Watoto 981 katika Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, wamepatiwa ujauzito ndani ya kipindi cha miezi sita

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,279
Watoto 981 katika Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, wamepatiwa ujauzito ndani ya kipindi cha miezi sita kilichoanzia mwezi Januari mwaka huu.

Kutokana na kitendo hicho cha ukatili wa kijinsia, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mwanaidi Ali Khamis, ameagiza watuhumiwa watafutwe na kuchukuliwa hatua. Naibu Waziri huyo alibaini hilo akiwa katika ziara ya siku tano wilayani humo iliyomalizika jana, iliyolenga kukagua na kujionea utoaji wa huduma za ustawi wa jamii na masuala ya maendeleo ya jamii.

Katika ziara hiyo pia alizindua Kituo cha Huduma Jumuishi kwa waathirika wa vitendo vya ukatili wa Kijinsia (One Stop Centre) katika Hospitali ya Wilaya ya Kibondo kitakachowezesha walengwa kupata huduma kwa pamoja na kwa muda mfupi.

Alisema taarifa hizo haziwezi kufumbiwa macho, badala yake watendaji wanaohusika wafanye kila linalowezekana kuhakikisha watuhumiwa wanapatikana na haki inatendeka katika kipindi kifupi.

“Jamii haiwezi kutegemea miujiza ya mafanikio ya kizazi kijacho endapo itabaki kufumbia macho vitendo vya ukatili wa kijinsia hususani dhidi ya wanawake na watoto kwa kuangalia watoto wao wanapata mimba katika umri mdogo na kukatisha ndoto zao,” alisema.

Alisema Sheria ya Mtoto inataja mashauri yao kukamilika ndani ya kipindi cha miezi sita, lakini kwa mazingira ya huduma za mkono kwa mkono, kuna umuhimu wa kuyamaliza muda mfupi zaidi. Ofisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Sophia Gwamagobe, alipongeza juhudi za pamoja kati ya serikali na wadau wa maendeleo katika kutafuta mwarobaini wa matatizo ya vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

Alisema kituo hicho kilichofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Save the Children, kitawezesha upatikanaji wa huduma hizo kwa pamoja kwa waathirika ndani ya muda mfupi.

Alisema kituo hicho kinajumuisha ofisi za polisi, maofisa ustawi na daktari.

Mwakilishi wa Save the Children, Jackson Nsabo, alisema wameshajenga kituo cha mkono kwa mkono ili kukabiliana na wimbi la vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto.

Chanzo: IPP Media
 
Hawa kwa kuwa wako mbali ule ujumbe wa Magufuli wa kuzaa sana utakuwa ndio umefika sasa
 
Back
Top Bottom