Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,468
- 23,745
Jambo alilofanya Samia Suluhu la kumpumzisha Aliyekuwa DC wa Hai Bwana Sabaya linapaswa liwe jadi ya nchi na wananchi husika. Halipaswi liwe ni jambo kuu la kitaifa katika ulimwengu wa watu wastaarabu,wenye akili au uelewa.
Alikuwepo Makonda Dar es salaam.alifanya aliyoyafanya mpaka alipokuja kutokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dsm. Watu wakafurahi sana wakiamini kukwama kwao kiuchumi na mateso wanayoyapata ni kutokana na Makonda. Na sasa hayupo wamepata suluhisho.
Makonda yupo mtaani anaendelea na maisha yake,hajafirisika,hana tatizo hana tu cheo cha ukuu wa mkoa ambacho by the way hakuzaliwa nacho so hajapungukiwa kitu maishani. Ana utajiri wake na miradi yake inaendelea. Watanzania wamebaki maskini, wana shida,wananyaswa n.k ila wamefurahi makonda si mkuu wa mkoa.
Binafsi sikuwahi mpenda Makonda. Sababu ni nyingi tu. Lakini sikuwahi kuona yeye ndo chanzo cha kila kitu katika maisha yangu.
Tufikiri kidogo. Yale mabaya yote aliyoyafanya au daiwa kuyafanya makonda amewajibika kwayo?ameshtakiwa? Hapana. Ila watanzania wanafurahia tu kuwa makonda si mkuu wa mkoa wa dsm.wameridhika.
Sabaya kijana mjueri na fedhuli kwa kila namna. Naye ameondelewa kwenye nafasi yake. Watanzania wanashukuru na kusema ndiyo zawadi ya sikukuu. Mh Rais akapumzike tu hata mwaka.
Yaani matatizo yote ya watanzania yameisha kwa sabaya kuvuliwa cheo.na hapo Mh. Rais amefanya kazi kubwa sana ya kutukuka. Wamemaliza maisha yanaendelea.
Nani aliyeturoga sisi watanzania?ambao kwa kiasi kikubwa tunaendeshwa na ashki,mihemko na jazba? Je matatizo ya waliotuibia pesa,waliotutesa,waliotufisadi,waliotudhuru ni kuvuliwa tu vyeo?baada ya hapo maisha yanaendelea?
Nliwahi sema watanzania ukiwafahamu ni rahisi sana kuwaongoza. Hawana makuu.mambo madogo madogo sana huyafanya makuu. Ukicheza na hayo unawaongoza milele.
Watanzania wengi ukishika kitambaa chekundu ukataka kujua wao wanasemaje. Usitake rangi ya kitambaa kwanza.waulize "nyie mnaona hiki kitambaa ni rangi gani?" wakisema cheusi. Waambie "swadakta nmeshika kitambaa cheusi hii ni rangi iliyopo kwenye bendera ya Taifa" watakushangilia sana.
Watanzania hawa hawa ndo walikuwa wanashangilia wenzao wakidhalilishwa kwenye mikutano.na hawa wakijakutwa nayo wao wana ruka kimanga.
Watanzania mpaka sasa hawajui wanataka nini.hawajui inchi yao inaenda wapi,hawajui wao wanaendesha vipi nchi.
Sukari shida,mafuta ya kupikia shida,madeni ya mkoponwa Helsb yalipandishwa asilimia kinyume na utaratibu.watanzania hayo hawaoni ni shida.
Watanzania wanapenda vitu rahisi rahisi tu. Wanafurahia vitu rahisi rahisi tu. Hawapendi kuumiza kichwa,hawajui mustakabali wa nchi yao na maisha yao.
Miaka 5 itakatika. Hamna tulichofanya kama nchi. Ila tutafurahi na kuruka ruka. Itakuja tena mingine. Tutashtuka. Matajiri wanabaki kuwa (wenyenchi) ni wanasiasa na maskini ni (wananchi) raia.
Hawatauliza kodi zao miaka yote kwa nini zinatajirisha wanasiasa?mtanzania anayepokea tsh 250,000 anakatwa kodi mbunge anayepokea zaidi ya mil 5. Hakatwi kodi. Bado tunaamini tatizo letu kubwa ni Sabaya na aliyekuwa Makonda. Wanasiasa watazidi kunawiri na kutuua pale tunapohatarisha vyeo vyao. Sababu hatuna akili.