Watanzania wanaotumia LinkedIn ni washamba

Watanzania wanaotumia LinkedIn ni washamba

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
9,263
Reaction score
12,197
Habarini za leo wakuu,

Leo nimeona niwaletee mada hii wakuu.

Katika uchunguzi wangu niliofanya Linkedln nimegundua watanzania wenye akaunti LinkedIn

1. Ni washamba kwa maana kwamba hawajui maana ya mtandao wa LinkedIn

2. Profile zao za kitoto kwa maana kwamba hazivutii kabisa. Hawaja zipambanua vya kutosha, sijui wanakwama wapi.

3. Ukiwaomba urafiki hawakubali ni washamba sana. Wanadhani ule mtandao ni sawa na facebook.

4. Hasa hawa wanaofanya kazi kwenye vikampuni na vitaasisi vizuri ndio wanao jidai zaidi kwa vile wapo makazini basi hawaoni haja ya kutumia LinkedIn zaidi. Ila siku wakitumbuliwa ndio wanaanza kukuru kakara za kutafuta connection LinkedIn

5. Wanajiona sana na ndio sababu hawakubali kuwa na connection na watu wengine. Ndio sababu utakuta jitu lina connection ya watu 10 kwenye LinkedIn yake. Huu ni ushamba wa hali ya juu na ni aibu.
Wewe unadhani mtu akikuomba urafiki anakuomba kazi sio, acheni ushamba dunia imebadirika hii.

Mtu kama Bill gates tajiri wa dunia ana connect hadi na wakulima waliopo afrika wala hajali anaelewa nini maana ya LinkedIn.

6. Sijui shida iko wapi kwa watanzania wenzangu. Nyie mlio makazini mnakwama wapi kujipambanua kwenye account zenu za LinkedIn.

Wakuu nisaidie kuwaponda hawa watu mimi nimeishia hapa.

Watanzania wa LinkedIn wanaboa sana.

Utakuta kijamaa kinafanya kikazi cha mshahara laki saba basi kinavimba kichwwaaaaaaaa. Ukikiomba urafiki hakikujibu kinakaa kimya tu.

Je ungekuwa na mishahara kama ya kwetu ungefika wapi wewe.

Funguka acha ushamba wenzako tunachati na akina Jenifer Lopez Linkedln tunashauriana mambo mbalimbali.

Acheni ushamba na vikazi vyenu vya mishahara ya mboga.
 
Ni kweli mkuu hata mimi nimeona hilo,hawajui maana ya huu mtandao.
mwingine amejiunga tu lakini hajui matumizi yake.

Watu wa kenya na ghana wanautumia vizuri huu mtandao maana hata kama wana kazi bado wanautumia vizuri muda wote same to me.

Utakuta kimtu kinafanya kazi tigo au voda na kimshahara chake cha laki 7 anavimba kichwa na hataki kupokea request utafikiri labda utamuibia au kumtapeli wakati hana mbele wala nyuma.

Bongo bado tuko nyuma sana kwenye haya mambo
 
Umomba connection kwa watanzania wote wenye account LinkedIn ukaona wanatabia sawa! Isije ikawa wewe ndio una matatizo maana ili mtu akukubali lazima muwe na skills, qualification zinazofanana. Jipambanue zaidi kwenye eneo la skills and qualification utapata wa kufanana na wewe.
 
Umomba connection kwa watanzania wote wenye account LinkedIn ukaona wanatabia sawa! Isije ilawa wewe ndio una matatizo maana ili mtu akukubali lazima muwe na skills, qualification zinazofanana. Jipambanue zaidi kwenye eneo la skills and qualification utapata wa kufanana na wewe.
Mkuu ingia LinkedIn utafute mtanzania mwenye connection ya watu kuanzia 1000 kwenda juu, ni wakuhesabika mkuu na wanafahamika
 
ushamba uliousemea na ulichokiandika hapa ni mbingu na ardhi.
 
Back
Top Bottom