Watanzania wanaotumia LinkedIn ni washamba

Watanzania wanaotumia LinkedIn ni washamba

Mimi nitakataa vipi request yako wakati LinkedIn sina, sitakuwa nayo na wala siihitaji?

Na unaanzaje kumfundisha mtu kwa attitude ya kwamba ni mshamba, ilhali humjui na hujui sababu zake za kukataa kuwa na network kubwa?

Kwa nini unafikiri kuwa na network kubwa ni muhimu kwa kila mtu?

Unaelewa kuna watu wanajali quality kuliko quantity?

Mkuu umeongea mambo ya msingi sana

Mtoa mada ameleta majivuno na kusimanga watu bila sababu za kimsingi

Halafu amejigamba ana mshahara mkubwa, sasa hiyo ina muhimu gani kwa watu ambao hawana maslahi na huo mshahara? Je mshahara mkubwa unaanzia kiasi gani?
 
Kumbe hizi hoja zote zimekuja baada ya kuambiwa ni washamba?usipaniki hilo ni neno la kawaida tu na mtu yeyote aweza kuwa mshamba mahali fulani.
Kwa mfano mimi ni mtoto wa mjini nimezaliwa dar town ila nikienda kijijini na wao wanaweza kuniona mimi mshamba kwa sababu kuna vitu vyao vya shamba mimi sivijui.
Kulazimisha mtu mwingine aishi kama wewe unavyotaka ni kitu kibaya sana.

Halafu kizabizabina cha kutaka kuwapa ushauri watu ambao hawajakuomba ushauri ni tabia ya ajabu sana.

Waacheni watu watumie account zao wanavyotaka.

Wewe mtu unayependa mtandao wa watu wengi akija mtu kukwambia futa connections zako zote ubaki na mbili tu, utaona sawa?

Acheni superioriry complex kwenye maisha ya watu baki ambao hawawajui na wala hawajawaomba ushauri.

Hii tabia ya kufuatiliafuatilia maisha ya watu msiowajua nayo ni ushamba.
 
Mkuu umeongea mambo ya msingi sana

Mtoa mada ameleta majivuno na kusimanga watu bila sababu za kimsingi

Halafu amejigamba ana mshahara mkubwa, sasa hiyo ina muhimu gani kwa watu ambao hawana maslahi na huo mshahara? Je mshahara mkubwa unaanzia kiasi gani?
Werevu hawajigambi kwa mshahara.

Niambie kuhusu patents, stocks, assets, investments.Real Estate. Ownership.

Anajigamba kwa mshahara?

Na sisi trust fund babies tutasema nini?
 
Hapa inawezekana kuna recruiters na HR clerks wamepewa kazi kutafuta candidates, sasa wanashindwa kufikisha malengo, wanataka kuingia kwenye profiles za watu kwa nguvu.

Mimi binafsi recruiters wananisumbua sana.

Wanajaza email yangu na simu wananipigia sana mpaka inakuwa kero.

Sasa ukiwa mtu kama mimi, ukiwa na profile ya LinkedIn, kukataa kero za recruiters, inabidi uwe selective sana katika watu unaowakubali katika network yako.

Mimi sipo LinkedIn lakini nasumbuliwa sana na recruiters. Kuna kipindi kila siku nilikuwa napata angalau simu tano na email ndiyo hazina idadi.I can imagine usumbufu kuongezeka maradufu kama ningekuwa LinkedIn.

Halafu linakuja jitu halinijui silijui linataka kuniambia habari zake tu lina impose a narrow wordview yake, kwamba wanaokataa network kubwa wote ni washamba.
 
Habarini za leo wakuu,

Leo nimeona niwaletee mada hii wakuu.

