani?? sio tuna kuja na mada za kulalamika tu....tukiwatunalalamika tu mwishowe tutazoea kulalamika...
 
ukweli hata iweje wewe umesoma shule za walimu 2 kingereza cha kubahatisha, leo hii ukafanye competition na watoto hawa watakushinda maana wao hawajasoma shule hizi za walimu njaa na wachache wenye uhaba wa vyoo, vitabu, hata nyumba za kuishi. mwalimu akiamka anawaza familia yake watakula nini lakini hawa wezetu wamesoma shule nzuri pengine nje ya nchi kwa system zote za shule
 
kuna Mtoi mmoja alikuwa ikulu.....kwa jina lako utakuja kupata......vuta subira....uongeze orodha ya watoto wa vigogo.....

Mkuu sijawahi kuwa na ndugu aliye wahi kushika nafasi nyeti serikalini wala mahali popote! Mimi ni one man army ninaye tegemea kujitoa mwenyewe maana sina wa kunishika mkono. Hata vidato nimevipita kwa wakesha hoi (wazazi) kukopanya sana huku na kule. Mungu hamtupi mja wake, kama sifa moja wapo ni kuwa na GPA nzuri tayari ninayo. Nangoja zitangazwe na mimi nikapigane vikumbo na watoto wasio jua taa za chemli na vibatari.
 
haya matatizo yana anzia kwenye mitihani yetu ya taifa mpaka vyuoni utakuta baadhi ya maLecture wanashughulika sana na hawa watoto wa wakubwa pengine hata wizi wa mitihani wanatumiwa sms au hata ujumbe ili wasiwapatie matokeo ya chini au hata kuwakamata na hii nilishaiona SUA wala sio kitu cha kubahatisha
 
Naomba nikusahihishe sio watoto wa wakubwa ni watoto viongozi wa CCM na Serikali yake. Wakubwa tunawajua bwana hao wamechutama kwenye title zao za kifisadi
 
1. FILBART SUMAYE,
2. PAMELA LOWASA,
3. ZARIA KAWAWA,
4. HERIETH LUMBANGA,
5. SALAMA MWINYI,
6. RECHAL MUGANDA,
7. SALMA MAHITA,
8. JUSTINA MUNGAI,
9. KENETH NCHIMBI,
10. BLASIA W. MKAPA,
11. VAOLETH LUHANJO,
12. LIKU KATE KAMBA,
13. THOMAS MONGELA na
14. JABIRI KIGODA.

Naona First eleven ya BoT imekamilika na ina reserve wakutosha.
 
Kawaida sana mi naona mfumo unawabeba, wao hata wasiajiliwe wanapewa mikopo mikubwa.
 
Hivi ukiwa mtoto wa kigogo ndiyo huna haki ya kuajiriwa BKT? Tufanye utafiti kwanza. Tujue taasisi inawaajiriwa wangapi? Kati yao watoto wa "vigogo" ni wangapi? Walipata ajira kihalali? Na tujue pia "kigogo" ni nani? Sio tuna kuja na mada za kulalamika tu.Tukiwatunalalamika tu mwishowe tutazoea kulalamika.

Umeguswa nini Mkuu? Anyway ishu ni hapo kwenye red! Hao vijana wa wakubwa ukifuatilia hata academic records history wengi ni vilaza maana tumesoma nao na wengine tunawajua vichwani ni 'empty heard'. Mtu anapata Division IV Form six lakini kwa vile Baba yake anapesa anamrusha nje kusoma digrii. Within five years laiter unashangaa yumo ndani ya 'Twin Towers'.
 
Haya sasa hawa ndio wanaitwa wasomi wa Tanzania....wanatoa mawazo mgando afadhali mkulima ambae hajaenda shule.... tutafika??

Kwa hiyo ulitaka nani aajiliwe? Kama vipi soma kozi zinazohusiana na mambo ya BOT ili ukaombe ajira huko kama unaona wivu kwa kuajiriwakwa watoto wa vigogo huko.
 
Nami nategemea siku moja nitapata ajira BoT pasipo na shaka!!nitapata kazi pale!!!
 
Back
Top Bottom