Watoto wa vigogo na ajira BoT

Watoto wa vigogo na ajira BoT

huyo kigoda jina lake la kwanza ni nani nimscan na antivirus yng
 
Kuna mtoto mmoja wa nkya.. Amekula degree yake university of alabama clemson tide.. Sasa wewe utoke na degree yako ya vyuo vya kata sijui udsm,mzumbe, udom utashindana nae vipi... Hata mimi kama mwajiri lazima reputation ya shule ihusike..

Watoto wa kishua wanakamata vitengo sababu wamesoma kwenye world class schools,,, na ujanja wanaotumia vigogo wakiona mtoto wake wasiwasi wanampeleka kwenye best centres ili awazidi vichwa wa shule za kata as udsm, mzumbe etc.. Sio bot tu had kwenye private sector wapo kibao sehem nyeti as vyuo walivyosoma vinawabeba
 
Kwanza watanzania wanachosha na ni mzigo mkubwa kumbeba Mtanzania,
Izihaka na uchunguzi wake usiokamilika kakurupuka sijui kautoa wapi
kaja kuropoka humu kwa kudhani kila mtu yuko standbye kusikiliza umbea,

mi sio mtoto wa kigogo lakini naamini juhudi zangu zinaweza kunifanya nikawa kigogo na watoto wangu pia wakaja kuwa watoto wa kigogo vilevile, sasa wewe kaa tu unalalamikia watoto wa vigogo kuwa na hiki au kile badala na wewe utafute kuwa hivyo mwisho utaishia kwenye umasikini na malalamiko..

watoto wa vigogo kuwa na nafasi serikalini ni haki yao kama wanauweza utendaji kuliko wewe uliyekalia maneno tuu vitendo huna
na ulifikiri wasome hivyo halafu wakafanye kazi wapi?
fikiria wewe ndo ungekua mtoto wa kigogo ungekataa kufanya kazi BOT?? Ungeranda randa mtaani kwa kuogopa watu wasione wewe mtoto wa kigogo unafanya kazi seriakalini au BOT???!!


JIPANGEE!!!
 
Kuajiri mmeajiri wenywe na kuchunguza mjichunguze wenyewe! Je kuna gharama zinazohusiana na kujichunguza? Acheni hizo hakuna chochote.
 
sawa mimi nimesoma hizo ulizoiita shule ya maana
na ya maana kweli si kitoto mwezi wa kwanza TRA walitoa nafasi za kazi nikaomba katika kufatilia sana nikakutana na hili ili uingie kazini hapo unatakiwa uhonge 3,000,000
sasa kama mimi mtoto wa mamantilie nitazitolea wapi hizo pesa?
Zaidi ya watoto wa vigogo kujazana huko loo
sasa hapo shule ya maana imenisaidia nini?

sie tunabanana huku kwa wasaka nyoka na bachelor za maana kutoka vyuo vya maana kwenye mishahara ya laki mbili na nusu, huku hukuti ujinga eti mtoto wa kigogo
 
Mtawala wa forum hii na wote kwa ujumla napenda kuwapa mada hii iwe kama ni ushahidi mojawapo wa sakata la BoT. Hili swala la watoto wa vigogo kuajiriwa Bot si la uongo kwani

1. Rogers Sumaye alipata ajira hata kabla hajamaliza shule Uk kwani kuna watu walianza kufanya interview za kumsindikiza.
2. Kigoda naye the same
3. Lowasa's the same
4. And many others who have brothers there or relatives

Ishu hapa sio kuwa na sifa za kufanya kazi Bot bali je walipitia usahili na taratibu za ajira serikalini?

Je ni watu wangapi wenye sifa walifanya interview na kushinda na bado wakapigwa chini?

Inasikitisha kuona kuwa hata Gavana mpya anatetea maovu akiwa ofisini hata mwezi haujaisha ni SHIDA hii

=======
Baadae: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/19573-watoto-wa-vigogo-bot-wasafishwa.html

hebu tu argue kama watu weunye upeo mkubwa wa kufikiri, sikubaliani na jinsi hawa wakubwa wanavyo wapachika watoto wao BOT kama vile opotunity sehemu nyingine zimeisha

nadhani hawa wakubwa uwezo wao wa kufikiri unaishia hapo BOT na hao watoto wao hawawezi kusavive nje ya BOT. ni ujinga tu, na niwaambie tu kwamba hiyo ni fahari ya muda mfupi sio kitu endelevu, means out of BOT no life

sasa sisi ambao hatukutokea kwenye familia za wakubwa kwa kuwa hatuwezi kuajiliwa BOT na tumesoma shule vizuri hii iwe ni changamoto nkwetu

tupanue uwezo wa kufikiri nje ya ajira za upendeleo! tuibue na kubuni biashara, miradi, ajira,kwa kutumia akili na elimu tuliyopata ili tuwaonyeshe hawa wanaokariri kuwamba silazima ufanya kazi BOT ndo uwa na Maisha bora

watu wanadhani kukaa Dar na kufanya kazi BOT ndo kila kitu,think out of the box! je ushawahi kufikiria kwenda Tabora kufuga nyuki kurina asali na kusambaza ni ajira babkubwa kuliko BOT???

