Watoto wa kiume ni wagumu kuwasadia wazazi wao kuliko watoto wa kike

Hyrax

JF-Expert Member
May 20, 2023
604
1,534
Hili jambo nimelifuatilia muda mrefu sana hapa barani africa esp. Tanzania wazazi wanaenjoy tu pale ambapo mama akipata toto la kiume jamii inakuchukulia mtu wa thamani sana yaani hongera unapata nyingi lakini kadri toto hilo la kiume linavyozidi kuwa kubwa ndivyo linavyoanza kuwa jitu la hovyo hata kusahau wazazi wake.

Tofauti sana na mitoto ya kike huwa yanakumbuka sana wazazi wao kwa kuwatunza na kuwa karibu nao zaidi sijaingia ndani zaidi kujua shida nini kati ya jinsi hizi mbili ila kwa hali inavyoendelea naona bora kuzaa toto la kike tu haya matoto ya kiume mengi ni hasara yakishafika ukubwani yanazingua wazazi wao kinoma hasa yakishaoa au yakianza tabia ya kuchovyachovya na kulewa.
 
Attachments

  • Mbosso ft Chley - Sele.mp3
    4.1 MB
Unajua kwann? Kwasababu mtoto wakiume huwa na majukumu mengi, hasa wale walio oa tofaut na mtoto wa kike anategemea zaid mume wake, nazan umeelewa
Hii kitu watu wengi hawaioni.

Mtoto wa kiume akishaoa, hapo ujue ana familia yake, ana familia ya wakwe, na ana wazazi wake waliomzaa. Wote hao wanamtegemea! We unategemea huyo mtu atajigawaje? Alishe familia yake, alipie gharama zote za maisha, ajenge, asomeshe, nk. Wakati mtoto wa kike yeye akiolewa hata kama ana kazi gharama zote anamuachia mumewe, yeye hela yake inabaki kwa matumizi yake binafsi tu. Sasa atashindwaje kusaidia wazazi wake? Wanaume hebu mtupumzishe tunapambana na mengi msitulaumu..!
 
Sahihi kabisa.
 
Hawa wanawake hawaelewi. Wanawake hawana gharama. Kula, kulala, matibabu, nguo na matumizi mengine mwanaume ndiyo anagharamika.
Hapo una watoto watatu, wanahitaji kula, matibabu, mavazi, sehemu ya kulala nk hapo weka mwanamke.
Utajigawaje?
Mod. Jibu lishapatikana.
Futeni uzi
 
watoto wa kiume tatizo sana sisi inahudhunisha sana
Ungekuwa mwanaume ungeelewa ila kwa vile ni mtoto wa kike hauelewi.
Hapo kwenda kwa mpenzi wako, unaomba nauli akutumie, akiugua akupe hela ya matibabu, tena huwa mnalalamika hatuwahudumii. Ukipata mimba, unaomba hela ya kwenda klinik, siku ya kujifungua unaomba hela, kula, kuvaa n.k vyote hivyo unaomba hela kwa mwanaume ili hali na ww una kazi. Mwanaume huyo huyo ajenge nyumba, alipe ada n.k halafu ww hata kusaidia huwezi.
Wewe pesa yako haina kazi ndiyo maana ni rahisi sana kumpa mzazi.
"Ukitoa ngono, mwanamke hana cha kukupa"
 
Hatuwasaidi wazazi kwasababu wao tulipokuwa wadogo poketi mane walikuwa wanapewa dada zetu, kwaiyo dada zetu ndio wanarudisha ela walizokuwa wanapewa
 
Watoto wa kike sio risk takers,mtoto wa kike hata akizaa mtoto basi jina la mtoto litaitwa kwa nasibu ya baba na sio mama yaani kuonesha mwanamke jukumu la kulea anakaa kando.

Wanaume tuna option mbili tu ili tuwasaidie wazee.

1.tutafute sana hela na tuzipate kisha uwe na uwezo wa kuhudumia wazazi na familia yako.

2.jinyime na familia ili uwahudumie wazazi vizuri.

Mimi ninahisi mzazi anapoona mtoto anataka kuoa alafu mzazi anaona kabisa kwamba mwanangu hajanitoa magenotni vya kutosha,ama hajanisaidia vya kutisha basi mzazi suala la kuoa analikubali shingo upande.

Kwa ambao hamjaoa jitahidini kabla ya kuoa muwapush wazazi kama uwezo upo,sio unaoa huku mzazi kula yake kwa siku ni ya tabu,unaharakia nini kuoa ?

Kama kijana jipe jukumu la kuwatoa wazazi kwanza kabla ya kuoa then kuoa kuje baadae,sio unaoaoa ovyo tu huku wazazi wakishinda njaa.

Binafsi najiskia tabu sana kuona kijana anashindwa kuwasaidia wazazi kisa tu ana majukumu ya kifamilia,kwani hii familia yako imewakuta wwzazi ama wazazi ndo wameikuta familia yako ?

Wakeup wanaume.
 
Binafsi najiskia tabu sana kuona kijana anashindwa kuwasaidia wazazi kisa tu ana majukumu ya kifamilia,kwani hii familia yako imewakuta wwzazi ama wazazi ndo wameikuta familia yako ?

Wakeup wanaume.
Mbona ukiwa mtu mzima wazazi wenyewe ndio wanakutimua ukaanzishe familia yako? Tena wakiona unachelewa wanaanza maneno ya shombo na kejeli.

Ina maana kijana unatakiwa uwalee wazazi mpaka wafe ndio wewe uoe?
 
Kumbe ndo maana furaha hainiishi kila ninapowaona mabinti zangu wawili.......watoto pekee nilionao
 
Mbona ukiwa mtu mzima wazazi wenyewe ndio wanakutimua ukaanzishe familia yako? Tena wakiona unachelewa wanaanza maneno ya shombo na kejeli.

Ina maana kijana unatakiwa uwalee wazazi mpaka wafe ndio wewe uoe?
KAma wazazi wako wamekufukuza maana yake hawawezi kukuhudumia,so unatakiwa uwaze kwamba kama hawawezi kukuhudumia maana yake inatakiwa uwasaidie.

Lakini pia kama wamekufukuza kwa roho mbaya zao,unatakiwa ujiulize kwa nini hawakukufukuza wakati unanyonya ? Ni kwa sababu wakati huo usingeweza kujitegemea.

So usijekuleta propaganda yoyote ili ujitoe kwenye ustaarabu wa kuwasaidia wazazi pale unapopata uwezo,kuwasaidia wazazi ni jambo la mtoto.

UNadhani nani atamsaidia mzazi anapokwama ?
Haya mambo ni kubadilishana,mzazi humkuza mtoto na mtoto amsaidie mzazi anaposhindwa.
Ina maana kijana unatakiwa uwalee wazazi mpaka wafe ndio wewe uoe?
huo ni ufahamu wako mkuu.

Lengo hapa nikuwainua wazazi kwanza then unaoa.

Unakuta wazazi kula shida mahitaji ni tatizo,kama kuna means yoyote ya kuwafanyia inatakiwa uifanye ili kula isiwe tatizo kwao na mahitaji madogomadogo then ndio unavuta jiko.

LEngo sio wazazi uwafanye wawe matajiri hapana lakini kuna ile kuwasapoti na kuhakikisha kwamba kula kwao hakuwapi shida,na mahitaji madogo madogo ya kila siku sio tatizo.

Lakini mtu anapapatua ndoa huku wazazi kula ni kwa mashaka,huu sio uungwana.
 
Back
Top Bottom