Watanzania wanaotumia LinkedIn ni washamba

Watanzania wanaotumia LinkedIn ni washamba

Ndio maana tukasema watanzania hawajui matumizi ya Linkedin.
Kwa hayo majibu unayotoa ndio inadhihirisha wazi kwamba maneno ya mtoa mada ni kweli.
Haiwezekani niwaombe connections Directors/CEOs wa nchi mbalimbali wa Kenya,Dubai,Pakistan,Oman,Qatar na wana accept requests bila mashaka halafu wewe kapuku umeajiriwa sijui ni office clerk/administrator ndio uniogope kukubali request yangu na kuanza kunata kwa kipi cha maana ulichonacho au una kitu gani cha kuibiwa/kutapeliwa?
Mkuu wewe ni mgeni sana mitandao kama hiyo na una attitude ya kishamba sana.
Kukubali ovyo ovyo hizo request bila mpangalio zinaleta noise sana kiasi unaweza kukosa kusoma au kufuatilia jumbe au habari muhimu toka kwenye connection zenye faida kibiashara kwako au mambo mengine muhimu kwako.

Zinajaa invitation za ajabu na matangazo ya kipuuzi mengi, huko inbox kuna jamaa wanatuma maombi kibao ya kazi kama wewe ni mtu wa recruitment. Unsolicited job applications kama takataka.

Labda profile yako in info very insignificant kiasi kwamba hupati kero hizi ndiyo maana huwaelewi watu wanachagua watu wa kuwakubalia request zao.

Kama haujui hata internet scammers wapo wengi huko Linkedin kama mitandao mingine.
 
Acha kutufokea, ki tecno changu, bando langu, acc yangu, tena mi kule wala sihangaikagi na makampuni mi naangaliaga pisi nzuri nzuri tu naziomba connection, nina connection hadi na kile kidemu chembambaa sijui ni mkewe sijui mdogo wake na Mo, kajinga nishakatongoza sana kalijibu mara moja tu[emoji26]
 
Umenikumbusha miaka iyo mtu akiwa FB anajiona mjanja hatare. Sasa leo wameanza wa Linkedin
 
Hapa inawezekana kuna recruiters na HR clerks wamepewa kazi kutafuta candidates, sasa wanashindwa kufikisha malengo, wanataka kuingia kwenye profiles za watu kwa nguvu.

Mimi binafsi recruiters wananisumbua sana.

Wanajaza email yangu na simu wananipigia sana mpaka inakuwa kero.

Sasa ukiwa mtu kama mimi, ukiwa na profile ya LinkedIn, kukataa kero za recruiters, inabidi uwe selective sana katika watu unaowakubali katika network yako.

Mimi sipo LinkedIn lakini nasumbuliwa sana na recruiters. Kuna kipindi kila siku nilikuwa napata angalau simu tano na email ndiyo hazina idadi.I can imagine usumbufu kuongezeka maradufu kama ningekuwa LinkedIn.

Halafu linakuja jitu halinijui silijui linataka kuniambia habari zake tu lina impose a narrow wordview yake, kwamba wanaokataa network kubwa wote ni washamba.
Umetumia nguvu kubwa sana kuandika mambo ya msingi sana. Unfortunately unampigia mbuzi gitaa. Wapongeze tu halafu yanakuwa yameisha. Usikute huko LinkedIn kaingia mwaka huu ndio anataka kutuonyesha kuwa naye Yupo!
 
Sio kila mtu aliyeko LinkedIn anatafuta kazi,wengine wanafanya marketing,consultancy n.k
Ninachokiona mshkaji unateseka San. .
Si kila mtu anaweka social media Priority,
BTW kwanini unafikiri ni vema kuhangaika na LinkedIn wakat tayar una kaz na Inakulipa vizur?
Si kila mtu anafikiria kuhama kila mara ...
 
Jamani mifumo yetu ya maisha ki digitali kwa sisi watanzania bado hatujatayarishwa nayo hasa vizazi vya nyuma na kati labda kwa vizazi vya sasa Ndio vinaeza kwenda na speed nzuri ya ki maisha kimitandao.Mkumbuke tu Haya mambo ya internet yameanza sio miaka mingi hapa kwetu Kwa Hiyo twendeni taraatibu tu.Tutafika.
 
Kwani kuna mashindano kwamba ni lazima uwe na connection ya kuanzia 1,000 kwenda juu? Ni moja ya masharti kule LinkedIn kwa kila mwanachama? [emoji15][emoji15][emoji15]
Huwa ina shangaza sana kuna watu wengine wasipopata followers wana kuwa inferior kabisa
.badhani ni kutojikubali tu
 
Habarini za leo wakuu,

Leo nimeona niwaletee mada hii wakuu.