au kwenda kilombelo kulima miwa. Arusha kulima NGano ni great oppotunuty na inaweza kukulipa kuliko kukaa kwenye kiyoyozi BOT.

nafikiri tusiwalaumu tuwasikitikie kwa ujinga wanaishi na kufikiri in artificial life

na kutokuona mbali, there are many oppotunities out of BOT
 
Mkuu sijawahi kuwa na ndugu aliye wahi kushika nafasi nyeti serikalini wala mahali popote! Mimi ni one man army ninaye tegemea kujitoa mwenyewe maana sina wa kunishika mkono. Hata vidato nimevipita kwa wakesha hoi (wazazi) kukopanya sana huku na kule. Mungu hamtupi mja wake, kama sifa moja wapo ni kuwa na GPA nzuri tayari ninayo. Nangoja zitangazwe na mimi nikapigane vikumbo na watoto wasio jua taa za chemli na vibatari.
Umesema wazazi wako walikupigania sana... hili linaondoa sifa za one man army... wewe tuma maombi yako kisha waambie una undugu na yule Mtoi wa ikulu... nadhani utapata kwa sifa ya jina lako
... ha ha ha ha
 
Gazeti la Jamuhuri la October 23, 2012 Limewataja vijana wafuatao kuwa ni watoto wa vigogo waliojazana BOT: Kweli Tanzania ina wenyewe


Salama Ali Hassan Mwinyi
Filbert Tluway Sumaye
Zaria Rashid Kawawa
Blasia William Mkapa
Herriet Marten Lumbanga
Pamela Edward Lowassa
Rachel Muganda
Salma Omary Mahita
Justine Mungai
Kenneth Nchimbi
Violet Philemon Luhanjo
Liku Kate Kamba
Thomas Mongela
Jabir Abdallah Kigoda
 
Gazeti la Jamuhuri la October 23, 2012 Limewataja vijana wafuatao kuwa ni watoto wa vigogo waliojazana BOT: Kweli Tanzania ina wenyewe


Salama Ali Hassan Mwinyi
Filbert Tluway Sumaye
Zaria Rashid Kawawa
Blasia William Mkapa
Herriet Marten Lumbanga
Pamela Edward Lowassa
Rachel Muganda
Salma Omary Mahita
Justine Mungai
Kenneth Nchimbi
Violet Philemon Luhanjo
Liku Kate Kamba
Thomas Mongela
Jabir Abdallah Kigoda
Ulitaka waende kufanya kazi wapi
 
Gazeti la Jamuhuri la October 23, 2012 Limewataja vijana wafuatao kuwa ni watoto wa vigogo waliojazana BOT: Kweli Tanzania ina wenyewe


Salama Ali Hassan Mwinyi
Filbert Tluway Sumaye
Zaria Rashid Kawawa
Blasia William Mkapa
Herriet Marten Lumbanga
Pamela Edward Lowassa
Rachel Muganda
Salma Omary Mahita
Justine Mungai
Kenneth Nchimbi
Violet Philemon Luhanjo
Liku Kate Kamba
Thomas Mongela
Jabir Abdallah Kigoda

Wapo kumi na nne tu??? basi vigogo wa nchi hii wazembe sana
 
Gazeti la Jamuhuri la October 23, 2012 Limewataja vijana wafuatao kuwa ni watoto wa vigogo waliojazana BOT: Kweli Tanzania ina wenyewe


Salama Ali Hassan Mwinyi
Filbert Tluway Sumaye
Zaria Rashid Kawawa
Blasia William Mkapa
Herriet Marten Lumbanga
Pamela Edward Lowassa
Rachel Muganda
Salma Omary Mahita
Justine Mungai
Kenneth Nchimbi
Violet Philemon Luhanjo
Liku Kate Kamba
Thomas Mongela
Jabir Abdallah Kigoda

Aaah, ndugu yangu waache wale kwani kila kitu na wakati wake. Ipo siku nao watakuwa wanayachungulia majengo hayo kama kituo cha polisi.
 
Hivi watoto wa walalahoi hawana bongo? Kweli aliye nacho ataongezewa na asiye nacho hata kidogo alichonacho atanyang'anywa.
 
Hivi watoto wa walalahoi hawana bongo? Kweli aliye nacho ataongezewa na asiye nacho hata kidogo alichonacho atanyang'anywa.

Sehemu zote muhimu basi utaona watu wanajiriwa kwa memo tu, hamna cha interview wala competence! inawezekana
hao wote wamesomea banking au financial management au whatever, lakini hapo sidhani kama ulipita mchujo na hao
wote wakawa ndio cream!!!!
 
Tanzania itajengwa na wenye moyo،italiwa ma wenye meno. Wanadhani Nchi ni ya Kifame! Ipo siku watatoa maelezo kama watoto wao ndiyo pekee wenye akili.
 
Back
Top Bottom