Katika uchunguzi wangu niliofanya Linkedln nimegundua watanzania wenye akaunti LinkedIn

1. Ni washamba kwa maana kwamba hawajui maana ya mtandao wa LinkedIn

2. Profile zao za kitoto kwa maana kwamba hazivutii kabisa. Hawaja zipambanua vya kutosha, sijui wanakwama wapi.

3. Ukiwaomba urafiki hawakubali ni washamba sana. Wanadhani ule mtandao ni sawa na facebook.

4. Hasa hawa wanaofanya kazi kwenye vikampuni na vitaasisi vizuri ndio wanao jidai zaidi kwa vile wapo makazini basi hawaoni haja ya kutumia LinkedIn zaidi. Ila siku wakitumbuliwa ndio wanaanza kukuru kakara za kutafuta connection LinkedIn

5. Wanajiona sana na ndio sababu hawakubali kuwa na connection na watu wengine. Ndio sababu utakuta jitu lina connection ya watu 10 kwenye LinkedIn yake. Huu ni ushamba wa hali ya juu na ni aibu.
Wewe unadhani mtu akikuomba urafiki anakuomba kazi sio, acheni ushamba dunia imebadirika hii.

Mtu kama Bill gates tajiri wa dunia ana connect hadi na wakulima waliopo afrika wala hajali anaelewa nini maana ya LinkedIn.

6. Sijui shida iko wapi kwa watanzania wenzangu. Nyie mlio makazini mnakwama wapi kujipambanua kwenye account zenu za LinkedIn.

Wakuu nisaidie kuwaponda hawa watu mimi nimeishia hapa.

Watanzania wa LinkedIn wanaboa sana.

Utakuta kijamaa kinafanya kikazi cha mshahara laki saba basi kinavimba kichwwaaaaaaaa. Ukikiomba urafiki hakikujibu kinakaa kimya tu.

Je ungekuwa na mishahara kama ya kwetu ungefika wapi wewe.

Funguka acha ushamba wenzako tunachati na akina Jenifer Lopez Linkedln tunashauriana mambo mbalimbali.

Acheni ushamba na vikazi vyenu vya mishahara ya mboga.
Tune ya andiko lako Ni Kama umekata,tamaa, una msongo ...Sasa sijui huwa mnachati Nini na Jeniffer Lopez,Usije ukaanzs mtusi!
 
Mimi ni mtumiaji wa Linkedin. Haya ndo ambayo nashauri mtu ufanye kabla hujaomba connection na mtu mwingine. Hakikisha ume update profile yako na imekaa ki profession. Unakuta mtu kaandika kwenye profile yake kwamba kasoma "Street University" au profile ipo tupu, hivi kuna mtu yoyote atakubali ku accept connection yako? Nafikiri kabla ya kulaumu ni vyema tujikague wapi tunakosea. Namba mbili unapotaka connection na mtu lazima kuwe na sababu, ile sio kama Facebook. Sababu inaweza ikawa mnafahamiana au unaona kuna kitu mnashare katika professions zenu na ingekuwa vyema muunganike. Ni hayo tu
 
Mtu anayekuja hapa na kuleta kashfa za jumla kwamba Watanzania ni washamba, mpaka hapo tu kashajionesha hayuko professional na naweza kuelewa kwa nini watu wanamkataa huko LinkedIn.

Mtu professional hata kama kaona watu kweli washamba, na watu ni washamba kweli, presentation yake inatakiwa iwe helpful, isiwe ya kuwazodoa watu kwa majivuno, itoe mafunzo kwa heshima na unyenyekevu.
 
Kama hujanufaika mpaka unataka zaidi, tafakari, chukua hatua
Mimi nanufaika sana kupitia LinkedIn, ila natumia LinkedIn kujijengea umaarufu. Kuonyesha uwezo wangu, kuionyesha dunia na Tanzania kwa ujumla kwamba inavijana bado wa kuijenga ili kuonyesha positive impact.
 
Werevu hawajigambi kwa mshahara.

Niambie kuhusu patents, stocks, assets, investments.Real Estate. Ownership.

Anajigamba kwa mshahara?

Na sisi trust fund babies tutasema nini?
Ah ah waache watoto wa liomaliza chuo Hapa karibuni.....kwanza LinkedIn hawashauri kua na connection nyingi zisizokusaidia...kila baada ya mda wananiletea option ya kupunguza nisiowajua..Sasa Hawa watoto wanachukulia linked Kama Instagram.....
 
Habarini za leo wakuu,

Leo nimeona niwaletee mada hii wakuu.

