Polisi: Wanawake 349 Iringa wafanyiwa ukatili wa kijinsia kwa kipindi cha Januari hadi Oktoba, 2023

Bull Bucka

Member
Oct 5, 2023
34
46
Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa kupitia Kamisheni ya Polisi Jamii na Dawati la Jinsia na watoto limeandaa shughuli mbalimbali ikiwa ni sehemu ya utelekezaji wa kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia yenye kauli mbiu isemyo "Wekeza kuzuia ukatili wa kijinsia".

Akizungumza na Askari wa kike mkoani hapa Kamanda wa Polisi Iringa, ACP Allan Bukumbi, amesema kwa kipindi cha Januari hadi Oktoba 2023 Wanawake 349 wamefanyiwa ukatili wa kijinsia wakati kwa upande wa Wanaume waliofanyiwa ukatili ni 49 kwa kipindi hicho.

Kamanda Bukumbi amesema takwimu zinaonyesha kuwepo kwa kiwango kikubwa cha matukio kwa wanawake na watoto hivyo Jeshi la Polisi linapambana kutokomeza vitendo hivyo vinavyosababishwa na uelewa mdogo, mila potofu, ulevi, imani za kishirikina pamoja na migogoro ya kifamilia.

Aidha, amewataka Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoani Iringa (TPF - Net Iringa) kuwa mfano mzuri kwenye jamii na kupambana na vitendo hivyo vya ukatili kwa wanawake na watoto pamoja na kuwa na umoja na ushirikiano.

Kwa upande wake Mkuu wa Dawati la jinsia na watoto Iringa, Mkaguzi wa Polisi Elizabeth Swai amesema kesi za ukatili wa kijinsia mara nyingi hutokea kwa watu wa karibu ambapo changamoto kubwa ni kwa wanandugu kutotoa ushirikiano kwa Polisi na kuanza usuluhishi baina yao jambo linalopelekea kurudisha nyuma jitihada za kupambana na ukatili wa kijinsia na kuitaka jamii kubadilika ili kutokomeza vitendo hivyo.

Nuru FM
 
Back
Top Bottom