Katika uchunguzi wangu niliofanya Linkedln nimegundua watanzania wenye akaunti LinkedIn

1. Ni washamba kwa maana kwamba hawajui maana ya mtandao wa LinkedIn

2. Profile zao za kitoto kwa maana kwamba hazivutii kabisa. Hawaja zipambanua vya kutosha, sijui wanakwama wapi.

3. Ukiwaomba urafiki hawakubali ni washamba sana. Wanadhani ule mtandao ni sawa na facebook.

4. Hasa hawa wanaofanya kazi kwenye vikampuni na vitaasisi vizuri ndio wanao jidai zaidi kwa vile wapo makazini basi hawaoni haja ya kutumia LinkedIn zaidi. Ila siku wakitumbuliwa ndio wanaanza kukuru kakara za kutafuta connection LinkedIn

5. Wanajiona sana na ndio sababu hawakubali kuwa na connection na watu wengine. Ndio sababu utakuta jitu lina connection ya watu 10 kwenye LinkedIn yake. Huu ni ushamba wa hali ya juu na ni aibu.
Wewe unadhani mtu akikuomba urafiki anakuomba kazi sio, acheni ushamba dunia imebadirika hii.

Mtu kama Bill gates tajiri wa dunia ana connect hadi na wakulima waliopo afrika wala hajali anaelewa nini maana ya LinkedIn.

6. Sijui shida iko wapi kwa watanzania wenzangu. Nyie mlio makazini mnakwama wapi kujipambanua kwenye account zenu za LinkedIn.

Wakuu nisaidie kuwaponda hawa watu mimi nimeishia hapa.

Watanzania wa LinkedIn wanaboa sana.

Utakuta kijamaa kinafanya kikazi cha mshahara laki saba basi kinavimba kichwwaaaaaaaa. Ukikiomba urafiki hakikujibu kinakaa kimya tu.

Je ungekuwa na mishahara kama ya kwetu ungefika wapi wewe.

Funguka acha ushamba wenzako tunachati na akina Jenifer Lopez Linkedln tunashauriana mambo mbalimbali.

Acheni ushamba na vikazi vyenu vya mishahara ya mboga.
wewe tafuta wambea wenzako,unalizimisha connection ,ubnormal kweli wewe.
 
Aibu ni pale unapotaka kulazimisha kila mtu afanye kama unavyotaka wewe.

Unaelewa kwamba kila mtu ana historia tofauti, na unapoona wewe umejua leo, watu wengine wameshapita miaka ya tisini huko?

Watu tumeona Geocities Rings, nini LinkedIn?

Unaelewa Geocities Rings ni nini na zilikuwepo kwenye internet mwaka gani mpaka mwaka gani?

Unaelewa security risks za LinkedIn?

Unaelewa identity theft ni nini?

Unaelewa commoditization of social media data ni nini?

Unaekewa kwamba wewe ukiwa unakaa kwenye matako ya dunia unaweza ku afford data zako kuwa all over the place, lakini kuna watu wako duniani kwenye high security risk na identity theft, na LinkedIn ni source ya information nyingi sana kwa identity thieves?

Unaelewa profiling?

Unaelewa kwamba wewe na mimi hatuishi dunia moja?
Usijisumbue hawezi kuelewa . She/ he is too immature
 
Hakuna mtu nimemlazimisha kuniunga urafiki ila tulikuwa tunapeana mawaidha na kuwafundisha umuhimu wa kuwa na connections nyingi Linkedin.
Wewe ukikataa kuaccept request yangu hujanikomoa maisha yangu yatabaki yaleyale.
Na wewe ukipata connection 5000 inakusaidia nini na watu huwajui huna tija wala skillset wala elimu wala experience inakusaidia nini kwenye maisha yako?
 
Na wewe ukipata connection 5000 inakusaidia nini na watu huwajui huna tija wala skillset wala elimu wala experience inakusaidia nini kwenye maisha yako?
Sio itanisaidia nini imeshanisaidia sana tu with accordance to my CV.
Thus why nawashangaa watanzania wenzangu kutojua umuhimu wa Linkedin.
Ukubwa wa CV na kujitangaza ni vitu vinategemeana.
Imagine mtu awe na CV nzuri halafu awe amejifungia huko namtumbo na kisimu cha tochi atamjua nani na CV yake.
 
Mimi ninao 2000+ nina update profile mara kibao na ni jobless vilevile sasa sijui nakwama wapi?
Umeitumiaje hiyo profile kuwafikia recruiters? Kuna namna nyingi za kuongeza visibility kwa potential employees. Mfano kuchangia kwenye posts zenye mwelekeo wa fani yako ukawashirikisha ujuzi wako ni moja ya njia hizo. Kuna na nyingine nyingi.

Fanya homework yako kujua unafeli wapi...
 
Back
Top Bottom