Dkt. Samizi aadhimisha mitatu ya mama kwa kuzindua magati ya maji- Kibondo, wiki ya maji

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
Alhamisi 21 Machi, 2024

Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Dkt. Florence George Samizi amezindua Mradi wa Maji Safi na kisima Cha Maji katika eneo la Malagarasi na Gati la Maji Stendi ya Mabasi katika Uzinduzi wa Wiki ya Maji ambayo inaenda sambamba na Miaka Mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan hatua itakayosaidia kupunguza kero ya maji safi Kwa wakazi wa maeneo mbalimbali katika Jimbo la Muhambwe.

Aidha, mnamo Mwaka 2020/2021 mradi wa Maji (Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo) kutokana na ruzuku kutoka serikalini utoaji wa huduma ya Maji uliongezeka kutoka 37.12% hadi kufikia 67.64% ambayo imegharimu kiasi Cha Tsh. 2,910,545,367.73 (Bil. 2.9) katika kipindi cha 2022 - 2024. MIAKA MITATU YA RAIS DKT. SAMIA NA SAMIZI (Jimboni).

Baada ya Uzinduzi, Dkt. Florence Samizi amehutubia wananchi kuwashukuru Kwa kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi na Serikali inayoundwa na CCM na kumpongeza Rais Samia kwa kazi kubwa anayoifanya; kuhakikisha anatekeleza malengo ya KUMTUA NDOO MWANAMKE katika Jimbo la Muhambwe huku akimpongeza pia Waziri wa Maji, Jumaa Aweso pamoja na Eng Aidan na Eng Almas wa Kibondo kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maji.

IMG-20240322-WA0003.jpg



#MamaImara
#JimboSalama
 
Back
Top Bottom