Katika uchunguzi wangu niliofanya Linkedln nimegundua watanzania wenye akaunti LinkedIn

1. Ni washamba kwa maana kwamba hawajui maana ya mtandao wa LinkedIn

2. Profile zao za kitoto kwa maana kwamba hazivutii kabisa. Hawaja zipambanua vya kutosha, sijui wanakwama wapi.

3. Ukiwaomba urafiki hawakubali ni washamba sana. Wanadhani ule mtandao ni sawa na facebook.

4. Hasa hawa wanaofanya kazi kwenye vikampuni na vitaasisi vizuri ndio wanao jidai zaidi kwa vile wapo makazini basi hawaoni haja ya kutumia LinkedIn zaidi. Ila siku wakitumbuliwa ndio wanaanza kukuru kakara za kutafuta connection LinkedIn

5. Wanajiona sana na ndio sababu hawakubali kuwa na connection na watu wengine. Ndio sababu utakuta jitu lina connection ya watu 10 kwenye LinkedIn yake. Huu ni ushamba wa hali ya juu na ni aibu.
Wewe unadhani mtu akikuomba urafiki anakuomba kazi sio, acheni ushamba dunia imebadirika hii.

Mtu kama Bill gates tajiri wa dunia ana connect hadi na wakulima waliopo afrika wala hajali anaelewa nini maana ya LinkedIn.

6. Sijui shida iko wapi kwa watanzania wenzangu. Nyie mlio makazini mnakwama wapi kujipambanua kwenye account zenu za LinkedIn.

Wakuu nisaidie kuwaponda hawa watu mimi nimeishia hapa.

Watanzania wa LinkedIn wanaboa sana.

Utakuta kijamaa kinafanya kikazi cha mshahara laki saba basi kinavimba kichwwaaaaaaaa. Ukikiomba urafiki hakikujibu kinakaa kimya tu.

Je ungekuwa na mishahara kama ya kwetu ungefika wapi wewe.

Funguka acha ushamba wenzako tunachati na akina Jenifer Lopez Linkedln tunashauriana mambo mbalimbali.

Acheni ushamba na vikazi vyenu vya mishahara ya mboga.
Ulipo generalise nimekufahamu wewe ni kiumbe wa aina gani
 
Mi naona mleta mada ndiye mshamba
Angekuwa na busara angeeleza faida za kuwa na connection nyingi linkeldin. Badala yake kaonyesha chuki na wivu wa kunyimwa connections.
 
Jiangalie wewe usije ukawa ndiye mwenye tatizo hilo. Unawezaje kwenda kuomba urafiki LinkedIn? Unalazimishaje kila mtu akubali kuwa rafiki na kila mtu? Kule ni mahala pa kazi. Na ndiyo sababu mtu kabla hajarespond kwanza anaangalia profile yako kama inatija katika shughuli zake.

Ndiyo sababu wasimamizi wa LinkedIn wanakuambia omba connections na watu unaowafahamu siyo kuvamia vamia. Au uombe introduction na siyo kuparamia. Ukiona mtu kanyamaza hajakujibu ujue anajiheshimu vinginevyo angeweza kukujibu tofauti. Hapo siyo Instagram wala Facebook.

Kule watu wanatafuta maarifa na influence wewe unakwenda kutafuta urafiki.

Ushauri wangu, kama lengo lako ni kutaka marafiki huko si mahala pako.
Washamba wanaozungumzwa mshaibuka[emoji1][emoji1]
 
Sawa tumejua una unamshahara mkubwa.
Nilifikiri utasema unagawio kubwa.
 
Mi naona mleta mada ndiye mshamba
Angekuwa na busara angeeleza faida za kuwa na connection nyingi linkeldin. Badala yake kaonyesha chuki na wivu wa kunyimwa connections.

Stress zitawaua vijana. Mtoa mada anaonyesha chuki ya wazi. Majigambo mengi kumbe mtumwa sema ana mshahara mkubwa.
 
Wewe sijui ni wa nchi gani lakini hebu tupe solution badala ya kuponda tu bila kutoa suluhisho
 
Endeleeni kuupa promo huu mtandao utashangaa juma lokole naye kajiunga.
 
Back
Top Bottom