Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 15,290
- 9,720
Ndugu zangu Watanzania,
Ni ukweli ulio wazi kuwa ukitaka kumficha jambo mtanzania basi wewe weka jambo husika katika mfumo wa maandishi halafu kaa pembeni na utulie tu uone atakachokifanya. Ndio maana namuunga mkono Rais samia aliyesema watanzania wapewe Elimu ya katiba kwa miaka mitatu, japo mimi naona kwa watanzania hawa inapaswa iwe ni miaka minne ya elimu ya katiba ndio wataelewa vizuri.
Nimeshangazwa na watu kushangaa chama cha Mapinduzi kupitia mwenezi wake kutoa maelekezo kwa Waziri Mkuu kumaliza na kutatua changamoto za ardhi ndani ya miezi sita. Napenda kuwaambia kuwa chama ni kikubwa kuliko waziri mkuu na serikali yote kwa ujumla wake.chama kinaweza kuielekeza serikali kufanya jambo lolote lile na serikali inapaswa kutekeleza ndani ya muda husika na kurudisha mrejesho.
Ili mtu ateuliwe na awe waziri mkuu wa Taifa letu ni lazima mtu huyo awe mbunge aliyechaguliwa kutoka jimboni moja kwa moja na siyo kuteuliwa na Rais kupitia zile nafasi kumi,.na ili mtu awe mbunge ni lazima awe mwanachama wa chama cha siasa na awe amependekezwa na chama husika kugombea na kupeperusha bendera ya chama husika katika uchaguzi. Mpaka hapa unaona na kuelewa ni nani mkubwa kati ya chama na waziri mkuu,maana kuufikia uwaziri mkuu ni lazima uwe kwanza mbunge wa kuchaguliwa ambapo ni lazima uwe umetokana na chama cha siasa. Kwa hiyo waziri Mkuu ni mdogo kwa CCM na anapaswa kutekeleza maagizo ya CCM.
Kwa kuelewa zaidi chukua katiba yetu na soma ibara ya 51 ili kuyaelewa vyema haya niliyoandika hapa. Maana naona kuna watu wanafanya kukurupuka na kuropoka sana kutokana na uelewa mdogo wa katiba yetu na kuwa wavivu wa kusoma katiba yetu,wengine ni wasomi lakini wavivu wa kusoma katiba na kuingia kwenye mkumbo wa kuongea vitu pasipo kuelewa katiba inasema nini.
Lakini pia kwa mujibu wa ibara ya 39 ya katiba yetu imeeleza wazi wazi kuwa ili mtu awe Rais wa Taifa letu ni lazima awe mwanachama wa chama cha siasa na awe amependekezwa na chama husika kupeperusha bendera ya chama chake.mpaka hapa unaona pia hata Rais mwenyewe ni mdogo kwa chama na kwamba anapaswa Kufuata ,kutii, kutekeleza na kutimiza maelekezo ya chama chake.kwa hiyo chama kinauwezo wa kumuagiza hata Rais kufanya na kutekeleza jambo lolote lile lenye maslahi kwa Taifa letu na watanzania wote kwa ujumla wake. Maana mtu hawezi kuwa Rais kama hana chama hata kama mtu huyo anapendwa kiasi gani.hatuna mgombea binafsi katika nchi yetu.
Ikumbukwe na kueleweka ya kuwa chama ndicho huunda serikali,lakini katu na kamwe serikali haiundi chama. CCM ndiyo iliyounda serikali na siyo serikali iliyoiunda CCM,kwa hiyo serikali ipo chini ya CCM kwa kutekeleza ilani ya CCM.
CCM Ndio huenda na kupanda majukwaani kuomba kura kwa wananchi na kunadi ilani yake. CCM Ndio hupigwa vumbi,jua na kutoka jasho majukwaani ili kuomba ridhaa ya watanzania kuongoza nchi .kwa hiyo watendaji wote wa serikali wana wajibu wa kutekeleza ilani ya CCM kikamilifu. Na CCM inapaswa kuhakikisha kuwa hakuna uzembe unafanyika na mtendaji yeyote yule wa serikali katika utekelezaji wa ilani yake.hakuna cha nani wala nani linapokuja suala la utekelezaji wa ilani yake, ni lazima iwe kali na mbogo maana ni CCM Ndio itakayokwenda kuulizwa na wananchi imefanya nini katika miaka mitano iliyokuwa imepewa kuongoza Taifa letu.
Kabla ya kulalamika lalamika tuwe tunasoma kwanza katiba yetu ,tuwe tunatafuta kwanza taarifa sahihi,ukweli wa mambo,tuwe watafiti ,tuwe wafuatiliaji wa mambo na siyo kukaririshwa vitu kama makasuku na wapotoshaji .tunahitaji kuwa na utamaduni wa kusoma mambo ili kujenga ufahamu wa mambo mengi.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.